Nasikitika nimeshindwa kupata mwanamke wa kuoa

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Ndugu zangu..

Kwa huzuni na masikitiko makuu, ndugu yenu na rafiki yenu nakaribia kukata tamaa sasa. Nimejitahidi kutafuta mwanamke wa kuoa lakini wapi.

Kila mwanamke ninaye mpata hakidhi vigezo , japo najua hakuna mkamilifu ila hawa nakutana nao naona ni madanga tuu, ni mebet hela nyingi, akili na muda kwenye kutafuta mke sasa nimechoka kabisa.

Ndugu zangu nasikitika sana kila mwanamke ambaye unakuta labda basi anadalili za kumuoa basi ni single mama na mini sihitaji kuoa single mama

Nasikitika sana natafuta hadi mabinti wa umri kwanzia miaka 23-28 ila wapi , bhana. Wanawake wa kuoa mnawapata wapi nyie.

Nimejaribu kanisani sioni, nimejaribu kwenye vyuo huku mabinti wanao kubali ni wadogo na wapo kupiga mizinga tuu hawana hata future..

Nimezurura sana mpaka miguu inauma, nimeweka vijiwe kila mahali mpaka watu wananishanga nimekuaje sasa hivi lengo nikupata mke lakini wapi.

Natembea sana nasindikiza mabinti na shangaa shangaa huku na huko ila mwisho wasiku naishia kuambiwa "asante tuu"

Ndugu zangu nyie wake zenu mlipata wapi kwa nini mimi nakosa mke.. au na shida gani mimi.
 
Back
Top Bottom