Nasitisha rasmi leo kua mteja wa VODACOM!

Nasitisha rasmi leo kua mteja wa VODACOM!

Ni kweli kabisa kwa majibu waliyokupa Vodacom hawawezi kuzuia pesa iliyokwenda kwenye account ya Bank wenye hayo mamlaka ni bank husika.

Vodacom wana mamalaka na account za M-PESA tu, yani hata leo hii ukikosea kutuma pesa badala ya Polisi ukatuma pesa Magereza hawawezi kukurejeshea itabidi uwasiliane na magereza wakurejeshee.
Uhuru unao we hama tu.
M-pesa ni habari nyingine kwa malipo ya mitandaoni na kupokea mapesa ya mitandaoni.
Hahahahah...mtandao wa uhakika ni Vodacom tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hii mitandao ya simu ninapopiga huduma kwa wateja halafu akapokea mwanamke huwa naanza kuhesabu maumivu.

Ni wa hovyo sana hawa wadada. Samahani wanawake wote
 
Hapo unaongea na watu wa bank. Halafu watu wa bank wanawasiliana na selcom kuzuia fedh kutolewa. Hapo iwe hata Tigo au Airtel hawahusiki
 
Voda nimewavumilia nimechoka, hii namba nitaiacha itakuwa kwa ajili ya kupoke simu tu siweki tena vocha, hapa nafanya mchakato wa kuhamia ttcl, wamenichosha.
 
Vodacom wanafanya kimazoea muda wa kuachana nao umefika!!
Inauma sana vodacom mmechangia hela yangu kupotea. Jana nimehamisha hela kutoka bank kwenda mpesa bahati mbaya nikakosea namba na kurusha kwenye namba tofauti. Nimewaomba nyie vodacom mzuie namba ya mtu aliyepokea hela mkakataa kuwa hamuwezi kufanya hivyo ila niwasiliane na bank ndio wairudishie hiyo hela (stupid response). Mnajua kabisa mchakato wa bank utachkua mda mrefu so ili kuepusha kupotea kwa hela yangu mlipaswa kuzuia huyo mtu asiitoe. Kuna mdada anajibu UJINGA kua yeye hawezi kuingia kwenye account ya mteja mwingine! mbona baada ya mimi kuwapa hilo jibu bank kua nyinyi hamna uwezo wa kuingia kwenye acc ya mteja mwingine walipowatafuta mliingia (wakati its too late) na mkawajibu kua hela ishatolewa tangia jana!!? Mnafahamu kua kama mngetoa ushirikiano sahihi jana hela yangu isingepotea!!? SHAME ON YOU MAFACILITATOR WA WIZI, STUPID.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye muhtasary wa habari. Nimeona chief wa vodacom yuko lupango. Amefanza nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom