Nampongeza Rais Mwinyi kwa mapumziko ya Mwaka mpya wa kiislamu

Zee la madawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,878
Reaction score
4,424
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza kuwa Jumatano, Juni 17, 2026, itakuwa siku ya mapumziko ili kusherehekea mwaka mpya wa Kiislamu, 1448 Hijiria.

======================
FB_IMG_1781512034737.jpg

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametangaza kuwa Jumatano, Juni 17, 2026 itakuwa siku ya mapumziko kwa Zanzibar ili kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1448 Hijria.Rais Dkt.

Mwinyi ametoa tamko hilo leo, Juni 15, 2026 Ikulu Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Serikali wa kuutambua Mwaka Mpya wa Kislamu kuwa miongoni mwa siku muhimu Zanzibar.

Amesema siku hiyo itatoa fursa kwa Wananchi, hususan waumini wa dini ya Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya kwa ibada, dua na matendo mema pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuijaalia Zanzibar na Tanzania kwa ujumla amani, umoja na ustawi.

Alhaj Dkt. Mwinyi amewataka Wananchi kuutumia mwaka mpya huo kujitathmini, kuimarisha uchamungu, kusaidiana na kuendeleza maadili mema yanayojenga familia na Taıta lenye mshıkamano.

Aidha, amezitaka Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi, Waajiri na Wananchi wote kuzingatia tangazo hilo kwa mujibu wa taratibu zilızowekwa.Rais Dkt. Mwinyi amewatakia Waislamu na Wananchi wote heri ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1448 Hijria, akimuomba Mwenyezi Mungu aufanye kuwa mwaka wa kheri, amani, afya njema na maendeleo kwa wote.​
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametangaza kuwa Jumatano, Juni 17, 2026 itakuwa siku ya mapumziko kwa Zanzibar ili kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1448 Hijria.Rais Dkt.

Mwinyi ametoa tamko hilo leo, Juni 15, 2026 Ikulu Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Serikali wa kuutambua Mwaka Mpya wa Kislamu kuwa miongoni mwa siku muhimu Zanzibar.

Amesema siku hiyo itatoa fursa kwa Wananchi, hususan waumini wa dini ya Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya kwa ibada, dua na matendo mema pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuijaalia Zanzibar na Tanzania kwa ujumla amani, umoja na ustawi.

Alhaj Dkt. Mwinyi amewataka Wananchi kuutumia mwaka mpya huo kujitathmini, kuimarisha uchamungu, kusaidiana na kuendeleza maadili mema yanayojenga familia na Taıta lenye mshıkamano.

Aidha, amezitaka Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi, Waajiri na Wananchi wote kuzingatia tangazo hilo kwa mujibu wa taratibu zilızowekwa.Rais Dkt. Mwinyi amewatakia Waislamu na Wananchi wote heri ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1448 Hijria, akimuomba Mwenyezi Mungu aufanye kuwa mwaka wa kheri, amani, afya njema na maendeleo kwa wote.
 
Zanzibar sio sehemu ya muungano.
 
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakari Zubeir Ally amemuomba Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kumshawishi Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili mapumziko ya Mwaka Mpya wa Kiislamu Hijiryya yawe Nchi nzima.

Mufti ameyasema hayo leo Juni 15, 2026 mbele ya Rais Dkt. Mwinyi wakati wa mwendelezo wa Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu visiwani Zanzibar.

“Mimi nitumie nafasi hii kwamba mapumzo tunayaomba pia na kule Bara yaenee kwasababu Nchi ni moja, hii inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaomba na sisi ieneee Tanzania nzima kwa kuwa Dkt. Mwinyi amethubutu kufanya jambo hili, namuomba Mungu awape zaidi Taufiq na uweze kumshauri Rais wa Jamhuri hili jambo liweze kuzagaa na kwa jambo hili ni sababu ya moja kwa moja kupata daraja la juu katika pepo,”amesema Mufti Zubeir.

Rais Dkt. Mwinyi ametangaza kuwa Jumatano Juni 17, 2026 itakuwa siku ya mapumziko kwa Zanzibar ili kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1447 Hijirrya.
#MillardAyoUPDATES
IMG_1474.jpeg
 
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakari Zubeir Ally amemuomba Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kumshawishi Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili mapumziko ya Mwaka Mpya wa Kiislamu Hijiryya yawe Nchi nzima.

Mufti ameyasema hayo leo Juni 15, 2026 mbele ya Rais Dkt. Mwinyi wakati wa mwendelezo wa Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu visiwani Zanzibar.

“Mimi nitumie nafasi hii kwamba mapumzo tunayaomba pia na kule Bara yaenee kwasababu Nchi ni moja, hii inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaomba na sisi ieneee Tanzania nzima kwa kuwa Dkt. Mwinyi amethubutu kufanya jambo hili, namuomba Mungu awape zaidi Taufiq na uweze kumshauri Rais wa Jamhuri hili jambo liweze kuzagaa na kwa jambo hili ni sababu ya moja kwa moja kupata daraja la juu katika pepo,”amesema Mufti Zubeir.

Rais Dkt. Mwinyi ametangaza kuwa Jumatano Juni 17, 2026 itakuwa siku ya mapumziko kwa Zanzibar ili kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1447 Hijirrya.​
 
hii nchi kwa namna ilivyo tegemezi
wafanyakazi hawakupaswa kupewa hata public holidays.
siku nikiwa rais nitafuta sikukuu zote mnazotumia kupumzika hovyo hovyo.
 
Back
Top Bottom