Nashindwa kumwambia kuwa mdomo wake unatoa harufu

Display Name

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
423
451
Habari wakuu,
Nina ndugu yangu ambaye ni binti mzuri na anaakili vizuri na uwezo mzuri sana wa kufikiria.

Anatatizo la mdomo kunuka ila yeye mwenyewe hajui kama anahilo tatizo. Mimi huwa navumilia sababu ni ndugu yangu na pia napata woga wa kumwambia kwamba mdomo wake unatoa harufu kali kwa sababu ni msichana msafi mno na anayejijali ila tu naona hapo kwa mdomo ndio kuna shida.

Nimewahi kukutana na mdogo wa ex wake akaniambia kaka yake alikua hapendi/hafurahishwi na harufu yake ya mdomo ila huyu ex hakuwahi mwambia bidada.

Natamani kweli nimsaidie kwenye hili ila nakusa jinsi ya kufanya ukizingatia naogopa kumwambia. Kuna kipindi kuna mtu aliniekeza dawa flani hizi ya meno nikaiweka hapo ili tuwe tunatumia pamoja ili imsaidie kiukweli ile dawa haikua na ladha nzuri mdomoni yeye akaenda kununua nyingine akasema ile ni mbaya.

Sasa nashindwa namna. Nifanyeje? Au nichune tu nimwache na tatizo lake kila mtu eendelee na maisha yake.
 
Jamani, hilo nalo linahitaji ushauri kweli???!
Ni ndugu yako, hajui kama anatatizo hebu fanya kumsaidia basi. Mwambie kama ni tatizo aende kupata matibabu, maana inawezekana anaswaki vyema tuu ila bado hiyo harufu inakuwepo.
Huyo aliyemwacha nae ni Bashite tuu hana lolote, yaani kumwambia mpenzi wake kuwa ana tatizo fulani ameona tabu hadi amwache jamani!!? Hakuwa na mapenzi ya dhati kabisaa. We mwambie usiwe na wasi wasi tena atakushukuru mno
 
d13f83c72282c613e04ff8e7a5709ea6.jpg
4c5a617719e18c88f7f8f351a017201d.jpg
695d87a74a19d6e1fff9c65d120108e2.jpg
 
Please atamimi nilikuwa na hilo tatizo mwambie hatumie hizo lister na baada ya kupiga mswaki ndy aweke kwenye kifuniko asukutuwe baadae ateme na apige mswaki asubuhi na wakati wa kulala nenda supermarket zinapatikana
 
Please atamimi nilikuwa na hilo tatizo mwambie hatumie hizo lister na baada ya kupiga mswaki ndy aweke kwenye kifuniko asukutuwe baadae ateme na apige mswaki asubuhi na wakati wa kulala nenda supermarket zinapatikana

ipi ni nzuri hapo naona zipo na rangi tofauti tofauti
 
ukishindwa kabisa kumface tafuta namba ngeni mtumie ujumbe elezeq yote muelekeze hadi dawa ya kutumia muelekeze jinsi gani aprove kama kweli kinywa chake kinatoa harufu ye mwenye ataenda kutafuta dawa kimya kimya ukishindwa kuandika na ujumbe kwa namba ngeni basi nawewe kinywa chako kitakua na shida
 
Ni nduguyo na unashindwa mwambia??? Tumia lugha ya upole umwambie.
Unaweza ukafanya kama utani wakati mnacheka na kumwambia "leo huswaki" akisema kaswaki unamjibu "mbona mdomo unatoa harufu hivyo!?"
Natumiaga hii njia and it works. Kama alipiga mswaki atajistukia kua ana tatizo.
 
Tatizo LA kunuka mdomo linaweza sababishwa na mchafuko wa tumbo, au throats sijui kwa kiswahili na pia kutokupiga mswaki vizuri, kinachotakiwa kumwambia ukweli na inabidi aende kwa dentist akachunguze chanzo ni nini? Au atumie halimeter kipimo cha kupima kama unatoa harufu.
 
Back
Top Bottom