Nashindwa kumwelewa kwakweli

Nashindwa kumwelewa kwakweli

Challya

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2019
Posts
469
Reaction score
609
Habari wana JF,poleni na harakati za kulijenga taifa.
Naombeni ushauri wenu kwa haya yanayonikuta sasa. Mimi nipo kwenye uhusiano na msichana ambaye kiukweli nampenda sana na nipo tayari kumuoa mda wowote, sina mwingine zaidi yake ila mambo anayonifanyia nashindwa kumuelewa. Mwanzoni tulikuwa tunapendana sana alikuwa hana tatizo ila amekuja kubadilika ghafla na mimi huwa nampa mahitaji yake yote anayohitaji hata ndugu zake huwa nawasaidia,na nimeshamtambulisha kwetu anajulikana na kwetu wanampenda sana ila visa vyake ni hivi;
1. Huwa nataka sana kufanya mpango wa kwenda kwao kujitambulisha rasmi lakini yeye anakataa,yaani hataki kabisa.
2. Huwa hataki kabisa niguse simu yake,nikigusa tu anakuwa mkali kama pilipili ila mimi huwa nipo muwazi kwake kwa kila kitu,mambo yangu ya maendeleo namuhusisha lakini haonyeshi interest, simu yangu huwa namuachia muda wowote akitaka.
3. Pia ana tabia ya uongo sana, yaani unaweza kumuuliza yupo wapi akakwambia yupo nyumbani ila nikimpigia simu dada yake kumuuliza naambiwa hayupo,ni mengi sana ameshanidanganya mimi,mengi sana,sio mkweli kabisa.
4. Ana tabia anatoka kazini anapitia sehemu zake huko anazojua anarudi nyumbani kwao usiku mida ya saa nne au saa tano usiku,kwao wenyewe wameshamchoka na tabia zake,wanamlalamikia sana(Anaishi na mama yake tu,amelelewa na single mother)
5. Nilikuwa nimeshafanya mpango kabisa wa kumvisha pete ya uchumba ila huwezi amini alikataa
7. Huwa nikimwambia tutoke out huwa anasema anakuja lakini hata haji(Mara nyingi tu ameshanifanyia hivyo)
8. Baada ya kuwa nae kwa miezi minne nikamgusia kuhusu suala la kufanya mapenzi,amekataa kabisaa anasema eti hadi aolewe ndio atafanya na sio kwamba ni bikra,sio bikra..amekataa kabisa.
9. Huwa sijawahi kuacha kumpa chochote anachohitaji,mm naona ni kama tu ananitumia ili mambo yake yaende sawa lakini hanipendi...maana kama ni kuhitisha pesa anahitisha sana
10. Nikiwa nachat nae,yaani text zinajibiwa polepole hadi kero,namtumia text inajibiwa baada ya madakika au lisaa,halafu yupo kabisa online
11. Yaani hayupo romantic kabisa,daahh yaaani huu uhusiano sioni nafaidika chochote,sifaidiki chochote kabisa hapa,naloose tu na kupata stress kila siku
12. Huwa ananiudhi sanaa na huwa ninapomwambia tuachane,huwa anakuwa mnyonge na kunibembeleza vya kutosha turudiane,atawatumia watu mbalimbali kuongea na mm,analia machozi na kuahidi kutorudia,sasa unakuta tu namsamehe na kurudiana nae lakini baada ya muda anarudia yaleyale tena.
8. Yaani ni mrahisi sana kuomba msamaha ila ni mrahisi sana kurudia kosa.
9. Halafu naamini sisi wanaume mwanamke ambaye una malengo nae huwezi kumruhusu avae hovyo,ila sasa yeye mavazi anayovaa hayana maadili ila nikimwambia ni mbishi kupindukia.
10. Halafu huwezi amini na kanisani huwa hakosi,anajua kusali sana na huwa anasoma biblia sana...huyu simuelewi kweli.
11. Halafu ni mtu ambaye hata status anazoweka Whatsapp hazina maadili kabisa,yaani hadi huwa namuuliza hivi wewe huna watu wa heshima huku,huna aibu lkn ni mbishi hasikii
12. Kiufupi ni mtu ambaye inaonyesha hana interest na mm.
13. Pia ni mtu wa hasira sana, yaani huwa anaongea na mimi kwa hasira lakini watu wengine anaongea nao kwa kucheka
14. Company yake ni ya wasichana walioshindikana, yaani ambao hawajiheshimu

Wakuu ni visa vingi huyu msichana amenifanyia,hivi ni baadhi tu. Ni miezi saba sasa tangu niwe nae ila kila siku ni visa, mimi nahisi atakuwa na wanaume wengine ila mimi atakuwa tu ananitumia kujinufaisha kiuchumi tu....sasa nataka niachane nae kabisa na hata nimblock kabisa ijapokuwa nampenda sana,wakuu naumia kwasababu nimekuwa muaminifu sana kwake,sijawahi kumcheat...kweli huyu dada atajuta sana,bado ana akili za kitoto,hajajua anachotaka huyu.
NISHAURINI TU,JE MWANAMKE KAMA HUYU UNAMCHUKULIAJE NA JE USHAKUWA NA MTU KAMA HUYU?
1562433291578quote.jpeg
 
Ana Umri gani?unatongoza kizamani wewe....utaishia kutunza tu tafuta darsa ufundishwe
 
Hiyo dhana ya kusema unampenda sana ndo inayokufanya ushindwe kumwacha na amegundua udhaifu wako dats y anakunyanyasa achana nae huyo sio mwanamke ni Malaya ,hapo unatafuta kufa mapema ,kama hela unayo utapata mwanamke mwingine atakayekujali na kukuheshimu achana na huyo Malaya wako
 
Even though no one promised that life would be fair. But why can things like this happen to someone with a good and caring heart like yours?

Achana nae tu huyo anakupotezea muda na rasilimali zako
 
Yote hayo alokufanyia bado tu unataka kumuoa? Rangi gani mpk sasa hujaona maana ameshakuonyesha rangi zote na wewe bado unamn'gang'ania? Nyie ndio kwenye ndoa mnachinjaga wake zenu wakati tabia mbaya ulishazijua toka mwanzo na ungeweza kujiepusha nae
 
Itakuwa hajamfikisha mkuu jitafute!mwanamke ukimkuna jinsi anavyotaka hata ukimtukana na bado atakuomba msamaha
 
Nimesoma no 1,2 3 tu bado unaomba ushaili? kila siku nasema mwanaume kulialia mapenzi ni ujinga nivyema tukatumia akili tuachane na hisia madem walivyo wengi ivi unalia lia kisa bwege mmoja uliekutana nae una meno 32
 
Ss mpk hapo unaitaji nn tena zaidi ya kujitakia stresss!!!dalili zote za udangaji zipo mezani kwako
ushauli muache tena mwambie akimaliza akutafute
 
Sasa kama umeshajua na ukaisema kwenye number 12 ..unataka nini tena mkuu. Iyo mali haikufai fanya juu chini uforce mzigo then lala mbele
 
Kama kusoma huwezi ,ina maana hata picha huoni mkuu???
 
Hii ID mnatumia watu wawili tofauti?

Huyo mwenzako ana akili kuliko wewe.
 
Back
Top Bottom