Nassoro Mwinchui ni Simba lialia lakini tumtayarishe kuchezesha CAF.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,247
Reaction score
16,169
Mwamuzi wa dabi ya tarehe 01 March ni Nassoro Mwinchui ingawa wote tunajua kuwa inaipenda sana Coastal Union na Simba ss na alishapewa adhabu mara nyingi kwa kuzipa upendeleo Simba na Coasta kwa vipindi vya karibukaribu vilivyofuatana. Alishawahi kutumwa mara nyingi kuchezesha mechi za Yanga dhidi ya timu nyingine ili akazipe ulinzi timu hizo dhidi ya Yanga. Tunalijua hilo.

Amepewa kuchezesha mechi ambayo hata yeye anajua kuwa hata Patrice Motsepe, Rais wa CAF ataiangalia hii mechi. Hii ni mechi ambayo itamuinua au kumzamisha katika kazi yake ya upuliza filimbi kwenye mchezo wa kabumbu kwakuwa hata kamati ya waamuzi ya CAF itaikodolea macho vibaya sana hii mechi wakati huu wa maandalizi ya kuelekea AFCON 2027 Tanzania, Kenya na Uganda.

Asikubali kwenda uwanjani na maelekezo ya wavimbamacho ambayo wadau wa mpira watamzamisha kwenye jasho lake mwenyewe. Huwezi kwenda kuchezesha mechi za CAF za 2027 kabla ya kuchezesha dabi ya Simba na Yanga, timu zenye hadhi ya CAF championship kwa weledi mkubwa.

Apandishe thamani yake kupitia mechi hii, anyooke kama rula, nyeupe aiite nyeupe na nyeusi aseme ni nyeusi.
 
Mbona malalamiko yameanza mapema mapema hivi? Si mlisajili sowah,mwalimu,na mastaa kibao. Milio ya nini?
 
Ragiga kafungiwa mara ngapi kwa kuipendelea Yanga
 
Back
Top Bottom