Natabiri serikali kupiga marufuku Press Conferences

Second July

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
234
323
Wiki hii serikali ya awamu hii ilipata pigo kubwa baada ya Tundu Lissu kuibua sakata la kuzuiwa kwa ndege yetu huko Canada na wadeni wetu.
Hakika kuvuja kwa taatifa hii na kupelekwa moja kwa moja kwa wananchi tena kupitia kwa mbaya wa serikali (TL) imewanyong'onyesha sana chama dola na serikali. Suala hili limezua taharuki ndani ya chama na serikali na kuona kama wamevuliwa nguo baada ya kulifanya kuwa siri na baadae kufichuka. Hii imepelekea majibu tofuti tofaut toka ndani ya serikali, chama na wasomi wanaovizia kuteuluwa na serikali ktk nyazifa mbalimbali.

Serikali sikivu na ya wanyonge inayowahurumia masikini (kama inavyojinasibu) haiwez kuvumilia kuvuliwa nguo kiasi hiki. Ss hiv inafanya jitihada za hali ya juu kuwapata wote waliovujisha habari hii na sasa imeshaweka mikakati ya kuhakikisha jambo la namna hii halitaweza kutokea tena. Mkatakati wa kwanza ni ule utakaotangazwa hivi karibuni wa kupiga marufuku press conference yeyote ile mpaka upate kibali toka polisi (rpc) au kwa kwa vibaraka wakuu wa serikali (wakuu wa ilaya - DC). Ikumbukwe wanasiasa wa upinzani wameshabanwa kuongea kuptia Bungeni ( no bunge live na maagizo kwa Spika na Naibu wake kuwabana wapinzani kuzungumza) na kuzuia mikutano ya hadhara. Hii threat ya Press Conference walikuwa hawajaiona mpk pale TL alipowavuruga wikii hii.

Sasa muda mwafaka wa serikali ya wanyonge na watu masikin kuzuia Press cobference yeyote mpk kibali umewadia. Stay Tuned. Awamu hii tutayaona mengi sana ambayo tulikuwa hata hatuyafikirii kuyokea nchini kwetu. Na awamu hii itakuja kuwa awamu mbaya zaidi iliyowahi kutokea TZ kisiasa na kiuchumi.
 
Bora kabisa maana kuna baadhi ya watu wakiwekewa mic nyingi mbele yao akili zinawaruka na kuanza kuropoka hovyo kama wenda wazimu
 
Ninahakika waziri wa habari atapiga marufuku press conference.
Je litakuwa ni suluhisho la kudumu?
 
Bora kabisa maana kuna baadhi ya watu wakiwekewa mic nyingi mbele yao akili zinawaruka na kuanza kuropoka hovyo kama wenda wazimu
Kwhy hata sisi tukiwa na press conference ya kutambulisha bidhaa yetu mpya sokoni itabid tumwone DC, OCD au RPC.
Poor you...
Mnaturudisha miaka themanini na tisini ya Ukaburu SA.
 
Bora kabisa maana kuna baadhi ya watu wakiwekewa mic nyingi mbele yao akili zinawaruka na kuanza kuropoka hovyo kama wenda wazimu
Yule anayezunguka nchi nzima akilalamika na kuongea upuuzi kumbe ni mic zinamsumbua!!!!

Ama kweli waogope kupanda ndege,waogope kiingereza,wamwogope Lissu na hili nalo walitolee tamko,madaktari mbadilishieni kichaa dozi zimemzidi
 
  • Thanks
Reactions: 999
Ninahakika waziri wa habari atapiga marufuku press conference.
Je litakuwa ni suluhisho la kudumu?
Nikikumbuka walovyotumia nguvu nying kumzuia Nape kufanya press conference lkn mwisho wa siku akaifanya akiwa juu ya gari, nikikumbuka walivyomuweka kizuizin katibu wao Kinana asiongee na waandishi wa habari, yani naona kabisa adhabu kali kwa chombo chochote kile kitakachorusha habari ama kuchapisha habari yyt ile kutoka press conference isiyokuwa na kibali.
 
Press Conference nazo zina mipaka yake. Haki ya kufanya Press Conference inaendana na wajibu wa kuzingatia amani na utulivu. Mara nyingine watu wana abuse haki yao ya kufanya Press Conference. Wengi wameshindwa kutofautisha uhuru wa kutoa maoni na wajibu wa kuzingatia sheria.
 
Kwhy ss hv kila kitu kinavuruga amani nanutulivu eeehh. Hii awamu yenu ya viwanda vip???

Kwanini hampend kuambiwa ukwel lkn???

Kwahiyo mltaka mfiche suala la kuzuiwa kwa ndege kutokana na deni tena lililosababibishwa na kiranja mkuu!!! Yaani mnaitia nchi hasara alafu mnataka tusiambiwe. Mbn mnataka kuturudisha enzi za ujima. Badilikeni dunia inabadirika.

Halafu kwanini kila kitu mkuu anaogopa?? Anakimbia mpk kivuli chake mwenyewe ana tatizo gani?? Kwann hajiamin??
 
  • Thanks
Reactions: 999
Umesahau DW Swahili services na Al Jazeera. Pia kuna utube mahojiano yanafanyika kule kisha kitu kinatambazwa mtandaoni. Akili ndogo KAMWE haiwezi kushinda akili kubwa.

Tutakuwa tunaongea live na BBC au Dutch radio
 
Exactly ndicho kinachotakiwa hatutaki press conference za aina ya Mange.
 
Bora kabisa maana kuna baadhi ya watu wakiwekewa mic nyingi mbele yao akili zinawaruka na kuanza kuropoka hovyo kama wenda wazimu
Uko sawa na Banyamulenge mwenzako,
Dunia hii si ile, msifikiri inarudi nyuma kuwafuatisha mnachotaka.
 
Press Conference nazo zina mipaka yake. Haki ya kufanya Press Conference inaendana na wajibu wa kuzingatia amani na utulivu. Mara nyingine watu wana abuse haki yao ya kufanya Press Conference. Wengi wameshindwa kutofautisha uhuru wa kutoa maoni na wajibu wa kuzingatia sheria.
Hata viwanda vina mipaka yake.
Ndiyo maana kwa Tz cherehani 4 ni kiwanda tosha
 
Back
Top Bottom