Nasumbuliwa kupewa cheti cha mtoto RITA

ngome1838

JF-Expert Member
Feb 20, 2019
2,029
2,471
Jamani huu ni mwezi wa pili nafuatilia cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya mtoto wangu ambaye anataka kuomba mkopo kwa ajili ya elimu ya juu.

Nimeshafuatilia mpaka nimechoka, wamedai mara nikalete kiapo, imenitoka hela kwani ilinibidi niende kwa wakili binafsi kwakuwa Mahakama zilikuwa zimefungwa. Kila nikienda wanadai hawaoni faili langu.

Nisaidieni, nifanyeje au huko kwenu hivi vyeti vya kuzaliwa vinapatikanaje?
 
Jamani huu ni mwezi wa pili nafuatilia cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya mtoto wangu ambaye anataka kuomba mkopo kwa ajili ya elimu ya juu. Nmesfuatilia mpaka nimechoka, wamedai mara nikalete kiapo, imenitoka hela kwani ilinibidi niende kwa wakili binafsi kwakuwa mahakama zilikuwa zimefungwa. Kila nikienda wanadai hawaoni faili langu. Nisaidieni, nifanyeje au huko kwenu hivi vyeti vya kuzaliwa vinapatikanaje?
Tatizo lako ni moja tu Mkuu.
Unashindwa kujiongeza hata pale unapotengenezewa nafasi ya kujiongeza.
Pia kujiongeza ni best option kuliko kupoteza muda wako kila siku kufuatilia cheti.
 
Nyoosha maelezo sasa ajiongeze vipi
Tatizo lako ni moja tu Mkuu.
Unashindwa kujiongeza hata pale unapotengenezewa nafasi ya kujiongeza.
Pia kujiongeza ni best option kuliko kupoteza muda wako kila siku kufuatilia cheti.
 
Toa hela upate cheti. Mimi enzi zangu nilitoka kijijini na kuja kukipata hapo posta siku hiyo hiyo! Nilihitaji cheti ili nijiunge chuo hivyo sikuwa na namna.
 
Rita pale bana acha tu yaan toka iwe lazma kupata cheti baaasi imeshakua fursa hyo kwa wadau ila poa tu ipo siku
 
KUNA UMUHIMU WA KUPATA CHETI CHA KUZALIWA PALE TU MTOTO ANAPOZALIWA MAPEMAAAA...HUKU UKUBWANI MAJANGA MENGI
 
Jamani huu ni mwezi wa pili nafuatilia cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya mtoto wangu ambaye anataka kuomba mkopo kwa ajili ya elimu ya juu.

Nimeshafuatilia mpaka nimechoka, wamedai mara nikalete kiapo, imenitoka hela kwani ilinibidi niende kwa wakili binafsi kwakuwa Mahakama zilikuwa zimefungwa. Kila nikienda wanadai hawaoni faili langu.

Nisaidieni, nifanyeje au huko kwenu hivi vyeti vya kuzaliwa vinapatikanaje?
Pole sana!
Waulize nani anapaswa kukutafutia faili kama si wao?
Kuna dawati la malalamiko pia,wafikishie hili.Pia faili huhusisha taarifa/vyeti vya wateja wote wa mwezi husika,sasa wanaposema hawaoni wanaleta walakini ktk utendaji wao.Ila ni wazi wanataka rushwa,wategee mtego wanase,Wapigie takukuru 112 waambatane nawe.
 
Mazingira yaliyopo hospitali ya Mnazi mmoja nimeyapenda sana, maana punde mama unapojifungua basi ndani ya wiki unapata cheti cha mwanao hapo hapo hospitali. Hakuna haja ya kuwa na tangazo na kuanza kusumbuka kutafuta cheti wala nini.
Haya masuala ya kutafuta cheti ukubwani yalinifanya niombwe rushwa na mama mtu mzima kipindi nipo O-level. Nilimpatia pesa lakini kesho yake nilipoenda aliona aibu na akarudisha hela yangu.
 
Jamani huu ni mwezi wa pili nafuatilia cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya mtoto wangu ambaye anataka kuomba mkopo kwa ajili ya elimu ya juu.

