Nasumbuliwa na tumbo naombeni msahada wenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasumbuliwa na tumbo naombeni msahada wenu

Discussion in 'JF Doctor' started by THE ONETATUS, Oct 10, 2012.

 1. THE ONETATUS

  THE ONETATUS Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumbo linanisumbua sana nilijarb kwenda hosp nikachukua vipimo nikahambiwa choo ndio kinasumbua nikapewa dawa hila dawa haijanisaidia chochote pia naweza nisipate aja kubwa kwa muda wa siku 4 hadi 5 na nikila muda kidogo njaa nisaidieni jamani
   
 2. rushanju

  rushanju JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 2,344
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  pima damu kuona kama kuna typhoid
   
 3. THE ONETATUS

  THE ONETATUS Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  damu nishapima ila typhoid hakuna nkubwawangu
   
 4. a

  amigooo Senior Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu tuwasiliane kwa kuweza kukusaidia tatizo lako. Zipo lishe muhimu zilizoandaliwa kiasilia kwa ajili ya kuondoa matatizo ya tumbo. healthwealthfirst@gmail.com
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,618
  Trophy Points: 280
  Mkuu.@THE ONETATUS Una Matatizo ya UKOSEFU WA KUTOPATA CHOO KIURAHISI : Soma tiba rahisi
  [HR][/HR]UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

  Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

  Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

  MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
  Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

  NINI HUSABABISHA TATIZO?
  Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

  NINI KIFANYIKE?
  Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni

  mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi

  mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja

  ya kwenda chooni. Ili usifanye haraka na upate muda wa

  kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula

  kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya

  matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

  Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu

  yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya

  uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla

  hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya

  kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa

  choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na

  matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula

  vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa

  unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.

  Ninakushauri Nenda tena kamuone Dakatari.
   
 6. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Jaribu kupima Vidonda vya tumbo au gesi mkuu
   
 7. THE ONETATUS

  THE ONETATUS Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuuu iyo nayo tayari nimepima sina vidonda vya tumbo!!
   
 8. THE ONETATUS

  THE ONETATUS Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashhuru sana mkubwa ngoja kwanza niyafanyie kazi ulonambia ikishindikana niende tena kwa dactari.
   
 9. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Dawa gani umepata ulipokwenda hospitali. Dawa unayohitaji ni edema. Huo ndio msahada unaohitaji.
   
 10. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Edema??
  Duh?!Mkuu???..hua naheshimu sana comments zako lakini hapa siyo mkuu..either kuwa serious kidogo na compassionate na wagonjwa mkuu.
   
Loading...