Nassari: Lowassa anahusika kunipiga

Nassari: Lowassa anahusika kunipiga

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,506
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemtuhumu Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kwamba anahusika na kipigo alichokipata kutokana na chuki aliyonayo kwake.

Aidha amemtuhumu Spika wa Bunge, Anne Makinda kwamba naye ni miongoni mwa watu wanaomchukia pamoja na viongozi wengine wa Bunge, kwa kuwa hakuna kati yao aliyempigia simu au kumtumia ujumbe wa kumjulia hali kutokana na kipigo alichopata ambacho kimemsababishia maumivu makali.

Akizungumza jana akiwa kwenye chumba alicholazwa katika Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ufahamu Muhimbili (Moi), Nassari alidai Lowassa ambaye amewahi kuwa waziri mkuu kabla ya kujiuzulu, amemchukia tangu alipomshinda mkwewe Sioi Sumari, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Aprili mwaka jana.

Nassari aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Selian ya jijini Arusha kabla ya kuhamishiwa MOI, alidai kupigwa na kuchaniwa nguo na Green Guard wakati alipokuwa katika jitihada zake za kuhesabu kura kwenye uchaguzi wa udiwani wa Kata ya Makuyuni-Monduli.

"Kipigo nilichopata Lowassa anahusika ananichukia, anataka urais lakini hawezi kuupata kwa kuuumiza watu kama hivi, alifikiri kwamba nitakufa sitakufa hadi kwa mapenzi ya Mungu," alisema.

Alisema kuna jambo ambalo wananchi wanapaswa kulifikiria ni jinsi ambavyo kumekuwa na matukio ya kutekwa na kuvamiwa, lakini hakuna yanayohusisha kiongozi wa CCM, badala yake ni raia wa kawaida na viongozi wa dini na siasa. Nassari alidai akiwa kama wakala mkuu wa Chadema katika kata hiyo, alikumbana na mambo kadhaa yaliyomshangaza, ikiwa ni pamoja na kufanyiwa jaribio la kutekwa mara mbili, kabla ya kushambuliwa kwa kipigo.

Alisema pia anashukuru kwamba askari wawili waliokuwepo katika eneo hilo walijitahidi kutaka kumnusuru, lakini walizidiwa nguvu na vijana hao, hasa kutokana na kutokuwa na bunduki, ambapo yeye alipofanikiwa kuchoropoka alikimbilia bastola yake na kuwanyoshea vijana hao bila kufyatua.

Akizungumzia kuhusu hali yake, Nassari alisema amepimwa kipimo cha X-ray ambapo imeonyesha kuwa pingili za mgongo wake zipo sawa, lakini daktari ameshauri afanyiwe kipimo kingine kiitwacho MRI ili kuangalia hali ya mishipa kutokana na maumivu makali anayoendelea kuyapata.

Aidha alitumia fursa hiyo kumshukuru Mbunge wa Kuteuliwa, Joseph Mbatia kuwa ndiye aliyemsaidia kufanya mipango kuwasiliana na uongozi wa Bunge na kumwezesha kuhamishiwa Moi, baada ya wabunge wote wa Chadema kwenda Arusha kushughulikia waliofariki kwa bomu.

Hata hivyo, Lowassa alipotafutwa kuhusiana na tuhuma hizo alikataa kuzungumzia suala hilo na kusema hilo aulizwe Msimamizi wa Uchaguzi, Paulo Kitaleki.

Mwananchi ilimtafuta Kitaleki ambaye pia ni katibu tarafa, alikanusha kuhusika kwa Lowassa akielezea kuwa siku ya tukio hilo alikuwa Geita.

"Huyu Nassari ni mwigizaji na anafaa kuwa msanii kwa kuwa anaigiza tu hata hakupigwa, bali yeye ndiyo aliyempiga Wakala wa CCM, Hussein Osama ambaye ni mlemavu, kisha akatimua mbio baada ya vijana kutaka kumkamata, nashangaa kumwona yupo hospitali akidai kupigwa, siyo kweli," alisema Kitaleki.

Habari kwa hisani ya Mwananchi.

Photo taken from Selian to Muhimbili hospital bed.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    15.9 KB · Views: 1,094
  • image.jpg
    image.jpg
    51.1 KB · Views: 1,051
Tanzania politics at its best.

Mpaka kufikia 2015 tutakuwa tumeona na kusikia mengi.

Politically, Today is Mh. Lowassa accusation day.

Kuna mkono wa Mh. Lowassa katika dhoruba hii ya kisiasa na kidini, This is according to Mh. Nassari. Is this true or is just a filthy insinuation?.

This is very serious allegation lakini wakati huo huo na yeye Mh. Nassari anapigwa dongo kama ni "mwigizaji" na hata hospitali ya Selian ilikuwa na angalizo tofauti ukilinganisha na kile Mh. Nassari alikuwa akikisema. Mgonjwa na dakitali wake wamepishana katika kujaza hospital exit form.

