Mpunilevel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2015
- 3,140
- 1,871
Jana wafuasi wenu wametwangana sana na kuumizana vibaya sana. Luckly hakuna mtu aliepoteza Maisha.
Huu si utamaduni wetu watanzania hata kidogo.
Haya tulizoea kuyaona nchi za ng'ambo. Lakini yameanza kuzoeleka hapa nchini.
Si Jambo la kupuuzwa hata kidogo na wapenda Amani.
Wakati Maalim Sef na Lipumba mkitunishiana misuri, wahanga wa timbwili lenu ni wafuasi wa chini kabisa. Ambao ndio hudhurika.
Familia zenu zikibaki salama kabisa.
Walio nyuma yenu kama washauri wenu hawafai kabisa hata kidogo.
Lengo lao ni kuona Cuf inasambaratika kabisa. Hii ndio itakua furaha yao.
Duniani siku zote mazungumzo mezani ndio hutatua matatizo yanayoikabili jamii yoyote, na si nguvu.
Maalim Sef na Professor Lipumba ni kitu gani ambacho kimewafanya hata kufikia hatua hii?, kumbukeni mlipotoka.
Naamini kama kujikwaa, wote mmejikwaa kwa namna moja ama nyingine.
Leo sitaweza zungumzia wapi mlijikwaa. Ila ni kweli kuna sehemu mlijikwaa na ni kawaida kwa binadamu yoyote yule, kwani hatujakamilika.
Naamini elimu na mafundisho ya dini ya kiislam mnayo.
Kiukweli dini ya kiislam katika mafundisho yake, inahimiza kuvumiliana na kusameheana kama mmekoseana.
Je? Mafundisho ya mtume Muhammad s.a.w ndio hayo mnayofanyiana?
Nawaombeni mkubali nyote kukaa mezani na kuondoa tofauti zenu, haijarishi mmekwazana kiasi gani.
Nyie ni kioo cha jamii, wengi wanawaangalia, msiwe mfano mbaya kwa jamii.
Namalizia kwa kuwaasa kukaa mezani na kuondoa tofauti zenu kwa mstakabali mwema wa CUF.
Neno ningelijua huja baadae.
Msitake maneno haya yaje myoyoni mwenu baadae.
Kila la Keri nyote