Nashauri Mrisho Gambo agombee ubunge 2020 Arusha mjini

Aisee itakuwa poa sana. Maana hicho kipigo atakachopata hata kile cha Batilda ni cha mtoto
 
Naelewa kwamba ccm imeanza kampeni mapema,karata wanazo changa waombe mungu zikubali,maana zikikataa watalia kilio cha mbwa,mdomo juu
 
Wewe unaipenda chadema huku unaipenda ccm mbona hueleweki mkuu??? Embu jifunze kuwa na msimamo kwanza

Isije ikawa wew ni Mamluki umetumwa kukihujumu chama...Maana hamnaga urafiki kati ya Simba mwenye njaa na Swala aliyenona
 
Kwa taarifa yako,sio kila anae cheka na wewe anakupenda.Wanafunika kombe mwana haramu apite.KWA JINSI NIMJUAVYO LEMA,neno moja tuu,arusha yoote ya kwake
Alivogoma kula hakuna mtu aliyesumbuka kama zamani.. Walichukulia poa Tu. Zamani Lema akiguswa tu kidogo Arusha Inaamka ila kwasasa mmmmmmh!
 
Hongera sana ila kumbuka ARUSHA MJINI haitorudi CCM mpaka mwisho wa dunia.
Ninavyoijua Arusha hata aende agombee magu mwenyewe hatopata kura labda za mezani wale watu wa Arusha sio wa kudanganywa aisee ! Watakulia hela zako na watakutema tu kwenye sanduku la kura pale ni upinzani hadi watoto wadogo ! Kama ni kweli Gambo atagombea basi atajidhalilisha bure !
 
Wewe unaipenda chadema huku unaipenda ccm mbona hueleweki mkuu??? Embu jifunze kuwa na msimamo kwanza

Isije ikawa wew ni Mamluki umetumwa kukihujumu chama...Maana hamnaga urafiki kati ya Simba mwenye njaa na Swala aliyenona
Sijawahi ipenda CCM. Ninasema haya Kwa mapenzi mema kabisa. Mbunge na Madiwani wa Arusha wawe makini. Mh Gambo ni mtu makini na anayejua siasa za kizazi hiki ambacho wagombea wengi wa CCM walikosa Pindi wanapokabiliana na Lema. Gambo anaweza kuwa Lema Mpya Arusha anayetokea upande wa CCM
 
Naelewa kwamba ccm imeanza kampeni mapema,karata wanazo changa waombe mungu zikubali,maana zikikataa watalia kilio cha mbwa,mdomo juu
Kazi kubwa aliyokabidhiwa Mrisho Gambo kuichukua Arusha Mjini. Na kasi anayoenda nayo si ya kubeza
 
Amuulize Davis Mosha jinsi alivyopigwa kichapo kibaya Moshi
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Kuna Mtu aliyeamini Ezekia Wenje atakosa Ubunge huko mwanza?
 
Mimi ninachojua ni kwamba kiongozi yeyote anayejua kero za wananchi na akajaribu kutatua kwa kuwashirikisha ipasavyo na wakatambua kweli mtu huyu yupo kwa ajili yao atakuwa kiongozi wa watu hao kwa muda mrefu lakini ukaweka kisogo interest zao na mtu mwingine akaja kuzifanyia kazi huyo ndiye watakaye kuwa na imani naye. Kwa mawazo yangu mimi yeye anatimiza wajibu wake kama kiongozi katika mkoa huo kwa sababu serikali hii lengo lake ni kutatua kero za watu na kuleta maendeleo. Uongozi thabiti ni ule wenye malengo ya kutatua kero za wananchi wake. Watu watapima kwa kuwatumikia
 
Chugga tangu lini wameipenda ccm zaidi ya pale mtaa wa Pangani ??? Hivi unadhani mrisho gambo ana ubavu wa kupambana na Lema Godbless??
 
Chugga tangu lini wameipenda ccm zaidi ya pale mtaa wa Pangani ??? Hivi unadhani mrisho gambo ana ubavu wa kupambana na Lema Godbless??
Ana uwezo huo sana. Anajiamini sana kama Lema alivo. Wakisimamishwa Kwenye Debate Lema anaweza kosa points.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…