Who's telling the truth ?.

Wanasiasa watendeeni haki wananchi wenu. Tanzania kwa sasa inaweweseka kwa sababu ya wanasiasa na siasa uchwara.

Hii sentensi tata sijui ina maana gani. Kwa kifupi tu tunaweza kuiweka kwa jinsi tunavyotaka na ikaleta maana.

Alisema kuna jambo ambalo wananchi wanapaswa kulifikiria ni jinsi ambavyo kumekuwa na matukio ya kutekwa na kuvamiwa, lakini hakuna yanayohusisha kiongozi wa CCM, badala yake ni raia wa kawaida na viongozi wa dini na siasa.
Mh. Nassari ana maanisha kama viongozi wa CCM hawajakumbwa na dhuruba hii ya kisiasa na kidini ina maana wao ndiyo watengenezaji. Really?.

Lakini pia anasahau kuna wengine tunasikia wanajiteka na kudai wametekwa kama ilivyotokea hapa JF, Zanzibar na Tanzania bara (Ludovick). Hawa nao sijui tuwaweke katika kundi lipi wakati vile vile hata yeye anadaiwa ni mgonjwa magumashi (FAKER).

Siasa za Tanzania ni vituko tupu.
 
Hii nchi ni ya kidictator lakin ipo siku watu wote wataghairi halafu tutaona kama majeshi ya polisi wataweza kupambana na umma!!-Na ndo mana hata Pinda usishangae anatoa kauli zile bungeni,wapigine

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Imefika kipindi hawa wanasiasa waache porojo na kupayuka...
Kama una ushahidi nenda kwenye vyombo stahiki kuliko kulalama...
Kwa kuendelea kulalama tu hivi, haitoi msaada kwa Nassari bali inazidi kumvimbisha kichwa mtuhumu wake...
 
Huyu dogo ana matatizo anataka bunge zima wampigie simu.
 
Ng'wamapalala; So PM alienda kumtembelea mgonjwa feki?read btn the lines man hujui kusoma ina maana hata pcha huwez kutazama?
 
So PM alienda kumtembelea mgonjwa feki?
Hili swali ungeliekeza kwenye uongozi wa hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya Selian, Arusha. Hata hivyo, kwani Waziri Mkuu ni dakitali ambaye alipaswa kujua kama Mh. Nassari ni mgonjwa au faker.

read btn the lines man hujui kusoma ina maana hata pcha huwez kutazama?
Why do I have to read between the lines when I can read the hospital statement ambayo inasema,
Akijibu tuhuma hizo Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Paul Kisanga amesema si kweli kwamba mbunge huyo alitoroka hospitalini hapo, bali alipewa ruhusa katika hali ya kawaida baada ya kuonekana hana tatizo lolote linalomsumbua tangu kufika hospitalini hapo.
Aidha amesema mbunge huyo katika kuondoka kwake hakua na masharti yoyote kuwa anahitaji kupata uhamisho wa kwenda katika hospitali nyingine yoyote kwa matibabu zaidi, kwa kuwa hata alipotembelewa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda alimweleza wazi kuwa afya yake imeimarika.
 
Hao green guard alikubaliana nao wasimpige usoni... wamempiga mgongoni tu. Kama amepigwa bila shaka walompiga ni gwanda guard.
 
Sikubaliani na Nassari...halafu kwa kauli zake hizi naamini amepunguza credibility.
Kwamba kwa sababu alimshinda mkwe wa Lowasa basi Lowasa anahusika...!
Kingine...,na kinachochekesha zaidi ni kuwa Makinda nae anahusika...,kisa...! Hajampigia simu/kumtumia sms...!
Kwenye hili,anapunguza credibility yake,asitafute mchawi, kutaka sifa kwa kuropoka ndio mchawi wake.
 
Hata mjinga ukimwambia hali hii hakika atakwambia tu ya kwamba mhusika ni EL.
Yeye aendelee kutumia kodi ya wanainchi vibaya kwani MUNGU iko muda atamrudishia majibu mchana kweupe!
 
Kwa jinsi ninavyomjua lowasa, nina uhakika 100% anahusika. Lowasa amechukua vijana wengi monduli na kuwaweka mfukoni, anawapa pesa na hata kuwanywesha pombe ili wadhuru watu! Lowasa hawezi kupata huo urais, ni mtu hatari sana!

Chadema hamueleweka si mnahitaji raisi strong... mr white ndo anawafaa.
 
Huyu jamaa baada ya kuangalia maendeleo ya afya yake ndio kwanza analalama kutaka apigiwe simu na watu wa CCM simuelewi kabisa.
 
Hakuna anaeaminika tena kila mmoja anavutia kwake

"To know the enemy is half the victory"
 
Back
Top Bottom