Nassari: Wanaopinga juhudi za serikali ya awamu ya tano wana matatizo

kijana wa leo

JF-Expert Member
Nov 28, 2011
2,801
2,000
Ungeweka hayo magazeti yote, hata hivyo ni mtizamo wake, hata tunaompinga kuna baadhi ya vitu tunakubaliana nae lakini kuna vitu anafanya vinaharibu msingi wa vile vizuri anavyofanya na ndio mana tunampinga. Kama hiyo kauli ni kweli ameisema basi siku siyo nyingi naye atakua kichaa mwenzetu.
 

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,871
2,000
Kama Nassari kasema hayo kweli basi anashida sehemu fulani maana hakuna mtu tz anampinga magufuli kwa kila jambo analolifanya. Yapo mambo mengi mazuri sana yaliyoshinda wenzake yeye anayafanya kwa hayo sote tunampongeza. Ila yapo mengine mengi pia anayatenda ambayo tuna haki ya kuyahoji na kuyapinga, sasa kufanya hivyo siyo ukichaa ni demokrasia unaochagizwa na utofauti wa maono na mtazamo. Kama tutafikia kiwango cha kuwaita wale tunaotofautiana nao mitazamo vichaa basi tutakuwa tumefika pabaya sana maana tunaweza kujikuta tunaita wazazi wetu, viongozi wetu wa vyama, viongozi wetu wa dini, viongozi wa serikali na watanzania wengine vichaa.
 

Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,210
2,000
Kichwa cha habari tu hakitoshi, ungeeleza habari yote ningekuelewa. Nimeshaona vichwa vya habari vingi tu haviendani kabisa na maelezo ya habari yenyewe.
Miaka ya nyuma kuna gazeti liliweka kichwa cha habari front page kwa maandishi makibwa, "WAZIRI AFUMANIWA" , kusoma ndani ili kujua ni waziri gani kumbe ni mkazi wa Morogoro aliyekuwa anaitwa Waziri ndiye alifumaniwa.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,861
2,000
Ccm mnaaibisha kwa uhuni wa kitoto. Unaka gazeti lako la Uhuru kisha kwa vile haliaminiki unalifunika kisha unasema magazeti mengi yamesema hivyo.
Hiyo ni fedheha kwani unaonyesha kuwa maneno hayo yanakushangaza hata wewe ingawa ungependa yawe hivyo. Unashangaa iweje Nasari aseme hivyo wakati mtu wenu watu wa kawaida wanazomea mpaka sauti yake.
Mnazidi kumuaibiasha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom