HESLB: Awamu ya pili 7,364 wapangiwa mikopo; wengine watapangiwa Oktoba 25

Elisha Sarikiel

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
851
1,000
heslb-login.png

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza leo (Ijumaa, Oktoba 22, 2021) orodha ya awamu ya pili yenye wanafunzi 7,364 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 19.4 Bilioni kwa mwaka wa masomo 2021/2022 unaotarajiwa kuanzia wiki ijayo.​

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru amesema kuwa orodha hiyo iliyotolewa leo inafanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza kufikia 45,095 waliopangiwa mikopo yenye kiasi cha thamani ya TZS 119.3 Bilioni.

Badru ameongeza kuwa HESLB tayari imeanza kupeleka fedha za wanafunzi hao waliopangiwa mikopo awamu ya pili katika vyuo mbalimbali na kuwataka wanafunzi kupata taarifa za kina katika akaunti walizotumia kuomba mkopo maarufu kama SIPA (Student’s Individual Permanent Account) na kujiandaa kwenda vyuoni kwa ajili ya kujisajili. “Serikali imeshatupatia fedha na tumeanza kuzipeleka vyuoni … lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi wanaopangiwa wanazikuta fedha vyuoni ambako watajisajili na kupokea ili watimize ndoto zao,” amesema Badru.

Tarehe ya kutolewa Orodha ya Awamu ya Tatu
Kuhusu kutangazwa kwa orodha ya Awamu ya Tatu, Badru amesema orodha ya wanafunzi waliopangiwa mikopo itatolewa Jumatatu, Oktoba 25, 2021 baada ya kukamilisha uchambuzi wa maombi unaoendelea na kuwataka waombaji mikopo kutembelea akaunti zao ya SIPA kupata taarifa kuhusu maombi yao.

“Orodha hii ya pili inajumuisha wanafunzi wenye sifa zikiwemo kuwa wahitaji, wameomba kwa usahihi na wamekamilisha taratibu za udahili wa chuo kimoja … tunakamilisha uchambuzi wa maombi mengine na tutaoa orodha ya tatu katika siku tatu zijazo, yaani Jumatatu Oktoba 25, 2021,” amesema Badru.

TZS 570 Bilioni zimetengwa kwa mikopo ya elimu ya juu 2021/2022
Kwa mujibu wa Badru, Serikali imetenga TZS 570 Bilioni kwa ajili ya mikopoya jumla ya wanafunzi 160,000. Kati yao, wanafunzi 70,000 watakuwa ni wanufaika wapya na wanafunzi zaidi ya 90,000 ni wale wanaoendelea na masomo baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka.

Fedha zimeanza kutumwa vyuoni
Wakati huohuo, Badru amesema HESLB imeshapokea fedha kwa ajili ya malipo ya wanafunzi na taratibu za malipo zimekamilika na fedha za wanafunzi zinatarajia kufika vyuoni kuanzia leo, Ijumaa Oktoba 22, 2021.

Wito
Aidha, Badru alisema HESLB inawasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa kwa awamu inayofuata ukiendelea.

Mwisho.
Imetolewa na:
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
DAR ES SALAAM
Ijumaa, Oktoba 22, 2021
 
cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
19,259
2,000
Hii mikopo si ya kukimbilia ni kitanzi Cha baadae nikikumbuka retention fee ilivokuwa inafanya Deni haliishi na sio kama Rais kuingilia kati ilikuwa kilio na kusaga meno, mdogo wangu nilimshauri asiombe mkopo na shule inaendelea hapo baadae hatakuja kuteseka
 
HESLB: UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA NA TAKWIMU ZISIZO SAHIHI

Tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zisizo sahihi za upangaji wa mikopo wa wanafunzi wa elimu ya juu ambazo zimekuwa zikisambazwa mitandaoni kuanzia jana, Oktoba 23, 2021.

Ufafanuzi wa jumla:
Hakuna mwanafunzi aliyepangiwa mkopo wa TZS 2,750 kwa mwaka wa masomo 2021/2022. Kati ya wanafunzi 45,095 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mkopo hadi sasa, mwanafunzi mwenye kiwango cha chini cha mkopo ni TZS 2,099,500 na kiwango cha juu ni TZS 6,431,500;

Upangaji mikopo huzingatia uhitaji wa wanafunzi na kipaumbele hutolewa kwa waombaji yatima, wenye ulemavu, waliofadhiliwa katika elimu ya sekondari na wanaotoka katika kaya masikini ambao wameomba mkopo kwa usahihi na kupata udahili;

Viwango vya jumla (lumpsum allocations) vya mikopo kwa wanufaika huzingatia uhitaji wa mwombaji na mahitaji ya kozi ya mnufaika mmoja mmoja.

