Nashauri Mrisho Gambo agombee ubunge 2020 Arusha mjini

Ethos

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2015
Posts
2,294
Reaction score
2,090
Mimi ni mpenzi wa CHADEMA kwa muda mrefu sasa hapa mkoani Arusha lakini kasi ya huyu kijana Mh. Mrisho Gambo ni kubwa sana na mbunge wetu Lema asipogutuka mapema atakuta mwenzake yupo mbali sana.

Tangu awe Mkuu wa Mkoa amefanya vitu vingi na sensitive sana.

Kukutana na walimu wote, kukutana na waandishi wa habari, kujadili kuhusu utalii na changamoto zake mkoani Arusha, suluhisho la mgogoro wa murieti na ujenzi wa Kituo cha Polisi Kwa Morombo ni baadhi ya mambo machache tu na yanayotia hamasa na kazidi kumjengea umaarufu na imani kwa wana arusha wote.

Yule Mh. Lema ninayemjua sijui yuko wapi kwa sasa. Juzi tu Mh. Gambo kaagiza pesa zilizookolewa kutokana na madiwani kujizidishia zitumiwe kulipia madeni ya walimu. Kama ni hivi CHADEMA itasalimika kweli?

Mrisho Gambo gombea ubunge 2020 ili wapinzani wa jifunze na kurudisha ule ushindani uliopotea kwa muda mrefu.

Arusha tunataka maendeleo sio vurugu tena.

Wasalaam,
 
Ukubali na yale matusi aliyomtukana yule Mwanasheria Korogwe .
 
Mimi ndie ninaekuambia sasa. ARUSHA MJINI haitorudi CCM. Ukombozi wa watu wa Arusha ulianza miaka mingi sana,kabla ya uhuru wa Tanganyika na sehemu tuliofikia ni kubwa sana.
Ukombozi kama ni wa kisiasa haubaki hivo hivo kama hamna juhudi za kuulea
 
Mi mwenyewe nina mpango wa kugombea ubunge jimbo la Arusha mjini, kinachonisumbua sina kadi ya CHADEMA mana fahari ya watu wa Arusha ni CHADEMA
Hapana sio Kwa zama Hizi... Naiona CCM ikirudi Kwenye mstari
 
Mimi ni mpenzi wa CHADEMA kwa muda mrefu sasa hapa mkoani Arusha lakini kasi ya huyu kijana Mh. Mrisho Gambo ni kubwa sana na mbunge wetu Lema asipogutuka mapema atakuta mwenzake yupo mbali sana.

Tangu awe Mkuu wa Mkoa amefanya vitu vingi na sensitive sana.

Kukutana na walimu wote, kukutana na waandishi wa habari, kujadili kuhusu utalii na changamoto zake mkoani Arusha, suluhisho la mgogoro wa murieti na ujenzi wa Kituo cha Polisi Kwa Morombo ni baadhi ya mambo machache tu na yanayotia hamasa na kazidi kumjengea umaarufu na imani kwa wana arusha wote.

Yule Mh. Lema ninayemjua sijui yuko wapi kwa sasa. Juzi tu Mh. Gambo kaagiza pesa zilizookolewa kutokana na madiwani kujizidishia zitumiwe kulipia madeni ya walimu. Kama ni hivi CHADEMA itasalimika kweli?

Mrisho Gambo gombea ubunge 2020 ili wapinzani wa jifunze na kurudisha ule ushindani uliopotea kwa muda mrefu.

Arusha tunataka maendeleo sio vurugu tena.

Wasalaam,
Ni ndoto zako tu, utaamka muda si mrefu.
 
Siasa ni kuwatumikia watu na kuwasaidia wananchi kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. Kama kweli Mrisho Gambo ana malengo ya kugombea ubunge 2020 aendeleze juhudi za kuwatumikia wananchi bega kwa bega lolote linawezekana kwani ni kijana na uwezo wa kuthubutu anao
 
Back
Top Bottom