Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 2,992
- 5,660
Bado nashindwa kumwelewa Mwamposa kwa kauli yake ya kutaka Serikali ichuje maudhui ya Mitandao ya kijamii
Ni kazi gani hii ambayo haijawahi kuonekana tangu dunia iumbwe? Unawezaje kuchuja maudhui yote yanayochapishwa mitandaoni?
Ni binadamu wa aina gani ambao hawajawahi kuonekana duniani watakaokuwa na uwezo wa kusoma maudhui yote yanayochapishwa Facebook au Instagram na kuchagua yale mazuri tu huku mabaya yakifutwa?
Kampuni ya META ina mfumo wa algorithm wa kukagau maudhui lakini hauwezi kusoma maudhui yote unategemea kupokea report pia
Bajeti ya kuweka teknolojia ya algorithm ndani ya bidhaa za META haikuwa chini ya trilioni 100 lakini uwezo wa algorithm ya kuchuja maudhui ukomo wake ndiyo huo
Anachokitafuta Mwamposa ni kipi kama sio kuendelea kusababishia matatizo kampuni za mitandao ya kijamii mfano JF, META, X Corp na wengineyo?
Sijapata kujua ni mtu wa aina gani asiyeweza hata kuheshimu uwekezaji wa kampuni za mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii inaendeshwa kwa mamilioni ya fedha na sio bure. Kuweka mtandao hewani kwa mwezi ni mamilioni ya fedha na usipoyalipa basi mtandao wako unakua off
Kauli kama hizi ndizo zilizoipelekea JF kupitia matatizo makubwa miaka ya nyuma zinafaa kukemewa kwa nguvu zote.
Soma Pia: Mwamposa ataka Mitandao ya Kijamii idhibitiwe. Adai inafanya watu kuwa wavivu
Jambo linalonisikitisha ni namna JF wanavyoteseka kuhariri maudhui hii ni kazi kubwa sijapata kuona na huwa nawaonea sana huruma, META nao wanateseka tangu zamani kwa kulipishwa fines kila mara
Miaka ya nyuma walitokea viongozi wapuuzi wakaanza kushambulia mitandao ya kijamii ikapeleka matatizo makubwa sana kama mitandao kufungiwa huduma na utitiri wa kesi Mahakamani. Fikiria mwanzilishi wa mtandao aliwekeza kiasi gani cha fedha kuuweka mtandao hewani, ni bills za million ngapi analipa kila mwezi ili uwe hewani?
Leo mtu anatoka huko anaanza kutapika ujinga. Badala ya kuishauri Serikali ipambane na wavunja Sheria za mitandao anaharibu mtandao mzima kana kwamba watumiaji wote mitandaoni wanafanya upuuzi. Wafanyabiashara wangapi wanatumia mitandao kuuza bidhaa zao je ni Wananchi wangapi wanapata huduma zao mitandaoni? Stupid mind
Alihangaika X ifungiwe wakati algorithm ya X inakuletea maudhui uliyoyachagua wewe, ni nani anayependelea kufuatilia maudhui ya michezo akaletewa picha za uchi? Picha za uchi zinakuja pale mtumiaji anapokuwa na tabia ya kuzitafuta.
Ni Trillion ngapi Elon Musk amewekeza X leo unaanza kuharibu uwekezaji wake kwasababu ya watumiaji wachache wanaofuatilia mambo ya hovyo.
Je ni mamilioni mangapi ya watumiaji wanafanya biashara katika mtandao huo? Kwahiyo mtandao mzima ufungwe kwasababu ya watumiaji wachache wanaofuatilia mambo ya hovyo? Je hawa wanaofanya mambo ya maana haki yao unaipeleka wapi?
Unahukumuje watu wote kwasababu ya makosa ya watu wachache?