Display Name
JF-Expert Member
- Feb 11, 2014
- 423
- 451
Jamani naombeni ushauri kwenye hili.
Mimi kwa sasa naishi nyumbani kwa dada yangu ambapo ameolewa na ana watoto wawili wa kwanza ana miaka 9 na mwingine 6. Dada yangu hakufunga ndoa na huyu mwanaume (kanisani wala msikitini). Walianza tu kuishi kuisha huko zamani na baada ya miezi michache dadangu akawa mjamzito(mtoto mwenye miaka 9) ndo ukawa mwanzo wa maishi yao ya pamoja mpaka leo.
Sasa shida ipo hapa, huyu shemeji akawa na tabia za kuchepuka chepuka, watu walianza kusema wa hapo mahali tunapoishi kwa upande wangu nikawa siamini kabisa maneno yao hadi mambo yakawa mambo(kiasi kwamba hadi dadangu akawa anajua kuwa shem huyo anamcheat). Wakati mwingine hao wasichana wakawa wanampigia simu dadangu na mtukana maneno makali na kumwambia awapishe hapo nyumbani wenyewe waje waolewe(coz dadangu hajaolewa kiimani).
Hayo maneno aliyokuwa akitukanwa dadangu na hao wasichana yalikua hayamshughulishi shem wangu kwani hata hivo alionyesha wazi kuwa anachepuka na wala alikua haogopi na hakuwa anasikiliza ushuri wa mtu. Vikao vilifanyanywa vikihishisha ndugu zetu na ndugu wa mwanaume lakini haikusaidia. Haya yote wakati yanatokea dadangu alikua tayari ana watoto wawili na yalikua yakiendelea kwa mda wa miaka isopungua mitano. Muda wote huo tukawa tunamshauri(dadangu) afanye utaratibu wa kuachana na huyu mwanaume but yeye alitoa sababu nyingi za kuendelea kubaki pale hiyo hakuondoka.
Mimi nilikua nasoma chuo flani hivo nilikua wakati mwingine narudi hapo home kusalimia ila kutokana na hiyo nyumba kuwa haina amani wakati mwingine nilikua natamani hata nisiende pale ila nikawa naenda sababu nampenda sana dadangu na wale watoto afu nikwa namwonea huruma mno kwamba atakua mpweke, coz hapakua mbali sana na chuo wakati mwingine nilikaa hapo weekend na hata week days nikawa natokea hapo kwenda chuo.
Nilikua na rafiki yangu tunasoma pamoja ambaye kwao yeye ni mkoa mwingine so nikawa napenda kumualika anakuja nyumbani hapo siku za jumapili au jumamosi tunashinda pamoja hapo nyumbani afu anarudi hostel. Huyu rafikiangu akaanza mahusiano na shem wangu, mimi nikaja kujua kama baada ya mwezi hivi, niliambiwa na rafiki yangu mwingine. Nilipomwuliza akakubali, sikuwa na cha kumfanya zaidi nilimwambia nilivyoumizwa na kitende hicho na hata hivo hatukuweza kuendelea na urafiki. Dadangu alishangaa ana aliniuliza kwani haji tena nyumbani nkasema amepata marafiki wengine hua anaenda huko. sikumwambia dadangu yaliyotokea coz angeumia sana afu mi nilikua najilaumu coz mi ndo nimemtambulisha yule dada hapo nyumbani(hiyo ilikua mwaka jana km wa 7). Tukamaliza chuo kila mtu akaende upande wake.
Juzi dadangu amepata habari kwa mtu ambaye alifahamu kuwa shem alitembea na yule rafiki angu , alafu huyo mtu akamwambia kuwa hata mdogo wako anafahamu(yani mimi), dadangu alisikia uchungu sana na aliita(maana nilikua nimeenda kumsalimia mama mkubwa), nilipokuja nyumbani nilimkuta dadangu amelia kiasi kwamba hadi macho yamevimba, akaniuliza kama shem alitembea na yule dada na kama mi niliua najua. Kiukweli nilistuka kuona amepata hizo habari afu nguvu ikanijia nikakataa katakata kuwa sifahamu wala sijasikia coz alikua ananilaumu kwa nini sikumwambia. Nilikataa hadi nikalia coz wakati nakataa lakini roho ilikua inaniuma mno kuwa namdanganya zaidi na zaidi.
Leo nimeamka roho inanituma nimwambie ukweli but naogopa kuanzisha hiyo mada hivo sina raha mie mwenzenu, napata maumivu makali nikimwona shem na zaidi napata maumivu makali nikimwangalia dadangu mana kuna watu wanasema hadi leo rafikiangu na huyu shem wanaendelea na uhusiano.
NAOMBENI USHAURI WENU NIFANYEJE. NIMWAMBIE DADA ILI NIPATE AMANI AU NIBAKIE HIVI HIVI HUKU NAJUA UKWELI NA PIA WATU WANASEMA BADO WANAUHUSIANO?
Nifanyeje jamani, naombeni msaada wenu.