Mnufaika anaweza kupangiwa kipengele kimoja au zaidi kati ya
(i) Chakula na Malazi,
(ii) Ada ya Mafunzo,
(iii) Mafunzo kwa Vitendo,
(iv) Mahitaji Maalum ya Vitivo
(v) Vitabu na Viandikwa, na
(vi) Utafiti.

Hivyo, mnufaika hupangiwa vipengele kulingana na uhitaji wake na ambavyo vimo katika kozi aliyodahiliwa;
Kuhusu malipo ya fedha za chakula na malazi (Meals and Accommodation), kwa sasa, kila mnufaika hulipwa ni TZS 8,500 kwa siku na hulipwa kwa mikupuo minne kwa mwaka wa masomo na kwa wastani kwa kila mkupuo ni TZS 510,000;

Kuhusu idadi ya wanufaika wa mwaka wa kwanza, mpaka sasa jumla ya wanufaika wapya wapatao 45,095 wamepangiwa mikopo katika awamu mbili na awamu ya tatu inayotarajiwa kutolewa Oktoba 25, 2021 itakuwa na wanufaika wapya wasiopungua 12,000;
Aidha, kwa wanafunzi ambao hawajaridhika na kiwango walichopangiwa sasa, dirisha la rufaa litafunguliwa mwanzoni mwa mwezi Novemba, 2021. Dirisha hili ni fursa kwa wanafunzi kuwasilisha maombi ya kuongezewa viwango vya mikopo.

Hitimisho
Tunatoa wito kwa wanafunzi-wanufaika wa mikopo kuendelea kufuatilia taarifa za mikopo kupitia akaunti zao mahususi zinazojulikana kama SIPA. Aidha, kwa wanafunzi waliopo vyuoni, wawasiliane na Maafisa Mikopo ili kufahamu ratiba za maafisa wa HESLB watakaofika vyuoni kukutana na wanafunzi na kufafanua masuala mbalimbali yanayohusu mikopo.

Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru,
MKURUGENZI MTENDAJI,
Oktoba 24, 2021
DAR ES SALAAM
 
Zee Korofi

Senior Member
Oct 5, 2021
160
250
Hii mikopo si ya kukimbilia ni kitanzi Cha baadae nikikumbuka retention fee ilivokuwa inafanya Deni haliishi na sio kama Rais kuingilia kati ilikuwa kilio na kusaga meno, mdogo wangu nilimshauri asiombe mkopo na shule inaendelea hapo baadae hatakuja kuteseka
Hongera mno kwa kumuambia ukweli, so now hakuna retention fee?
 
Elisha Sarikiel

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
851
1,000
heslb-login.png

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza leo (Ijumaa, Oktoba 22, 2021) orodha ya awamu ya pili yenye wanafunzi 7,364 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 19.4 Bilioni kwa mwaka wa masomo 2021/2022 unaotarajiwa kuanzia wiki ijayo.​

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru amesema kuwa orodha hiyo iliyotolewa leo inafanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza kufikia 45,095 waliopangiwa mikopo yenye kiasi cha thamani ya TZS 119.3 Bilioni.

Badru ameongeza kuwa HESLB tayari imeanza kupeleka fedha za wanafunzi hao waliopangiwa mikopo awamu ya pili katika vyuo mbalimbali na kuwataka wanafunzi kupata taarifa za kina katika akaunti walizotumia kuomba mkopo maarufu kama SIPA (Student’s Individual Permanent Account) na kujiandaa kwenda vyuoni kwa ajili ya kujisajili. “Serikali imeshatupatia fedha na tumeanza kuzipeleka vyuoni … lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi wanaopangiwa wanazikuta fedha vyuoni ambako watajisajili na kupokea ili watimize ndoto zao,” amesema Badru.

Tarehe ya kutolewa Orodha ya Awamu ya Tatu
Kuhusu kutangazwa kwa orodha ya Awamu ya Tatu, Badru amesema orodha ya wanafunzi waliopangiwa mikopo itatolewa Jumatatu, Oktoba 25, 2021 baada ya kukamilisha uchambuzi wa maombi unaoendelea na kuwataka waombaji mikopo kutembelea akaunti zao ya SIPA kupata taarifa kuhusu maombi yao.

“Orodha hii ya pili inajumuisha wanafunzi wenye sifa zikiwemo kuwa wahitaji, wameomba kwa usahihi na wamekamilisha taratibu za udahili wa chuo kimoja … tunakamilisha uchambuzi wa maombi mengine na tutaoa orodha ya tatu katika siku tatu zijazo, yaani Jumatatu Oktoba 25, 2021,” amesema Badru.

TZS 570 Bilioni zimetengwa kwa mikopo ya elimu ya juu 2021/2022
Kwa mujibu wa Badru, Serikali imetenga TZS 570 Bilioni kwa ajili ya mikopoya jumla ya wanafunzi 160,000. Kati yao, wanafunzi 70,000 watakuwa ni wanufaika wapya na wanafunzi zaidi ya 90,000 ni wale wanaoendelea na masomo baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka.

Fedha zimeanza kutumwa vyuoni
Wakati huohuo, Badru amesema HESLB imeshapokea fedha kwa ajili ya malipo ya wanafunzi na taratibu za malipo zimekamilika na fedha za wanafunzi zinatarajia kufika vyuoni kuanzia leo, Ijumaa Oktoba 22, 2021.

Wito
Aidha, Badru alisema HESLB inawasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa kwa awamu inayofuata ukiendelea.

Mwisho.
Imetolewa na:
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
DAR ES SALAAM
Ijumaa, Oktoba 22, 2021

HESLB YATANGAZA ORODHA YA NNE YENYE WABUFAIKA 5,003​

Wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 11.6 bilioni

Wanufaika mwaka wa kwanza sasa wafikia 65,359
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Ijumaa, Oktoba 29, 2021) imetangaza Orodha ya Nne yenye wanafunzi wapya 5,003 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 11.6 bilioni.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amewaeleza wanahabari jijini Dar es salaam kuwa baada ya kutangazwa kwa orodha hiyo, jumla ya wanufaika wa mwaka wa kwanza sasa imefikia 65,359 ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 168.9 bilioni.

“Orodha hii ya nne ina wanufaika 5,003 ambao muda wowote kuanzia sasa wanaweza kuingia katika akaunti zao za SIPA walizoombea mkopo na kupata taarifa zaidi,” amesema Badru katika mkutano na wanahabari uliofanyika katika ofisi za HESLB jijini Dar es salaam.

Akifafanua zaidi kuhusu wanufaika hao 65,359, Badru amesema wanufaika 1,133 ni yatima waliofiwa wazazi wawili; 9,450 waliofiwa na mzazi mmoja; 198 ni wanafunzi wenye ulemavu; 2,919 walifadhiliwa na taasisi mbalimbali katika masomo yao ya sekondari; na 51,559 wanatoka katika kaya masikini.

“Kwa takwimu hizi, mtaona kuwa ile dhamira ya Serikali kuwawezesha vijana kutoka kaya masikini inathibitika,” amesema Badru na kuongeza kuwa asilimia 41 ya wanufaika 65,359 ni wanawake na asilimia 59 ni wanaume.

Mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo

Wakati huohuo, Badru amesema kuwa HESLB inakamilisha malipo ya wanafunzi 74,440 ambao ni wanufaika wanaoendelea na masomo baada ya kupokea matokeo yao ya mitihani yanayothibitisha kuwa wamefaulu kuendelea na masomo.

“Tuna wanufaika zaidi ya 98,000 wanaoendelea na masomo na hadi leo (Ijumaa, Oktoba 29, 2021) tumeshapokea matokeo ya mitihani ya wanafunzi 74,440 waliofaulu na tutaanza kutuma fedha kesho,” amesema Badru na kuvikumbusha vyuo kuwasilisha matokeo ya wanufaika waliobaki.

Dirisha la Rufaa

Kuhusu hatua inayofuata, Badru amesema dirisha la rufaa litafunguliwa Novemba 6, 2021 ili kuwapa fursa wanafunzi ambao hawajaridhika na viwango vya mikopo vya sasa kuwasilisha maombi ya kuongezewa.

Wanaoendelea na masomo na wameomba mkopo kwa 2021/2022

“Tumekua tukipokea maswali kuhusu wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao wameomba mkopo mwaka huu … tunakamilisha orodha yao na tutaitoa siku chache zijazo baada ya kujiridhisha na uhitaji wao na kuthibitisha kuwa wamefaulu mitihani yao na matokeo yao yamewasilishwa kwetu,” amefafanua Badru.

Elimu kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza

Katika hatua nyingine, Badru amesema maafisa wa HESLB wanaendelea na mikutano na wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopo vyuoni ili kuwaelimisha kuhusu taratibu za malipo na kufafanua masuala mbalimbali yanayojitokeza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom