Bodi ya Mikopo wasijibu kwa ujumla ujumla Kiwango kidogo cha mikopo kwa wanafunzi

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,873
HESLB wamejitetea kwamba kiwango cha chini cha mkopo walichotoa kwa mwanafunzi ni Tsh2,099,500. Hi ni taarifa ya jumla jumla na haina msingi.Hiyo ni fedha ya kujikimu na hutolewa sawa kwa wote. Bodi waseme kiwango cha chini cha Ada walichotoa ni Shiling ngapi?

Mwaka huu zaidi ya wanafunzi elfu 8 wa mwaka 1 wameomba mkopo na fedha iliyotolewa na serikali ni Tsh. Bil. 570. Hivyo walichofanya HESLB ni kugawa kidogo kidogo kutaka Rais aone kwamba kiwango alichotoa kimetosha na wanafunzi wengi wamepata mkopo mwaka huu

HESLB wanapaswa kueleza kwa takwimu kiwango cha chini cha fedha ya Ada, fedha ya mafunzo na viandikwa waliyowapa wanafunzi ni shilingi ngapi? Na ni wanafunzi wangapi wamepewa Ada, fedha ya mafunzo na viandikwa na wangapi wamenyimwa kabisa.Sio kuongea kiujumla

Si mara ya kwanza kwa HESLB kutoa mkopo wa kiwango kidogo kwa wanafunzi. 2016 kuna wanafunzi walipewa hadi elf 5 kama mkopo kwa mwaka. Baada ya wanafunzi kupiga kelele 20/10/2016, saa 2 usiku Waziri Prof. Ndalichako kupitia TBC akaagiza bodi kupanga mikopo upya

Unampa fedha ya ada mwanafunzi Tsh. 400,500 hadi Tsh. 256,000 kati ya Ada Tsh. 3,000,000, kati ya 2,000,000 kati ya 1,500,000 ambayo wanafunzi wanapaswa lipa chuoni ili wasajiliwe kuanza masomo. Umemsaidia nini huyu mwanafunzi? .Huu ni mzigo kwa wazazi maskini.

BATCH-1 ya wanufaika 37731 iliwekwa wazi pia kwenye PDF umma tukaona.Aliyepewa Tsh.2,750 yupo BATCH 2 tulitarajia Bodi ingetoa PDF-Document ya orodha ya BATCH-2 kwa umma ili tujionee wote mwanafunzi aliyepewa Tsh. 2,750.Ila hadi sasa Bodi haijatoa PDF ya BATCH-2

Aliyepewa Tsh. 2,750 aliomba taarifa zake zisiwe wazi, tulitegemea Bodi itoe majina kwa umma tuone ila Bodi hawajatoa PDF ya BATCH-2 kwa umma.Badala yake wametuma taarifa za kiwango cha fedha kwenye akaunti binafsi za wanafunzi (SIPA) ili hizi kasoro umma tusizione.

Kiwango cha chini cha fedha ya Ada walichotoa Bodi ya mikopo ni Tsh.400,500 hadi Tsh.256,000 waliopewa kiasi hiki katika Ada ni wanafunzi wengi zaidi ya 90%. Mwanafunzi aliyepewa Tsh2,750 alinyimwa Ada. Tsh. 2,750 aliyopewa ni katika fedha ya field na categori nyingine.

Serikal ifahamu kwamba fedha iliyotoa kwa HESLB Tsh.Bil 570 haitoshi Fedha ni ndogo idadi ni kubwa hivyo iongeze fedha kwani kuna wanafunzi wenye sifa hawajapata mkopo hata senti, wengine wamepewa kidogo na kunyimwa categori zingine na wengine wamenyimwa ada

Hoja sio bodi ya mikopo itake kuonekana imetoa mikopo kwa wanafunzi wengi, hoja hapa ni serikali kupitia bodi ya mikopo kutoa mkopo ambao utamnufaisha mwanafunzi kusoma na kumaliza mzunguko wa elimu yake, sio kutoa ada laki 2 kama walivyotoa, ikiwa ada ya chuo kwa mwanafunzi ni Milion moja na nusu, hapo umemsaidia nini?

IMG-20211025-WA0190.jpg
 
Halafu Ndalichako na wenzake hapo wizarani wakitumbuliwa watakuja watu kusema walikuwa team SG ndio maana wametumbuliwa.
Ila kiukweli yule mama hatoshi kusimamia elimu ya nchi hii.
 
Halaf pia najiuliza na kwanini Allocation wametoa za mwaka mmoja tu kwa vijana hawa fedha haijulikani miaka mingne kama itakuepo au shida nini?
 
Halafu Ndalichako na wenzake hapo wizarani wakitumbuliwa watakuja watu kusema walikuwa team SG ndio maana wametumbuliwa.
Ila kiukweli yule mama hatoshi kusimamia elimu ya nchi hii.
Unahisi shida ni ndalichako? Kama kiwango cha pesa kilichotolewa na serikali ni kidogo, utamlaumu ndalichako?
 
Unahisi shida ni ndalichako? Kama kiwango cha pesa kilichotolewa na serikali ni kidogo, utamlaumu ndalichako?
kwani bajeti ya HESLB inasomwa na nani bungeni? Nani anayetakiwa kusema hapa hela haitoshi fungu liongezwe?
 
shida hapa ni watu kulazimisha sifa za kuonesha awamu hii wengi wamepewa mikopo wakati uwezo wa kuwapa hakuna.......
 
Nilishasema hii bodi ifutiliwe mbali maana haina msaada wowote kwa wanafunzi zaidi ya kuwabebesha furushi la misumari. Fedha za ufadhili wa wanafunzi zirudi kutolewa na wizara kwa wanafunzi waliochaguliwa kwenye vyuo vikuu vya umma pekee.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom