Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 76,284
- 108,300
athante thana
Una umri gani binti?
athante thana
emmy 2nyi pole sana kwa yaliyokukuta. Kupoteza mtu umpendae ni tukio ambalo karibu wote tutakutana nalo kwenye maisha yetu. Ni tukio ambapo halitaepukika kwa wengi. Kwa hiyo, hauko peke yako. Hapo ulipo labda utakuwa umeshajiuliza kwa nini hili limetokea kwako? Why you? Lakini muda huu kuna watu wengi wengine wamepoteza wawapendao. Wengine ndiyo kwanza wamepoteza wawapendao dakika mija iliyopita na wako kwenye vilio. Tatizo hatuwafahamu lakini wapo somewhere.habari zenu wana jamvi., mwenzenu nlikua na mpenz 2lopendana sana kwa bahati nzur mwenyez mungu kamchukua.ni miez ming toka aondoke duniani lakin siku zote najawa na mawazo mpaka nahisi nachanganyikiwa thatha.. nsaidien jaman nifanye nin il mawazo angalau yapungue maana daaah...
yesu atampata wapi saivi?
emmy 2nyi pole sana kwa yaliyokukuta. Kupoteza mtu umpendae ni tukio ambalo karibu wote tutakutana nalo kwenye maisha yetu. Ni tukio ambapo halitaepukika kwa wengi. Kwa hiyo, hauko peke yako. Hapo ulipo labda utakuwa umeshajiuliza kwa nini hili limetokea kwako? Why you? Lakini muda huu kuna watu wengi wengine wamepoteza wawapendao. Wengine ndiyo kwanza wamepoteza wawapendao dakika mija iliyopita na wako kwenye vilio. Tatizo hatuwafahamu lakini wapo somewhere.
Suala lako lipo zaidi kwenye kukabiliana na kumpoteza umpandaye. Wako ambao wata-recover mapema, lakini pia wapo ambao itawachukua muda mrefu ku-recover. Kama alivyouliza Asprin hapo juu, sababu iliyosababisha mpaka umpendaye akapoteza maisha inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ku-recover.
Hata hivyo kuna mambo mengi yanaoweza kusaidia kuondokana na hali ya kujikuta unaomboleza kwa muda mrefu. Unaweza kujiuliza, je, bado unaomboleza na kwa nini bado unaomboleza? Walio karibu yako wanaweza kukusadia katika kujuia jinsi ya au kutoomboleza kabisa. Wengine watakushauri kuwa uwe strong zaidi, usahau yaliyopita au uendelea na maisha yako kama kawaida. Wengi hawatakukuhamasisha uendelee kuomboleza ili umalize kuomboleza naturally badala ya kulazimisha kuacha bila matakwa yako wewe mwenyewe. Bora kuwaambia kuwa unayeomboleza ni wewe na siyo wao.
Kuomboleza ni zaidi ya feelings zako. Inawezekana bado huamini kama umempoteza umpendae. Unaweza kuendelea kufikiria hivi kwa muda mrefu kutokana na mambo uliyofanya na marehemu mkiwa pamoja. Hili linaweza kukuathiri kimwili pia. Unawezajikuta unakonda kwa kufikiria mno, kuumwa kichwa, kulala mno, kukaa tuu bila kufanya chochote, n.k. Watu wengi wanaomboleza huwa wanapenda kukaa peke yao, japokuwa wapo wengine ambao wanapenda kuwa karibu na watu wengine. Wakati mwingine unaweza kuhisi umpandae yupo karibu nawe. That is normal.
Jambo la muhimu ni kukumbuka kuwa wewe ni mtu wa aina yake, una personality yako, experiences zako za maisha, ulikuwa na mahusiano special na marehemu, uelewa wa kipekee kuhusu maisha na vifo. Hiyo, uko tofauti na watu wengine na utaomboleza tofauti na watu wengine wanavyoomboleza. Hivyo, siyo kosa kwa kushindwa kumsahau. Inaweza kuchukua muda kumsahau.
Pamoja na wewe kuwa unique, upo wakati ambao utajua jinsi mwenendo wako wa kuomboleza unavyoendelea, hasa kama kifo cha umpendaye kilikuwa cha ghafla mno. Kila kitu kitaonekana kama siyo siyo real kweli. Upo wakati ambao utakuwa na masikitiko sana, kujisika kama mtu usiyekuwa na msaada wowote, kuwa na uoga, hasira, kujilaumu, maisha kuwa ovyo, n.k. Haya mambo yatakuja na kuondoka taratibu.
