Nashukuru Mungu kunusurika ajali leo

Uhai unathamani sana jameni kuliko kitu chochote, ukiambiwa upewe 20billion ila ikifika asubuhi utakufa hakika utokubali iyo pesa
 
Katika ajali niliyoipata mchana wa leo Jumamosi May 11, 2024..

Mwenyezi Mungu ameninusuru, na amenijalia ahuweni ya mapema kwenye majeraha mabaya niliopata kwenye mguu wangu wa kulia na kwenye michubuko michache maeneo mbalimbali ya mwili.

Nashukuru Mungu pia wahusika wengine wa ajali hiyo, ikiwa ni pamoja na dereva wangu, ambao vilevile wanaendelea vizuri. Hakuna alie lazwa hospitalini miongoni mwa wahusika wa gari tatu waliohusika kwenye ajali hiyo....

Nisingependa kumlaumu yeyote kwamba ndie sababu ya ajali ile. Sifa na Utukufu ni kwa Mungu sote tuko hai, athari za kwenye magari zinarekebishika.

Rai na wito wangu kwa watumiaji barabara wote.....

Ni vema kuzingatia sheria za barabarani, kuepuka kilevi na mwendo kasi kiholela, na daima kua waangalifu na makini barabarani, na kuhakikisha vyombo vitumikavyo barabarani ni salama, havina hitilafu zenye uwezo wa kusababisha ajali au uharibifu usio wa lazima, licha ya kwamba ajali haitabiriki na wala haitarajiwi na yeyote miongoni mwetu.....

Nawatakia safari njema watumia barabara wote humu nchi. Safiri Salama 🐒
Pole sana. Ingependeza tungejua ilikuwaje.
 
Pole ndugu na ajali,asubuhi ya leo wapo waliokuwa na mzaha wa visungura,japo sikumbuki walikuwa chawa wa wapi,ila ni matumaini yangu kuwa hukuwa umepata kileo chochote.
nashukuru sana ndugu,

mie situmii mkuu :DisGonBGud:
 
Katika ajali niliyoipata mchana wa leo Jumamosi May 11, 2024..

Mwenyezi Mungu ameninusuru, na amenijalia ahuweni ya mapema kwenye majeraha mabaya niliopata kwenye mguu wangu wa kulia na kwenye michubuko michache maeneo mbalimbali ya mwili.

Nashukuru Mungu pia wahusika wengine wa ajali hiyo, ikiwa ni pamoja na dereva wangu, ambao vilevile wanaendelea vizuri. Hakuna alie lazwa hospitalini miongoni mwa wahusika wa gari tatu waliohusika kwenye ajali hiyo....

Nisingependa kumlaumu yeyote kwamba ndie sababu ya ajali ile. Sifa na Utukufu ni kwa Mungu sote tuko hai, athari za kwenye magari zinarekebishika.

Rai na wito wangu kwa watumiaji barabara wote.....

Ni vema kuzingatia sheria za barabarani, kuepuka kilevi na mwendo kasi kiholela, na daima kua waangalifu na makini barabarani, na kuhakikisha vyombo vitumikavyo barabarani ni salama, havina hitilafu zenye uwezo wa kusababisha ajali au uharibifu usio wa lazima, licha ya kwamba ajali haitabiriki na wala haitarajiwi na yeyote miongoni mwetu.....

Nawatakia safari njema watumia barabara wote humu nchi. Safiri Salama 🐒
Pole sana.Tungekukosa aisee!Sijui nani tena angekuwa anaweka vingedere kwenye paragraphs zake!
 
Pole sana!

Katie sadaka ya shukrani na Mtumishi aombe nayo Ili ulinzi uimarishwe kwako kuelekea 2025!!

Coz wingu la kuelekea 2025 no jekundu sana na halitabiriki!!

Washindani wako jimboni wanaweza wakawa wameanza kazi!
shukran sana mkuu,

nimeamka salama, na hivi ninatokea huko uliposhauri ibada ya kwanza kabisa,

asanti kwa kunipa moyo:ClapHD:
 
pole sana boss Tlaatlaah nakuombea kwa Mungu akurejeshee afya njema ya kimwili na kiakili.

Pia wale wote walioguswa na Ajali hiyo nawaweka mikononi mwa mikono ya Kristo wakawe na amani na afya tele.

Pia naomba usogee inbox nina ombi moja private sana kwako
 
Back
Top Bottom