Nashindwa kumuelewa Mpenzi wangu

Nashindwa kumuelewa Mpenzi wangu

Papaa Tony

Member
Joined
Aug 21, 2013
Posts
65
Reaction score
48
Habari zenu wana JF.

Hii ni mara yangu ya kwanza kuomba ushauri kwawana jamvi.

Natokea mkoani mara. Kinachonitatiza ni kwamba, nina mpenzi ambae tumedumu nae kwa muda mrefu sasa lakini kuna kipindi tulipotezana kwamuda wa miaka mitatu.

Nahii ni baada ya yeye kuhamishwa shule na kwenda kusomea sehemu ambayo sikuijua. Kwao ni shy-town na mm ni mara. tulikutana shuleni na kuanzisha mahusiano.

kwakweli nilimpenda sana na hata alipokua akiondoka aliniahidi ipo siku tutakutana.

Tatizo linakuja baada ya kumaliza masomo. nilijitahidi kumtafuta na mwisho nilimpata tena.

Nilimuuliza kama anampenzi akaniambia alimpata lakini anamzingua. niliumia sana lakini akaniahidi kua hatarudia kunisaliti.

Sasa yapata mwezi na siku kadhaa nikimpigia simu inakua bize muda mwingi na ninapompata ananiambia nisubiri ana kazi atanitafuta. hakuna siku anayonitafuta na nikirudia kumpigia anakua mkali sana nakuniambia kama simuamini nitafute mwingine nawakati huo nikimuudhi analalamika na kuniambia simpendi. NIFANYEJE? naomba ushauri
 
hapo huna huyo unaemuita mpnz!fanya mipango mingine mkuu sanasana anaona unamkera tu'we kaa kimya uone kana atakutafuta usiumize kichwa!
 
Dogo piga chini, utakufa siku siyo zako.Shauri yako!!!
 
Nimekusoma mkuu. Ajabu ni kua nisipompigia simu ananilalamikia sana. Yaani analaumu mpaka kero. na nikipiga ndo hivyo utasikia mara ooo nilikua naongea na baba mara mama, ooo sijui rafiki yangu tulisoma nae.
 
Muache ana mpenzi wake huyo
we anakuweka pending in case akiachwa....concluded!!!
 
Habari zenu wana JF. Hii ni mara yangu ya kwanza kuomba ushauri kwawana jamvi. Natokea mkoani mara. Kinachonitatiza ni kwamba, nina mpenzi ambae tumedumu nae kwa muda mrefu sasa lakini kuna kipindi tulipotezana kwamuda wa miaka mitatu. Nahii ni baada ya yeye kuhamishwa shule na kwenda kusomea sehemu ambayo sikuijua. Kwao ni shy-town na mm ni mara. tulikutana shuleni na kuanzisha mahusiano. kwakweli nilimpenda sana na hata alipokua akiondoka aliniahidi ipo siku tutakutana. Tatizo linakuja baada ya kumaliza masomo. nilijitahidi kumtafuta na mwisho nilimpata tena. nilimuuliza kama anampenzi akaniambia alimpata lakini anamzingua. niliumia sana lakini akaniahidi kua hatarudia kunisaliti. sasa yapata mwezi na siku kadhaa nikimpigia simu inakua bize muda mwingi na ninapompata ananiambia nisubiri ana kazi atanitafuta. hakuna siku anayonitafuta na nikirudia kumpigia anakua mkali sana nakuniambia kama simuamini nitafute mwingine nawakati huo nikimuudhi analalamika na kuniambia simpendi. NIFANYEJE? naomba ushauri

Sio kwamba iko bize, ni amekublock.
 
Haihitaji akili nyingi kugundua kinachoendelea mkuu, Kifupi tayari UMEPIGWA chini...! Mapenzi ndivyo yalivyo
 
Mkuu hili mbona halihitaji kuomba hata ushauri? Hapo huna chako.
 
Noo! Hajaniblok Bali ni kweli anakua anaongea na mtu, sema hajui ku-activet waiting call. ila hua nategea tu akimaliza kuongea tu simu yake inaita, hapo ndo majanga yanaanzia.

Amewapanga kwa madaraja ya div 1,2,3,4,5 na wewe katika madaraja yake ni Div 5 yake
 
Back
Top Bottom