Apitakujilamba
JF-Expert Member
- Sep 27, 2013
- 205
- 83
Habarini wanajamviini, HERI YA MWAKAMPYA naomba leo nije na mada inayohusu Upendo.
Wilhelm Luetgert anaandika katika ‘Maadili ya Upendo':Amri ya kupenda inaonesha kwamba upendo ni wajibu. Upendo unaamriwa na ni utii. Mwanafalsafa wa Kijerumani Immanuel Kant anampinga Luetgert na kusema kwamba waweza tu kuamurumatendo ya nje, na si upendo. Kant anaendelea kusema, upendo ni maamuzi ya dhamiri huru na hisia za ndani kabisa na pia upendo ni kitu tusichoweza kukitengeneza. Kuna aina nne za Upendo katika maisha ya binadamu, kama ninavyoanisha hapo chini:
Upendo kwa mzazi na mtoto. Huu ni upendo asilia ambao mzazi anakuwa nao kwa mtoto wake na vivyo hivyo unakuwepo kwa mtoto. Tunaamini Mungu ni mzazi wa wanadamu wote na ana upendo kwa watu wote ndivyo hivyo aliumba upendo wa kipekee kwa mzazi kwa mtoto wake. Mara nyingi najiuliza ingekuwaje bila ya upendo huu wa mzazi kwa mtoto na mtoto kwa mzazi. Ingawa kuna wazazi wachache sana hawana upendo huu.
Upendo unaotokana na vitu ambavyo tunavipenda, maslahi na hobi (interests and hobies). Kuna wakati mtu anajikuta anampenda mtu kwa sababu wana maslahi au hobi zinazofanana. Mfano mtu anapenda kuimba basi atajikuta anampenda mtu kwa sababu ya uimbaji, vivyo hivyo na fani nyingine. Ndio maana kuna ndoa nyingi za namna hiyo yaani fani zinazofanana kama vile wasanii wa filamu, wanamuziki, madaktari, wahadhiri, wanamichezo, wachungaji. Hii inatokana na kuvutiwa na fani zao na pia uwepo wa ukaribu kutokana na fani na hobi zao.
Upendo unaotokana na muonekano au maumbile ya mtu. Kuna watu wengi tunajikuta unampenda mtu kwa muonekano wake. Mungu ameumba watu tofauti tofauti, kuna weupe, weusi, warefu, wafupi, sura mviringo, sura yai. Hapo kila mtu anachaguo lake. Hapa ndipo kuna mtego mkubwa kwenye upendo, watu wengi tumejikuta tukivutwa na muonekano au umbile la mtu. Kwa wanaume utaona wamejikita kwenye sura nzuri, tarakimu namba nane, miguu ya bia, makalio yalibinuka n.k. Wakati kwa wanawake wamejikita kwenye sura nzuri, urefu, mwili uliojaa na tumbo bapa lililogawanyika katika vipengele sita n.k.
Upendo wa Agape. Huu ni upendo asilia ambao mtu anakuwa nao ambao unatiririka moyoni. Upendo huu mara nyingi unakuwa hauna sababu, unakuta anyependwa siyo mzazi, hana maslahi au hobi zinazofanana na wala sio kwa sababu la umbile au muonekano. Upendo huu unaweza ukauona kwa Adamu ambaye alimpenda Hawa kwa jinsi alivyo vivyo hivyo kwa mtoto wa Ibrahimu aitwae Isaka alimpenda Rebecca kwa jinsi alivyo.
Hata leo naamini kila mtu katika nyakati fulani katika maisha tunakutana na mtu tunampenda tu bila sababu maalumu lakini kuna vitu vinakuwa vinatukwamisha. Moja ya vitu hivyo ni ndoto, mara nyingi tunakuwa tumeshajiumbia watu ambao tunataka kuwa nao katika maisha yetu, kwa hiyo anapotokea mtu ukajikuta unampenda lakini hayupo kama alivyo mara nyingi tunatumia nguvu nyingi kumkataa. Sababu nyingine ni marafiki huwa ni kikwazo kikubwa katika kumkubali mtu umpendae, mara nyingi tunajiuliza hivi rafiki yangu atanionaje n.k.
Angalizo, upendo wa agape aimanishi kwamba mtu hawezi kupenda mtu mwenye hobi sawa na yake au mwenye hela nyingi au wenye muonekano na umbile zuri. Inawezekana ukampenda mtu bila sababu yoyote yaani upendo wa agape bila kuweka kwanza hivyo vivutio hivyo kwanza.
Tofauti kati ya aina ya 2, 3 na 4 za upendo itajidhihirisha hasa baada ya ndoa na muda kupita, pale ambapo umeshaizoea sura ya mwandani wako, pale ambapo fani zinazofanana sio tija tena, pale ambapo sura nzuri imeanza kupata makunyazi, pale ambapo tarakimu namba nane imegeuka kuwa moja, pale ambapo tumbo paba lililogawanyika vipande sita limegeuka na kuwa kitambi, mshahara wa mamilioni umekwenda mpaka tuelfu. Hapo ndio upendo utakapodondoka kutoka asilimia 100 mpaka 0. Wengi huanza kujilaumu kwa nini wameoa au wameolewa na hao wapenzi wao. Lakini ni tofauti na upendo wa agape ambao wenyewe huzidi kukua kadiri siku zinavyoenda haijalishi changamoto wanazopitia. Upendo huvumilia, upendo haungaliii mabaya.
Naomba nimalizie na kipengele cha wimbo wa Ambwene Mwasongwe, NDOA NI KAMA JUA. IKIWA ASUBUHI WATU WENGI WANALITAMANI NA KULILIA NA PIA WANALISIFIA KUWA LINA VITAMINI, JUA HILO HILO WAKATI WA MCHANA WATU HULICHUKUA NA KULIKIMBIA KWA KUSEMA NI KALI MNO NA IKIFIKA JIONI WATU HULITAMANI HILO JUA.
Source: Mimi, Thomas Schrirmacher na Glenda
WAKATABAHU