Nashauri tufungue akaunti maalam ya kuwachangia wanachuo waliokosa mkopo

kilalile

JF-Expert Member
Jun 4, 2012
1,595
2,205
Watanzania wenzangu, ni ukweli usiopingika kuwa si kila aliye na sifa ya kujiunga na chuo kikuu pia ana sifa ya kupatiwa mkopo wa elimu ya juu.

Tukumbuke hizi ni taasisi mbili tofauti. TCU imeshafanya kazi yake ya kuwapangia wanachuo kwenye vyuo.

HESLB imeshafanya kazi yake ya kutoa mikopo kwa wale wenye vigezo vilivyoelekezwa.
Sasa basi, wenye uhitaji wa mikopo hiyo ni wengi, wengine wamejitokeza kwenye media wakiomba msaada, tumewaona. Wengine wameamua kurudi makwao, tunafahamu. Wengine wameshindwa hata kuripoti vyuoni.

Wazo ni kuwasaidia vijana wetu, tufungue akaunti kuwachangia kama kweli tunaguswa na kile kinachowakuta kwasasa.

Wazo likipita, taratibu za kuratibu zoezi zitaanza.
Nawasilisha.
 
Naona umekosa mkopo wewe haya hebu weka namba zako hapa nikutumie kwa m-pesa maana unalalamika sana unashindwa tu kufafanaua kwamba umekosa huo mkopo
 
Umeonyesha moyo wa kutaka kutoa, asante.
Wazo likipita nitatoa namba.
 
Kwa sasa walio wengi wanaishi kama mashetani. Nani akuchangie??!! Thubutu.

Tuendelee kumuombea mtukufu alegeze kamba. Wananchi wanapumulia pua moja!

-Kaveli-
 
Yule dogo aliyepata One ya Nane na kakosa Mkopo imeniuma sana.
 
Hicho hicho kidogo mkuu, kutoa ni moyo si utajiri
 
Kwann mwaka huu waliokosa ni wengi kulinganisha na mwaka jana? Kwann bajeti ipungue mwaka pamoja na JPM kujinadi kuwa serikali yake inazo pesa za kutosha?
 
Watanzania wenzangu, ni ukweli usiopingika kuwa si kila aliye na sifa ya kujiunga na chuo kikuu pia ana sifa ya kupatiwa mkopo wa elimu ya juu.
Tukumbuke hizi ni taasisi mbili tofauti. TCU imeshafanya kazi yake ya kuwapangia wanachuo kwenye vyuo.
HESLB imeshafanya kazi yake ya kutoa mikopo kwa wale wenye vigezo vilivyoelekezwa.
Sasa basi, wenye uhitaji wa mikopo hiyo ni wengi, wengine wamejitokeza kwenye media wakiomba msaada, tumewaona. Wengine wameamua kurudi makwao, tunafahamu. Wengine wameshindwa hata kuripoti vyuoni.
Wazo ni kuwasaidia vijana wetu, tufungue akaunti kuwachangia kama kweli tunaguswa na kile kinachowakuta kwasasa.
Wazo likipita, taratibu za kuratibu zoezi zitaanza.
Nawasilisha.

Tunatoa kodi kubwa sana kwa ajili ya serikali,tunakatwa katika mifuko ya kijamii,juzi wametangaza kuwa asilimia ya ulipaji mikopo kwa wahitimu imeongezeka..kama serikali pamoja na nguvu zote imeshindwa kumudu gharama za kuwapatia mkopo ata kwa asilimia 60 cc wananchi na hali ilivyo ngumu utawezaje..tuisome namba tu..
 
Kwa sasa walio wengi wanaishi kama mashetani. Nani akuchangie??!! Thubutu.

Tuendelee kumuombea mtukufu alegeze kamba. Wananchi wanapumulia pua moja!

