Hivi na wewe ni mtanzania? Sikusomi kabisa yaani
Mke wa mtu ameingiza hasara gani kwa taifa hili?? We talk issues of public interest, not personal attack.!
tanzania haina wanasheria hao ni maboga tu. Haiwezekani kila kesi tunashindwa
Acha ulevi,mpaka kesi inamfikia mwanasheria,kuna mengi yametokea,wewe umeangalia mtiririko wa ushahidi? Kwa taarifa yako si kazi ya mwanasheria kupika ushahidi ila kazi yake ni kuisadia mahakama kufikia maamuzi ya haki, na wala sio kuilazimisha,na anayeamua kesi ni jaji sio mwanasheria. Kuna kesi ngapi tunazijua serikali inajenga shule eneo la mtu bila fidia ikienda mahakamani inashindwa? Hata hiyo ya samaki ni kesi za wanasiasa kulazimisha ziende mahakamani wakati mwingine bila kusikiliza ushauri wa wanasheria ili kufuta aibu. Kwa akili zenu serikali ikifungua kesi lazima ishinde? Ili nani ashindwe? Raia? Kama ni hivyo ni bora mahakama zisiwepo na iwe inashinda moja kwa moja. SERIKALI KUTOKANA NA MABAVU YAKE HUWA INAKUWA IMESHAHARIBU KILA KITU NA WAKILI WA SERIKALI HUWA AKIENDA MAHAKAMANI MARA NYINGI ANA MITIGATE TU,ANAPUNGUZA MAKALI YA MAAMUZI
Hawa ndio wanasheria wa serikali ukoo wa Werema unategemea akasimame na Lisu, Msando, Marando n.k??Samaki ulishakula sasa unapiga kelele
Wewe ni mburura wa mwisho kabisa usiyejua kitu,embu tuambie kesi gani yenye maslahi ya taifa hawa wanasheria wa serikali wamesimamia na wakashinda?
Haiingii akilini kwa kesi yenye maslahi makubwa kwa serikali yetu kama hii ya samaki waliokamatwa kwenye meli iliyovua kweny bahari yetu bila kibali, kuambiwa kuwa serikali imeshindwa kesi na hivyo serikali yetu inadaiwa matilioni ya pesa. Yaani mwizi atuibie harafu tumlipe matilioni na amekamatwa na kidhibiti. Kwangu naona kuna haja serikali ifanye uchunguzi wa wanasheria wake waliosimamia kesi hii isije ikawa tumehujumiwa ili kuiangusha serikali na wao wale cha juu. Swali kwa wanasheria wa serikali: je kwa nn katk kesi nyng zinazoikutanisha serikali na watu binafsi, kwa asilimia kubwa watu binafsi wanashinda. Je, serikali inaajiri incompetent lawyers ukilinganisha na mawakili binafsi? au serikali inawakwamisha katika kusimamia kesi. Jamani tukumbuke na ile kesi ya Dowans kama siyo richmond tulivyoshndwa. Nakaribisha mchango naona kuna kitu hapa au labda ni uelewa wangu mdogo, naomba nifunguliwe macho
Kama ulistaajabu ya Richmond, yaone ya "Samaki wa Magufuli" sasa.
Toka lini Mwanasheria wa Tanzania akasimamia maslahi ya Tanganyika na akashinda? Ndiyo maana sisi wananchi tunataka Tanganyika ili tusimamie rasilimali za nchi yetu wenyewe, tuna uchungu nazo.