Nasumbuliwa na presha ya kushuka.

Veronica7598

JF-Expert Member
Jan 2, 2017
361
408
Wakuu habari za w,keend.

Wandugu naombeni msaada nasumbuliwa na presha ya kushuka, nina ujauzito wa miezi7 nimeenda hospital nimeambiwa nina presha ya kushuka.

Naombeni msaada kwa anaefaham jinsi kuondokana na hali hii, napata tabu sna pumzi zinabana nashindwa kulala nimeambiwa niwe nakunywa coca-cola lakin bado hali bado inasumbua.

MSAADA WENU WAKUU
 
unaweza kununua glucose pia pharmacy ukauchanganya na maji na kunywa.
 
Pole sana hii...natumai hali yako imetengemaa sasa.

Siku nyingine ikitokea fanya yafuatayo:

  • Kama amesimama basi alale kiubavu ubavu (ubavu wa kushoto) hii usaidia kuongeza mzunguko wa damu kwa kiumbe kilicho tumboni na hivyo basi kuzuia madhara yanayoweza kumpata mtoto tumboni pia uongeza mzunguko wa damu kwenye ubongo wa mama na hivyo kusaidia kupunguza kizunguzungu.
  • Kama eneo haliruhusu kulala labda (mfano kwenye basi) mama mjamzito akiwa amekaa ainamishe kichwa katikakti ya magoti hii husaidia kama mbinu ya hapo juu ila mbinu ya kulala ni njema zaidi.
  • Tafuteni msaada zaidi wa kitabubu kama kumuwaisha hospitali au kumuita daktari au muhudumu wa afya aliye karibu.
Nini husababisha kushuka kwa presha kipindi cha ujauzito??

  • Kusimama kwa haraka sana.
  • Kulalia mgongo (mama anashauriwa kulalia ubavu wa kushoto)
  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Kupungukiwa na maji mwilini (pia upungufu wa chakula)
  • Mwili kupata joto sana.
  • Kufanya kazi za nguvu sana.

Ni hayo tu kwa sasa ila ningependa sana kujua mama anaendeleaje
 
barikiwa mkuu
 
Tafuta kinywaji kinaitwa Guinness, mimina glass moja na kuinywa kila itokeapo mapigo ya moyo kushuka.

Upone upesi/haraka.
 
Back
Top Bottom