Mpauko
R.I.P
- Jan 19, 2019
- 2,323
- 3,463
Nilistaajabu sana kuona kwamba,
sumu humsamehe mwanaadam,
pale inapobembelezwa na maziwa,
Naye kiziwi atafarijiwa na kiziwi pia,
Hiyo ndiyo asili ya dunia.
Nastaajabu sana kuyajua haya,
hata tabia hubadilishwa na majina,
hata kama mwenendo wa mtu, utawasilishwa na sura yake.
Nastaajabu hakika.
nilipata habari kuhusukupuliza,
nikatambua mpaka upulize,
basi kuna mambo mawili,
Kuna kupuliza ili iwake,
na kuna kupuliza ili ipoe.
Dah sasa napata picha,
wakati napuliza kwa imani ipoe,
nikajikuta inawaka,
na baada ya moto kuzimika,
jivu halikuwa na thaman tena.
Naamini hata unapotembea,
huwezi jua ni hatua ipi italeta furaha, katika safari yako ya maisha,
endelea kupiga hatua,
furaha huja wakati usiotarajiwa.
hata kwa upande wa matatizo
nayo pia huja katika njia tofauti,
kuna muda mwengine matatizo huja, ili kukufanikishia malengo yako,
muda mwengine matatizo huja,
ili kukudhihirishia yupi rafiki wa kweli.
kuna muda mwingine matatizo huja, vile kipimo cha imani juu ya muumba,
si kila tatizo tunatakiwa kusimama,
katika upande wa huzuni na kilio,
Usihuzunike sana usichokimiliki,
enda ukiwa nacho kitakuhuzunisha,
Nakukumbusha tu huwezi pata jino, lenye afya kwa kinywa kililichooza,
hivyo basi itakuwa si busara,
kupigana na mtu alieamua kukupiga,
Pasi na kosa la mashiko,
Hewala basi shika zako hamsini,
Dunia hii yetu sote wanadamu,
Inua kichwa kwa matumaini.
sumu humsamehe mwanaadam,
pale inapobembelezwa na maziwa,
Naye kiziwi atafarijiwa na kiziwi pia,
Hiyo ndiyo asili ya dunia.
Nastaajabu sana kuyajua haya,
hata tabia hubadilishwa na majina,
hata kama mwenendo wa mtu, utawasilishwa na sura yake.
Nastaajabu hakika.
nilipata habari kuhusukupuliza,
nikatambua mpaka upulize,
basi kuna mambo mawili,
Kuna kupuliza ili iwake,
na kuna kupuliza ili ipoe.
Dah sasa napata picha,
wakati napuliza kwa imani ipoe,
nikajikuta inawaka,
na baada ya moto kuzimika,
jivu halikuwa na thaman tena.
Naamini hata unapotembea,
huwezi jua ni hatua ipi italeta furaha, katika safari yako ya maisha,
endelea kupiga hatua,
furaha huja wakati usiotarajiwa.
hata kwa upande wa matatizo
nayo pia huja katika njia tofauti,
kuna muda mwengine matatizo huja, ili kukufanikishia malengo yako,
muda mwengine matatizo huja,
ili kukudhihirishia yupi rafiki wa kweli.
kuna muda mwingine matatizo huja, vile kipimo cha imani juu ya muumba,
si kila tatizo tunatakiwa kusimama,
katika upande wa huzuni na kilio,
Usihuzunike sana usichokimiliki,
enda ukiwa nacho kitakuhuzunisha,
Nakukumbusha tu huwezi pata jino, lenye afya kwa kinywa kililichooza,
hivyo basi itakuwa si busara,
kupigana na mtu alieamua kukupiga,
Pasi na kosa la mashiko,
Hewala basi shika zako hamsini,
Dunia hii yetu sote wanadamu,
Inua kichwa kwa matumaini.