Nimeshafuatilia mpaka nimechoka, wamedai mara nikalete kiapo, imenitoka hela kwani ilinibidi niende kwa wakili binafsi kwakuwa Mahakama zilikuwa zimefungwa. Kila nikienda wanadai hawaoni faili langu.

Nisaidieni, nifanyeje au huko kwenu hivi vyeti vya kuzaliwa vinapatikanaje?

Hivi serikali ilisema inafungua dawati la malalamiko waliishia wapi na hiyo project
 
Jamani huu ni mwezi wa pili nafuatilia cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya mtoto wangu ambaye anataka kuomba mkopo kwa ajili ya elimu ya juu.

Nimeshafuatilia mpaka nimechoka, wamedai mara nikalete kiapo, imenitoka hela kwani ilinibidi niende kwa wakili binafsi kwakuwa Mahakama zilikuwa zimefungwa. Kila nikienda wanadai hawaoni faili langu.

Nisaidieni, nifanyeje au huko kwenu hivi vyeti vya kuzaliwa vinapatikanaje?
Rita kuna usumbufu sana tena wakijinga,nenda ofisi ya malalamiko utapata msaada.
Nilifutilia cheti hapo miezi 4 mpaka.
Lkn kwa sasa wapo nane nane wanatoa vyeti haraka ndani 2wiki unaambiwa ukifuate wilayani kwako tena kwa punguzo la bei.
 
RITA ni shida ukienda Taifa pale lazima utakutana na wamama wanalia 2 au 3 ukiwaliza vp wanasema wamechoka kusumbuliwa kuhusu kufuatilia vyeti vya watoto wao
Tatizo hi nchi watumishi wengi hawatimizi majukumu yao
 
Rita kuna usumbufu sana tena wakijinga,nenda ofisi ya malalamiko utapata msaada.
Nilifutilia cheti hapo miezi 4 mpaka.
Lkn kwa sasa wapo nane nane wanatoa vyeti haraka ndani 2wiki unaambiwa ukifuate wilayani kwako tena kwa punguzo la bei.
Hivi 8/8 Dar inafanyika wapi?
 
Jamani huu ni mwezi wa pili nafuatilia cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya mtoto wangu ambaye anataka kuomba mkopo kwa ajili ya elimu ya juu.

Nimeshafuatilia mpaka nimechoka, wamedai mara nikalete kiapo, imenitoka hela kwani ilinibidi niende kwa wakili binafsi kwakuwa Mahakama zilikuwa zimefungwa. Kila nikienda wanadai hawaoni faili langu.

Nisaidieni, nifanyeje au huko kwenu hivi vyeti vya kuzaliwa vinapatikanaje?
We we mcongo
 
Tatizo lako ni moja tu Mkuu.
Unashindwa kujiongeza hata pale unapotengenezewa nafasi ya kujiongeza.
Pia kujiongeza ni best option kuliko kupoteza muda wako kila siku kufuatilia cheti.
Kuna mtu alishawahi kukataliwa kumuwekea dhamana na mapolisi akiambiwa eti picha yake kwenyw kitambulisho chafu.
Akawa ana majonzi akaondoka. Vole kumhadithia ndugu yake tu..akamwambia ebo! Umeshindwa kusafisha picha yako mwenyewe?! Ndio mambo hayo sasa..
 
Hahaha sasa nenda uhamiaji kamuombee passport huyo mtoto, uhamiaji watakwambia ukalete cheti cha kuzaliwa na national ID.
Ukienda mara ya pili baada ya kutoka uhamiaji wata kupa. Usumbufu ndio nature ya Tanzania, hauepukiki.
Wazazi wangu hawana vyeti vya kuzaliwa na hata watendaji wa huko uhamiaji wazazi wao hawana, lakini ukienda wanavidai unaweza kudhani wazazi wako walikuwa wajinga kwanini hawana. Lakini havikuwa vikitolewa, na hata sasa ni kwa mbinde. Lakini wanapovidai utadhani vipo tu somewhere unaenda kuvichukua.
 
Back
Top Bottom