Nassari: Wanaopinga juhudi za serikali ya awamu ya tano wana matatizo

Hivi lengo la kuficha kichwa cha gazeti ni lipi
ad75041c8e6761810e65b63e964c97a4.jpg
6d2f0097147772fa5a266cf8a822f6a3.jpg
 
Hebu Weka wazi ni gazeti gami hilo

Ni kweli magazeti mengi ya leo yametoa habari hii ya NASSARI mbuge wa Arumeru mashariki kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli na serikali yake na amesema kuwa atashirikiana naye kwa ajili ya maendeleo ya watanzania. Nassari siyo kama wale walioko gerezani wanaofanya kila mbinu ya kupambana na Rais na mwisho wake wanawakosesha wananchi wao haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa. Chadema wengi tu wanamkubali Magufuli na ndiyo maana hata akina Halima Mdee, John Mnyika na wengine waliamua kukaa kimya wakishughulika na kero za wananchi wao katika majimbo yao.
 
Who is Nassari?
Mbunge msomi,machachari, wa kudumu wa chadema wa mkoani arusha anayejitambua..lema alimsaidia katika harakati za mwanzo za kampeni..kijana alimwamini sana lema..lakini badae alishindwa kuzielewa harakati za lema sababu yeye alitaka ubunge kuwaletea watu wa kwao maendeleo na sio kuwa mwanaharakati..somo hapa ni kuwa lema ni mchaga kwao ni Moshi..maendeleo ya arusha na wana arusha sio jukumu lake sababu Moshi Mzee ndesamburo alishafanya makubwa tu..2020 wana arusha wajaribu kuweka muarusha mwenzao mwenye uchungu na jiji lake la arusha.. Toka lini mtu akawa na uchungu na nyumba ya jirani..angalia majimbo yote ya wanachadema ambao wamechaguliwa kwao..mfano; iringa kwa msigwa, mbeya kwa sugu, mikumi kwa prof jay, hai kwa mbowe, arumeru kwa nasary..na kadhalika..angalizo: sina maana ya ubaguzi hapa..ni uhalisia tu
 
uongozi wa sasa ,sawa na kujenga jengo baadaye ukaribomoa hapo ,walioona jengo limesimama watakusifia na upande wapili waliona unabomoa hakika watajiuliza maswali ndio uongozi wa awamu hii.
 
Onyesha aliposema anayekataa ni "chizi"? Nasari kasifia utatuaji wa migogoro ya ardhi kuna ajabu gani hapo? Kwani kutatua migogoro ya ardhi Arumeru ndio kuiweka nchi hii katika hali njema kiuchumi?
Watu wajinga wajinga ndio wanao tumia muda wao kuokoteza vichwa vya magazeti kutengeneza story kama nyie. Lete official statement ya nini alikuwa anazungumzia na kasemaje ueleweke
Haya kasema asiye muunga mkono Magufuli ana matatizo...
 
Alishatokea Tena Majukwaani na Magu wakati Mdee na Bulaya wakiwa wamewekwa Ndani, Leo hii wakati Lema yupo rumande kwa maono na ndoto dhidi ya Magufuli, Ben Saanane ametoweka, Max yupo Rumande, huyu Dogo anaropoka haya! amesahau kuwa Wakati akihoji wanafunzi wa Udom kufukuziwa mitaani na kuitwa Vilazza wabunge wote waliungana naye alipotupwa nje ya bunge? Mimi Nisiseme Mengi nataka nione Video yake akisema hayo, halafu ndio kitaendelea!
 
Baada tu ya kuficha jina la gazeti umeonekana mnafiki wa kiwango cha juu, UHURU lazima waandike upupu kuhusu chadema, nasari hawezi mpongeza , amepongeza juhudi za majaliwa kutatua migogoro ya ardhi, ambayo hata hivyo haijatatuliwa bado bali ametoa MATAMKO ya kumaliza migigoro hiyo kama ilivyo kawaida ya matamko mengi mengine.
Nenda angalia TV news
Je?Hata siasa mpaka 2020 nalo analiunga mkono? Mi naamin Kamanda kaliswa maneno kama hajalishwa maneno hajaeleweka vizuri binafsi kuna mambo President kayafanya saluti kuna mengine mmmmh
 
Hilo UHURU hata nyie wanaCCM hamliamini.