-Kaveli-

Alegezi yule jamaa..ameshasema itafika kipindi mtazoea tu..na alivyo na msimamo tutakiona
 
Kwann mwaka huu waliokosa ni wengi kulinganisha na mwaka jana? Kwann bajeti ipungue mwaka pamoja na JPM kujinadi kuwa serikali yake inazo pesa za kutosha?
Hoja yako ni ya msingi sana mkuu, ila tayari wameshakosa. Tulalamike tu kisha tunyamaze, tufanye jambo nashauri.
 
Watanzania wenzangu, ni ukweli usiopingika kuwa si kila aliye na sifa ya kujiunga na chuo kikuu pia ana sifa ya kupatiwa mkopo wa elimu ya juu.

Tukumbuke hizi ni taasisi mbili tofauti. TCU imeshafanya kazi yake ya kuwapangia wanachuo kwenye vyuo.

HESLB imeshafanya kazi yake ya kutoa mikopo kwa wale wenye vigezo vilivyoelekezwa.
Sasa basi, wenye uhitaji wa mikopo hiyo ni wengi, wengine wamejitokeza kwenye media wakiomba msaada, tumewaona. Wengine wameamua kurudi makwao, tunafahamu. Wengine wameshindwa hata kuripoti vyuoni.

Wazo ni kuwasaidia vijana wetu, tufungue akaunti kuwachangia kama kweli tunaguswa na kile kinachowakuta kwasasa.

Wazo likipita, taratibu za kuratibu zoezi zitaanza.
Nawasilisha.

Tunza familia yako na nduguzo kwanza, kama wapo sawa, kama bado hawako sawa acha kiherehere!
Chadema kwa nini wasiitumie hii fursa??
 
TCU na HESLB ni taasisi za umma ambazo shughuli zake zinategemeana. Wangekuwa serious hili jambo wangelipatia suluhu kirahisi tu.
1. TCU inadahili wanafunzi hao kila mwaka, hivyo inajua asilimia ya ufaulu ni kiasi gani. Kwa maana inaweza kufanya makadirio ya ufaulu kwa mwaka unaofuata.

2. HESLB inatoa mikopo kila mwaka, hivyo inajua idadi ya wanafunzi wanaoomba mikopo, pia inajua idadi ya wanaopata na idadi ya wanaokosa wakiwa na vigezo, inaweza kupata makisio ya miaka hata mitano mbele ya wanafunzi watakaoomba na kukidhi vigezo vya kupata mkopo.

3. Ikiwa ni hivyo, bajeti inayotosha inaweza kutengwa kwa vipaumbele vya taifa kwa kufuata makadirio yanayotokana na uzoefu wa miaka 5 - 10 nyuma.

4. Watalaamu wa kufanya hizo hesabu ndogo tu wapo, Serikali "kiziwi" haijaweka elimu kama kipaumbele muhimu.

5. Uchaguzi 2015, UKAWA elimu bure mpaka University, kiziwi elimu bure mpaka form four.

6. Wazo lako zuri, waombe Mods wasimamie ile auditing iwe inafanyika.

7. Namba imewekwa kilele cha mlima Kilimanjaro, kila mtu anaisoma kivyake.
 
Tunatoa kodi kubwa sana kwa ajili ya serikali,tunakatwa katika mifuko ya kijamii,juzi wametangaza kuwa asilimia ya ulipaji mikopo kwa wahitimu imeongezeka..kama serikali pamoja na nguvu zote imeshindwa kumudu gharama za kuwapatia mkopo ata kwa asilimia 60 cc wananchi na hali ilivyo ngumu utawezaje..tuisome namba tu..
Umeongea vizuri, je unajua mafahari wawili wakipigana nyasi ndio huumia?
Tuwasaidie vijana.
 
Yule dogo aliyepata One ya Nane na kakosa Mkopo imeniuma sana.
Mbona kuna sms zinasambaa mitandaoni kuwa kuna watu wamejitolea kumlipia ada na Hostel? Huyo hana shida tena,tuwafikirie wengine.
 
Back
Top Bottom