Natabiri haya siku 22 kuelekea uchaguzi

kimpango

JF-Expert Member
Apr 24, 2011
600
716
1.Television ya taifa na zingine washirika kumuonesha mwalimu Nyerere mara nyingi zaidi ya siku za nyuma wakiweka hotuba zisizoponda chama tawala lakini zikikaa mrengo wa kukitetea haya yatafanyika kuelekea 14 October kwenye kumbukumbu ya mwalimu

2. Umeme kuwepo siku nzima na nchi nzima siku zifuatazo siku CCM itakapoenda Mwanza na mikoa mingine mikubwa ili watu waweze kuona na kusikia mikutano yao live nchi nzima lakini mgao utaendelea siku wapinzani wap wangu wakipita mikoa hiyo hiyo either wakiwa wametangulia au baadaye.

3. Kukamatwa kwa kiongozi mkubwa wa chama kimoja kwa kosa lililompeleka mbasha au babu seya kortini na kutangazwa sana na vyombo vya habari ikiwemo kuwaweka wazi waathirika wa tukio hilo litapotokea kesi itaisha baadae baada ya uchaguzi.

4. Kulazimishwa kwa kuombwa sana kwa mke wa kiongozi wa kitaifa anayeheshimika kutoa tamko siku ya kilele cha maadhimisho ya marehemu mumewe kwa hotuba fupi itakayoandaliwa au mahojiano yatakayoandaliwa kuonesha kwamba fulani sio chaguo na mengineyo.

5. Kukamatwa kwa watu watakaokuwa na Silaha za kivita wakiitwa"magaidi wenye mafunzo ya kikomandoo"ambao watasema wameletwa na chama kimoja cha siasa kwa shughuli maalumu .kumbuka hawatakuwa watanzania watatoka nchi inayosifika kwa magaidi afrika .

7. Kujitoa au kushawishiwa kujitoa kwa chama kimoja au kiongozi wake mkuu kwa madai ya kutotendewa haki na muungano wao.

8.Wagombea urais wawili au watatu kutangaza kumuunga mkoani mgombea wa chama kingine na Hii wataifanya hadharani siku ya kufunga kampeni kwa hicho chama.

9.Siku ya ufungaji wa kampeni tutashuhudia mwenyekiti wa chama kimoja wenye mamlaka ki nchi akimtuhumu waziwazi na kumtaja jina mgombea wa chama pinzani na washirika wake wakuu kuhusika na ufisadi uliotajwa sana tukio hilo litafanyika na kuoneshwa live na TV na redio nchi nzima na kupewa uzito kwenye magazeti yote kesho yake.

Lakini siku inayofuata ambayo chama tuhumiwa kitataka kujibu mapigo umeme utakatika nchi nzima so hawatakuwa live zaidi ya uwanjani pia magazeti ya siku ya uchaguzi yatawekewa oda ya jumla na tutayapata jioni au tusipate kabisa yatakuwa yameandika habari hizo za kufunga kampeni na majibu ya tuhuma kwa uwazi na vielelezo lakini itakuwa too late.

10. Uchaguzi utagubikwa na fujo kwa karatasi kuchelewa Vituoni, polisi kutumia nguvu kubwa,watu kuvaa tishet za vyama wasivyoshabikia na kufanya vurugu ila tishet hzo ni mpyaaaa.

Baadhi ya vituo watu hawatapiga kura uhesabu wa kura kielectonic utaleta utata mkubwa kwa kutofautiana na uhalisia wa jumla ya kura zote.
Kurudiwa kura sehemu mbalimbali kwa sababu mbalimbali.

Kukamatwa kwa wapiga kura mamluki au wanaotaka kutumika kupigia

MENGINE NITALETA BAADAYE USINIBISHIE KAA UTICK KILA KITAKACHOTOKEA KUTOKANA NA MUDA KAMA NI MDAU CHUKUA TAHADHARI
 
Timu ya UKAWA zingatieni,mleta mada kaleta haya kwa indirect way ila ni kuvujisha mipango ya CCM wanayoiandaa wiki ya mwisho wa kampeni ili kuleta hadaa na taharuki!!!
 
Jamaa kavujisha mipango yote ya lumumba. Lazima utakuwa ni mmoja wapo wa wale ma captain. Wewe ni mzalendo Asante sana maana hata mie nilikuwa na hizi taarifa
 
UKAWA itisheni press conference na mtoe elimu ya kupiga kura kwa wananchi. Asiende mtu mmoja kama Mbatia bali siku hiyo jopo zima liwepo ili kuweka uzito na iwe live.

Vinginevyo, kama wadau walivyosema, uwezekano wa dotCom, bodaboda, na wapiga kura wengine ambao hawana experience kuharibu kura kwa kuweka X kwa wagombea wengine ni mkubwa mno ukizingatia uchaguzi huu ndio wa kwanza wa aina yake kwa watanzania kujitokeza kwa maelfu kupiga kura. Hawana experience na NEC haitaki kuwaelimisha, wasaidieni.
 
UKAWA itisheni press conference na mtoe elimu ya kupiga kura kwa wananchi. Asiende mtu mmoja kama Mbatia bali siku hiyo jopo zima liwepo ili kuweka uzito na iwe live.

Vinginevyo, kama wadau walivyosema, uwezekano wa dotCom, bodaboda, na wapiga kura wengine ambao hawana experience kuharibu kura kwa kuweka X kwa wagombea wengine ni mkubwa mno ukizingatia uchaguzi huu ndio wa kwanza wa aina yake kwa watanzania kujitokeza kwa maelfu kupiga kura. Hawana experience na NEC haitaki kuwaelimisha, wasaidieni.

Usitufanye watanzania mazombi kama ulivyo!kwani zoezi la upigaji wa kura ndo linafanyika Tz kwa mara ya kwanza?
 
Nina imani viongozi wamesha take measure juu ya hili hawa mazombie ccm ni kuwakaba tu koo waishiwe hewa mwisho wajifie rasmi ifikapo tarehe 25. Vingi tu walivyopanga vitachuja MUNGU YU UPANDE WA MWENYE HAKI SIKU ZOTE
VIVA UKAWA!!
 
Ahsante kwa utabiri ulio karibu sn na matukio halisi cc watz tunajipanga kukabiliana na hawa wakandamizaji
 
Back
Top Bottom