Ile CUF ya Lipumba na CUF ya Maalim inajirudia kwa CHADEMA ya Mbowe na CHADEMA ya Halima

fake ID

JF-Expert Member
May 19, 2014
391
1,000
Nakumbuka ilianza mzaha mzaha kama hivi. Huku wanafukuzwa, kule msajili anawatambua.

Mwisho mgawanyo ukatokea na sote tuliona kilichotokea watu wakagawana fito na CUF ikabaki hii ilivyo! Sisemi CHADEMA nayo itakuwa kama CUF ila naona hii trailer inavyoanza ni kama movie ile Ile.

Kipindi kile alitumika "msajili" kumtambua Sakaya na Lipumba na pesa zote za ruzuku, huku Maalim akisema hatambui chochote. Safari hii wamevuliwa uanachama "Spika" anasema atawalinda tena ikibidi "badamu patamwagika"

Hotuba ya Halima haina tofauti na ile ya Sakaya. Next ameshasema yeye ni CHADEMA kindaki ndaki. Kama vile Lipumba na maalim kila mmoja akidai CUF ni yake! Sasa Kuna vitu viwili vya kutilia mashaka.

1. Panya anapomkebehi paka hadharani na
2. Paka anapomsifia panya hadharani

Ngoja tuone
 

Ryaro wa Ryaro1233

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
353
1,000
Hii yote ni Kazi ya CCM, Kwani inajua Kuzichanga Karata vizuri, kwa vile wapinzani wana Njaa. Lakini Safari hii Walikuwa waende na Maji, wana kila sababu ya Kuvishukru Vyombo vya ulinzi na Tume ya uchaguzi ambayo ni tawi la CCM. Sababu ya kuwarubuni hao 19 ni hili tu wapete zile trillion za wanaowahita Mabeberu.

Basi Wapinzani Wakomae na Watoa Pesa na ukweli uwekwe wazi, maana hiyo hera hata faida yake itakuwa zaidi kwa CCM. Halafu EURO 21M za EU, ZILIENDA wapi isije ndo Ziligharimia Mabango na T-shirt za CCM wakati wa Usanii wa tarehe 28, October, 2020.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,706
2,000
Usimringanishe Mh. Mbowe na hizo COVID-19....

Zilishafujuzwa na chapter closed...wao waendelee kula pesa za ubunge wa kupewa na Ndugai who cares..
 

Lumwago

Senior Member
Aug 20, 2020
119
250
Ntakuwa wa mwisho kuamini kua Hawa wa mama wanaweza kuuwa cdm. Cdm Ni mpango wa mola. Hawa Ni njaa tu wanahoma ya kufikiri wataishi vp bila ubunge. Wanaogopa maisha nje ya ubunge.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom