Nashauri polisi wa Tanzania (especially Traffic) wafungiwe BodyCams

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,047
21,522
Salam wakuu,

Strait to the point, Leo nilikua natoka Chamwino Ikulu naelekea chalinze nyama, kuna sehemu kuna kibao Cha 50, japo nlikua nipo race nilipofika sehemu hiyo nikaanza kuendesha kwa Kama 30kph hivi. Ghafla nashangaa mbele nasimamishwa then jamaa Kama wanne wakaja wamenizunguka.

Wakaomba DL yangu nikawapatia, wakauliza kadi ya gari nikawapa, wakagua insurance iko Safi. Wameona everything is okay wakaanza kunisingizia I was speeding wakataka kuniandikia tiketi.

Nikabishana nao kama dakika 5 Ila mmoja wao akawa anasema bro jiongeze usichelewe uendako. Nikaona sio kesi nikawa nafungua glove compartment niwaachie hata buku 5 ya maji, Kuna mwenzao aliona kitu Fulani kilichoni+identify kama msela hivi, akarudi nyuma kisha akawaita wale wenzake wakaanza kunong'onezana then yule senior wao akaja akaanza kuapologise kwa samahani nyingi nikamwambia wasijali wakaniruhusu nikasepa. What I'm tryna say is:

Kama nchi za wenzetu zilizoendelea, Hawa Askari wa barabarani wakifungwa BodyCams itasaidia sana kupunguza mistreatment na kuziba mianya ya rushwa. Mfungo mwema, Ijumaa Kareem.
 
Ni wazo jema sana mkuu na nalunga mkono hoja, ingawa najua litapingwa vita na askari wenyewe na kuna asilimia kubwa likapuuzwa na Serikali sikivu, maana malalamiko ya askari wa barabarani na jeshi zima la askari kwa ujumla ni mengi mno na hayajaanza jana wala leo, na mapendekezo ya kurekebisha pia ni mengi sana lakini hayafanyiwi kazi.

Askari wa barabarani wamekuwa tatizo sana, wana faini za kubambikia pamoja na usumbufu tu kwa madereva barabarani. Pia hivi vimashine vya POS vimewapa kiburi na mwanya mkubwa wa RUSHWA sababu dereva unakuwa huna namna, ukubali au ukatae kosa yeye akiamua anaandika tu faini, utajua wewe kama ulipe au usilipe iendelee kusoma na riba.

Yaani bora yarudi yale makaratasi ya NOTIFICATION kama mtu unaona hujatendewa haki, mfike mahakamani kupata HAKI uendelee na safari yako. Na kesi za barabarani hazichukui hata saa 1 inakuwa imeisha, kuliko ujinga uliopo sasa. Hii ya kuwa na Camera za mwili itakuwa VYEMA sana. Wamezidi unyang'anyi hawa watu.
 
Yaani Tz matatizo ni mengi saana!! Kuna siku kanisimamisha mmoja , kakagua kila kitu kiko sawasawa, akaja dirishani anasema chemsha kichwa bwana mkubwa, nikamwambia unasemajee?? Akaanza kujichekesha!! Akanambia nenda tuu ndugu yangu!! Nikasikitika saana, nikajisemea hii ni nchi yangu siwezi kuhama!!! Labda viongozi wa dini mkazane kuelimisha watu tupunguze uovu!!!
 
Awamu ya 5 imetokomeza rushwaaaaaaa.-MATAGA

Kumbe tuko ya 6
 
Mzee vizur sana kwa wazo hili,,ila sehemu moja umesema mmoja wao aliona kitu fulani hivi kilichoku identify alaf ndo akaanza kunong'onezana na wenzake kisha waka apologize ni kitu gani iko?au walihisi umewarekodi kwa hidden camera hahahaha
 
Kwa biden kuna magari ya askari ndio yana camera na kuna state zingine polisi ndio wana izo bodycam nimegundua hili kupitia movies

Sasa kama watavaa hawa polis wa tz na kuto ziwasha au kuziharibu makusudi tuachane nao, cha msingi kila gari iwe na dashcam inayo rekodi ndani na nje am sure akija akiona tu vile hawezi ongea ujinga atafanya kazi yake na kuondoka.

Pia naomba mwenyr uelewa, mm najua kuwa ukisimamishwa na askari hautakiwi kushuka wewe unatulia hadi aje mwenyewe, na mazungumzo yafanyike ukiwa umekaa pale,maana wanatabia anasimamisha gari alafu anakusuburia utoke nje, kuna ndugu yangu nilikua kwenyr gari yake tilivyo simamishwa akasema "nampa dakika hasipokuja nasepa"

Nashauri sheria na haki za dereva zitangazwe sana kama matangazo ya vitambaa vya kike, ASKARI wakijua wananchi wanajua jambo flani wazi wazi itasaidia naona.
 
Salam wakuu,

Strait to the point, Leo nilikua natoka Chamwino Ikulu naelekea chalinze nyama, kuna sehemu kuna kibao Cha 50, japo nlikua nipo race nilipofika sehemu hiyo nikaanza kuendesha kwa Kama 30kph hivi. Ghafla nashangaa mbele nasimamishwa then jamaa Kama wanne wakaja wamenizunguka.

Wakaomba DL yangu nikawapatia, wakauliza kadi ya gari nikawapa, wakagua insurance iko Safi. Wameona everything is okay wakaanza kunisingizia I was speeding wakataka kuniandikia tiketi.

Nikabishana nao kama dakika 5 Ila mmoja wao akawa anasema bro jiongeze usichelewe uendako. Nikaona sio kesi nikawa nafungua glove compartment niwaachie hata buku 5 ya maji, Kuna mwenzao aliona kitu Fulani kilichoni+identify kama msela hivi, akarudi nyuma kisha akawaita wale wenzake wakaanza kunong'onezana then yule senior wao akaja akaanza kuapologise kwa samahani nyingi nikamwambia wasijali wakaniruhusu nikasepa. What I'm tryna say is:

Kama nchi za wenzetu zilizoendelea, Hawa Askari wa barabarani wakifungwa BodyCams itasaidia sana kupunguza mistreatment na kuziba mianya ya rushwa. Mfungo mwema, Ijumaa Kareem.
Mama SSH anasikio zuri kwenye haki!Traffic police (wengi wao) wanaharibu sura nzuri ya jeshi la polisi!Wanatia aibu jinsi wasivyo weledi.Rushwa iko waziwazi! Tumwombe mama afute ile rushwa ya kusafisha viatu vyao!
 
Back
Top Bottom