Nasubiri Siku J.Kikwete Ajibu Mapigo ya J.Magufuli

Mtoto Wabibi

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
451
294
Mara nyingi kama sio zote Raisi Magufuli amekuwa "akimchana live' raisi mstaafu J.Kikwete kutokana na utendaji wake katika serikali yake.Na ukizingatia hiyo michano live huwa inawekwa kwenye title mbali mbali za media hasa magazeti.

Na wakati huo huo toka kampeni hadi sasa mara zote J.kikwete amekuwa akimpa sifa nyingi huyu JPM. Ikumbukwe kuwa mkwere siku zote ana lugha zake za uswahilini yani akikupa kijembe huta kuja sahau na huwa kina nguvu sana kwenye media sana.Sijui kwanini huwa hapendi kujibu tuhuma dhidi yake lakini ikitokea kajibu basi jipange.

Nasubiri kwa hamu sana kijembe chake ( michano live) kwa JPM ambaye anaona fahari kuchana wenzake. Na media za bongo kwa kupamba......!

One day yes,lets wait
 
JK ni Mwanasiasa wa kuzaliwa sio wa kujifunza, tangu akiwa Primary alianzia kwny Chipukizi kuanzia 1974 akawa Katibu Msaidizi wa CCM ana miaka 41 ndani ya Chama msitegemee aropoke lolote.
Kinachomsumbua Dr. Magufuli ni ugeni wa kwny siasa kwani tangu alipoingia kwny Siasa 1995 hakuwahi kuwa Mwanasiasa alikuwa Kiongozi sasa ndo anajifunza kuwa Mwanasiasa akiwa tayari ni Rais.
Kama kuikuta Vibaya Nchi hii hakuna alieikuta Vibaya kama Mzee Ally Hassan Mwinyi kwa Mujibu wa Jaji Warioba aliekuwa PM wa kwanza wa Mwinyi anasema waliachiwa Nchi ikiwa haina hata Forex ya kulipia meli ya Mafuta iliyotia Nanga bandarini, kila bidhaa muhimu lazima ipatikane kwa Mbinde lakini hakuwa kusikika akilia lia Jukwaani wakati wake au hata baada ya kustaafu!
 
Kapoteza nafasi nzuri sana ya kumchana live pale alipomwambia kwamba amemuachia kazi ngumu sana. Kikwete angeomba mic na kumwambia maamuzi ya hawa Wanafunzi 7,802 tulifanya kama Serikali na wewe katika kikao cha Baraza la Mawaziri kuhusu mpango huu maalum wa kuongeza walimu wa sayansi nchini ulihudhuria na hukutoa pingamizi lolote sasa nakushangaa tena leo unawafukuza hawa Wanafunzi usiku wa manane tena kama mbwa koko. Angejizolea sifa nyingi sana na kumuacha Baba Jesca ndembe ndembe.

Mara nyingi kama sio zote Raisi Magufuli amekuwa "akimchana live' raisi mstaafu J.Kikwete kutokana na utendaji wake katika serikali yake.Na ukizingatia hiyo michano live huwa inawekwa kwenye title mbali mbali za media hasa magazeti.

Na wakati huo huo toka kampeni hadi sasa mara zote J.kikwete amekuwa akimpa sifa nyingi huyu JPM. Ikumbukwe kuwa mkwere siku zote ana lugha zake za uswahilini yani akikupa kijembe huta kuja sahau na huwa kina nguvu sana kwenye media sana.Sijui kwanini huwa hapendi kujibu tuhuma dhidi yake lakini ikitokea kajibu basi jipange.

Nasubiri kwa hamu sana kijembe chake ( michano live) kwa JPM ambaye anaona fahari kuchana wenzake. Na media za bongo kwa kupamba......!

One day yes,lets wait
 
Khalfani anaweza asijibu lolote maana huyu rais anaweza ajiuzulu akisikia maneno ya mswahili . Kikwete + Membe kachero + makamba jr ni watu wakuchungwa bila kusahau spy chief. Teacher watch out not everything to comment on public concerning your former boss , just advice as far as we diaspora we are not allowed to comment anything to this regime.
 
Kapoteza nafasi nzuri sana ya kumchana live pale alipomwambia kwamba amemuachia kazi ngumu sana. Kikwete angeomba mic na kumwambia maamuzi ya hawa Wanafunzi 7,802 tulifanya kama Serikali na wewe katika kikao cha Baraza la Mawaziri kuhusu mpango huu maalum wa kuongeza walimu wa sayansi nchini ulihudhuria na hukutoa pingamizi lolote sasa nakushangaa tena leo unawafukuza hawa Wanafunzi usiku wa manane tena kama mbwa koko. Angejizolea sifa nyingi sana na kumuacha Baba Jesca ndembe ndembe.
 
Siwezi kufikiri Kikwete atakuja kumjibu chochote Magu , sababu kubwa ni, Kikwete bado ni mwenyekiti wa chama kilichomuweka Magu madarakani, analazimika kupiga kimya, akijibu chochote itakuwa kama wanashindana "nani zaidi" hapo chama kitameguka na nyufa zitakazojitokeza ni vigumu kuziziba kwa miaka mingi ijayo waswahili wanasema " ukubwa jalala" ndio maana tunamuona Kikwete akijikausha kama si yeye
Huo ni ukomavu wa kisiasa na isichukuliwe vinginevyo , huku tukikumbuka ule msemo maarufu
"mtoto bado anakua akikua ataacha"
 
Jk hahitaki kujibu hoja kwa maneno. Anatumia formula ya "TIME WILL TELL" Na mpaka sasa tumeisha ona meng.

Mwaka hta hujaisha tofauti ya uongoz wa kikwete na Magu unaonekana kabisa.
 
Mara nyingi kama sio zote Raisi Magufuli amekuwa "akimchana live' raisi mstaafu J.Kikwete kutokana na utendaji wake katika serikali yake.Na ukizingatia hiyo michano live huwa inawekwa kwenye title mbali mbali za media hasa magazeti.

Na wakati huo huo toka kampeni hadi sasa mara zote J.kikwete amekuwa akimpa sifa nyingi huyu JPM. Ikumbukwe kuwa mkwere siku zote ana lugha zake za uswahilini yani akikupa kijembe huta kuja sahau na huwa kina nguvu sana kwenye media sana.Sijui kwanini huwa hapendi kujibu tuhuma dhidi yake lakini ikitokea kajibu basi jipange.

Nasubiri kwa hamu sana kijembe chake ( michano live) kwa JPM ambaye anaona fahari kuchana wenzake. Na media za bongo kwa kupamba......!

One day yes,lets wait

utasubili sana hadi ukome, na kama hujui JK na JPM wanashirikiana sana, magufuli kuongea ukweli haimaanishi anamsema JK, anawasema viongozi na watendaji wote waache uzembe. endelea kusubili ila utacho endelea kushuhudia ni JK kwenda ikulu kumpa ushauri JPM juu ya mambo mbalimbali.
unaakili ya kijinga sana ww.
 
Acha hasira rafiki yangu. Hizi siyo SIFA za kujaziwa. ZIPO! ANAZO TAYARI! Na "sifa" hizo ndizo zamfanya ASIJIBU mapigo.
Elewa tu ndugu yangu kuwa twachangia hoja kwa muktadha wa hoja yenyewe!
HAKUNA CHA MUKTADHA HAPA BANA.
 
Back
Top Bottom