Ndio maana umeficha jina la gazeti.
Hakika ndo maana ameficha jina la gazeti.nacho jua mimi ni kua nasari amesema wanaopinga juhudi za kuwaletea wanainchi maendeleo.na hajasema hilo neno kichaaa
 
Hivi mtu akiwa kichaa alafu wewe mzima ukapingana nae huyo kichaa sina wewe unachukuliwa kua kichaa
 
Ajiandae kuitwa msaliti,angoje matusi toka kwa MAVISHAA,angoje kupopolewa mawe toka ufipa maana kwao ukifikiri tofauti tu ni msaliti
 
Kama kweli Nassari kasema hivyo basi yeye ni kichaa wa kupelekwa milembe
 
Hii habari ipo kwenye magazeti ya Nipashe, Uhuru, Majira na Mtanzania, na hata Mwanachi.

Ujumbe umefika.
566bc4c580bf0416256244241f147f6f.jpg
Nimejaribu kufuatilia nimejiridhisha kuwa Nassari hakutamka haya yaliyoandikwa kwenye headline ya Uhuru, wala hajazungumza lolote kuhusu JPM, bali alizungumzia awamu ya tano. Na alijikita juu ya Waziri Mkuu kutatua migogoro ya mashamba jimboni kwake. Mkumbuke akiwa bungeni Nassari mara kwa mara amekuwa akipigia kelele suala la migogoro ya ardhi ikiwemo umiliki tata wa ardhi ambao umesababisha baadhi ya wananchi jimboni kwake kukosa ardhi.
Sioni kama kuna tatizo kwa Nassari kupongeza hatua hiyo.
 
Ccm mnaaibisha kwa uhuni wa kitoto. Unaka gazeti lako la Uhuru kisha kwa vile haliaminiki unalifunika kisha unasema magazeti mengi yamesema hivyo.
Hiyo ni fedheha kwani unaonyesha kuwa maneno hayo yanakushangaza hata wewe ingawa ungependa yawe hivyo. Unashangaa iweje Nasari aseme hivyo wakati mtu wenu watu wa kawaida wanazomea mpaka sauti yake.
Mnazidi kumuaibiasha
Ingeandikwa na TANZANIA DAIMA, ungeliikubali habari vizuri.
 
Ni kweli magazeti mengi ya leo yametoa habari hii ya NASSARI mbuge wa Arumeru mashariki kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli na serikali yake na amesema kuwa atashirikiana naye kwa ajili ya maendeleo ya watanzania. Nassari siyo kama wale walioko gerezani wanaofanya kila mbinu ya kupambana na Rais na mwisho wake wanawakosesha wananchi wao haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa. Chadema wengi tu wanamkubali Magufuli na ndiyo maana hata akina Halima Mdee, John Mnyika na wengine waliamua kukaa kimya wakishughulika na kero za wananchi wao katika majimbo yao.
Kauli ya Mbunge wa Chadema Arumeru Mashariki mh. Nassari katika mkutano wa majumuisho ya ziara ya waziri mkuu mh.Majaliwa mkoani Arusha ....... nanukuu .....

"Nashukuru sana kwa commitment ambayo serikali ya awamu ya tano imeonyesha, dhamira iliyopo ya kuwafikia wananchi na sisi kama wawakilishi wa wananchi ndo imekuwa, imekuwa kiu yetu kwa siku nyingi

...
Kwa hiyo nikuhakikishie kwamba feedback ambayo tunaipeleka kwa wananchi ni feedback nzuri, feedback ya mahusiano, feedback ya mashirikiano na atakuwa ni kiongozi mjinga tu ambae atakataa kushirikiana na kiongozi mwenzake eti kwa sababu ya tofauti ya vyama vya kisiasa ..."

Chanzo: Simu tv .... taarifa ya habari jana usiku
 
Nimejaribu kufuatilia nimejiridhisha kuwa Nassari hakutamka haya yaliyoandikwa kwenye headline ya Uhuru, wala hajazungumza lolote kuhusu JPM, bali alizungumzia awamu ya tano. Na alijikita juu ya Waziri Mkuu kutatua migogoro ya mashamba jimboni kwake. Mkumbuke akiwa bungeni Nassari mara kwa mara amekuwa akipigia kelele suala la migogoro ya ardhi ikiwemo umiliki tata wa ardhi ambao umesababisha baadhi ya wananchi jimboni kwake kukosa ardhi.
Sioni kama kuna tatizo kwa Nassari kupongeza hatua hiyo.
Jihabarishe zaidi mkuu kwa comment nilorusha hapo muda si mrefu
 
Back
Top Bottom