Chukulia, kwa mfano, yaliyokutokea kama ndege aliyekuwa amepunzika kwenye tawi la mti. Alikuwa anapenda na kufurahia sana kupunzika kwenye hilo tawi. Pia hilo tawi lilikuwa ni sehemu ya kujikinga na wanyama wakali na wale wawindaji wanaotumia manati kutungua ndege kwenye miti.
Hata hivyo, siku moja ukaja upepo mkali sana na kuvunja lile tawi. Ndege hakuwa worried sana kwa sababu alijua mambo mawili muhimu. Kwanza, hata bila ya lile tawi angeweza bado kupaa na kubakia salama kwa nguvu za mabawa yake. Pili kulikuwa na matawi mengine kwenye huo mti ambapo angeweza kujipunzisha pale kwa muda.
Mfano huu mdogo unajaribu kuonyesha mahusiano yetu kama wanadamu. Tunayo haki ya kufurahia mahusiano yetu kila tukipata nafasi, lakini hatwezi kwa sababu tunategemea sana kwenye hayo mahusiano na huwa tunaogopa sana kama tukimpoteza yule tumpendae. Nguvu zetu hazipo kwenye vitu vya nje bali kwenye mabawa yetu mawili: Mapenzi na busara.
Wakati unaendelea kuomboleza kwa kumpoteza umpendae (sikushauri uache), pia jaribu kutakafari yafuatayo:
Kutakafari haya masuala kunaweza kukusaidia kubadilisha style yako ya maisha yako, kuishi maisha ya maana hasa ya kuwepo hapa duniani, kupanua wigo wa tabia yako, purify your love au hata kuchunguza kwa undani ukweli wa maisha. Unaweza kugundua kuwa maisha ni ya maana sana kama tuu utakuwa unayaishi kwa kuthamini zaidi maisha ya wengine na mahitaji yao.
- Kumpoteza mtu ni sehemu ya mzunguko wa maisha yetu. Yoyote anayezaliwa ni lazima afe. Chochote kinachokua lazima kioze. Mara nyingi tunasahau kuwa miili yetu ni mortal.
- Inabidi tujiulize kifo ni nini? Kifo kinasabishwa na nini?
- Nini maana ya maisha? Madhumuni hasa ya maisha ni yapi? Kifo kinatulazimisha kufikiria kwa undani maana hasa ya maisha. Jaribu kutumia muda wako kwa kuangalia madhumuni hasa ya kuishi. Utakuta kuwa ipo siku wote tutakufa pia.
On the other hand, nilishahudhuria ibada ya mazishi ya mtu wangu wa karibu, mchungaji akasema kuwa huwa anashangaa sana pale watu wanapotaka kuwasahau wale wanaowapenda baada tuu ya kufariki. Akasema inabidi tusiwasahau bali tuendelee kuwakumbuka tena kila mara. Utawakumbukaje, mchungaji alidai kwa kututukuza na kuyaendeleza yale yote mazuri ambayo marehemu alikuwa anayafanya au alikuwa amepanga au kutamani kuyafanya. Kama marehemu alikuwa anathamini zaidi maisha ya wengine na mahitaji yao, basi usimsahau bali endelea kumkumbuka kwa hayo na ikiwezekana yaendeleze kwa niaba yake.
habari zenu wana jamvi., mwenzenu nlikua na mpenz 2lopendana sana kwa bahati nzur mwenyez mungu kamchukua.ni miez ming toka aondoke duniani lakin siku zote najawa na mawazo mpaka nahisi nachanganyikiwa thatha.. nsaidien jaman nifanye nin il mawazo angalau yapungue maana daaah...
sthante sana mkuu kwa maneno yako mazuri,ntaufanyia kazi ushauri wako wenye baraka na neema ndani yake.. mwenyez mungu akubarik
Una umri gani binti?
Tupo kwa majonzi ujue
Nahisi kama yu ngali mdogo, sasa akiendelea kuishi katika majonzi kama hivi si ajabu akapata tabu kwenye mahusiano mengine.
Thatha afanyaje?thiunajua tena thikitiko la mahaba