Uchaguzi 2020 Kwenye Issue ya Membe, Maalim Seif umeover react na hii siyo sawa

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Kwanza niseme waziwazi kuwa mimi namuunga mkono Tundu Antipas Lissu kuwa ndiye mgombea ninayeamini anaweza kumng'oa John Joseph Magufuli na ndiye nitakayempigia kura.

Lakini pamoja na hayo lazima nikiri kuwa chama kinachonivutia nchini kwa sera, kuzungumza masuala ya wananchi kwa hoja mathubuti, kwa utafiti wa kisomi, mipango mkakati na ilani ni ACT Wazalendo

Lakini pamoja na hayo nimeshtushwa sana na kauli ya mwenyekiti wa ACT ndugu Maalim Seif aliyoitoa dhidi ya Ndugu Benard Cammilius Membe, binafsi naiona kama ni kauli ambayo kama ilibidi kutolewa basi ingetolewa kwa namna na style nyingine tofauti na aliyotumia maalim Seif.

1. Ndugu Maalim, Bernad Membe ni mkubwa mwenzio anastahili staha na heshima mbele ya Umma
Kwa hadhi, umri na utumishi uliotukuka wa mh Membe kwa nchi hii siyo sawa na siyo sahihi hata kidogo kwenda kuongea kwa style uliyotumia pale mbele ya vyombo vya habari. Siyo sawa kumkaripia mheshimiwa Membe kama mtoto mdogo. Mimi kama mwananchi ninayependa ustawi wa Demokrasia nchini, sidhani kama ni sahihi viongozi, tena viongozi wakubwa kuitisha press conference na kuanza kushambuliana katika vyombo vya habari.

ACT ina vikao, kama Membe alikosea ilikuwa ni jukumu lako kumuita na kuongea naye ili kuelewa kiundani hasa alikuwa anamaanisha nini, na hata kama alikosea hilo suala halimalizwi kwenye press conference bali ndani ya vikao vya chama na kama ikibidi ndo mnatoa press release juu ya maamuzi ya vikao vya chama, siyo mwenyekiti anaitisha vikao kwenda "kumsuta" mgombea wake mwenyewe. Hii nidhamu ya wapi, au nidhamu ni kwa wadogo tu?

2. Kiongozi wa Chama alimhakikishia Ndugu Membe heshima
Wakati akihojiwa na chombo kimoja cha nje, Kipindi cha ujio wa Membe hapo ACT, Kiongozi mkuu wa Chama alimhakikishia ndugu Membe heshima, na akasema pengine kilichowaondoa akina Lowasa Chadema ni kujihisi hawaheshimiwi vya kutosha. Sasa haijapita miezi minne tangu mheshimiwa Membe aingie ACT mnaanza kumkoromea Mgombea urais wenu wenyewe, mliompitisha kwenye vikao halali, mkaturushia sisi wananchi Live kwenye TV, kwa mbwembwe kubwa, mkaenda kumtambulisha unguja na Pemba halafu mnakuja kumrebuke hadharani na kumchallenge eti afanye kampeni tuone, Yaani mnaanza kumdhihaki badala ya kutafuta naye suluhu juu ya suala hilo ambalo yeye na ACT wamewekeza mtaji mkubwa kabisa. Au mnadhani ACT ni nyie wawili Zitto na Maalim peke yenu na kwamba siye wananchi hatuna stake katika maamuzi ya chama kwa ujumla wake?

3. Kuna maisha baada ya Uchaguzi
ACT inatakiwa ikitoka katika uchaguzi huu iwe moja, iwe na nguvu kubwa zaidi ya kuendeleza mapambano ya kupanua demokrasia nchini na kujijenga zaidi. Sasa mtajijengaje wakati mmeraruana humu ndani kwa ndani kisa tu mmeona mgombea wenu uchaguzi umemkalia vibaya na badala ya kukaa kama chama mje na stratergy ya pamoja ya kuwaeleza wananchi msimamo halisi wa chama baada ya kukaa kikao tena na tena bila kuchoka na mgombea, nyie mnaanza kumuattack. Nyie ACT Wazalendo hebu tuelezeni, ni lini na ni wapi kamati kuu ya Chama ilikaa na mgombea na mkasema kuwa sasa Wewe Membe siyo Mgombea tena kwa tiketi ya ACT bali sasa mgombea wetu ni Lissu?. Haiwezekani utashi wa Zitto na Maalim peke yenu kwa sababu ya maslahi yenu binafsi ya kisiasa ya leo na ya kesho mkaamua tu kuwa hatukuungi mkono bali tunamuunga mkono yule. Kama mlitaka hivyo nyinyi sasa mlimpitisha awe gombea kwa sababu gani, kwani mlilazimishwa kuweka mgombea?

4. ACT mlimpitisha Membe kihalali msijifanye hamumjui
Mkutano mkuu mliufanya, mkaturushia Live kwenye TV, mkaserebuka sana, mkatwambia kuwa Membe ndiye mwenyewe, baada ya hapo mkazindua na Ilani yenu, mkamkabidhi Membe sasa hamuwezi kuja hivi kwetu sisi wananchi kienyejienyeji eti hamumjui kuwa ni mgombea halali wa ACT. Sasa kama Maalim anaweza kumruka Kimanga mgombea wake yeye mwenyewe aliyempitisha huku akiwa ni mwenyekiti wa Kikao atashindwaje kuwakana Wazanzibar wakishampigia kura na kuwa raisi?. Hivi vitu nyie ACT msidhani ni vidogo, ni vikubwa sana kwetu wananchi maana tunapima uwezo wenu wa kuendesha mambo yenu wenyewe!

5. Maalim kuna Profesa Omar ambaye ni mgombea mwenza wa Membe, naye ni mgombea halali vipi amekubali naye kuunga mkono mgombea wa chama kingine?
Hii ishu siyo ya Membe peke yake maana kuna mgombea mwenza wake, naye ni mgombea halali, ana jasho lake kwenye jambo hili na anataka aje awe makamu wa raisi. Kama unadhani ulishamalizana na Membe je chama kilipata ridhaa ya mgombea mwenza?, au maalim unadhani kuwa kwa kuwa profesa Omar ni mzanzibari basi unammudu tu na mambo yatajesha yenyewe, kwamba atakaa kimya kwa sababu "Simba" kaunguruma. Haya mambo siyo rahisi kihivyo Maalim. Tunataka chama cha ACT kiheshimu kanuni, taratibu na vikao vyake chenyewe, ili tupate vyama makini, vitakavyojenga demokrasia ya kweli nchini!

6. Hakukuwa na ulazima kwenye kipindi hiki cha lala salama kuonyesha udhaifu ndani ya chama
Kama ilitakiwa kuwapa signal wananchi kiujumla na wafuasi wa Membe wamchague Lissu ilitakiwa kutumia lugha nzuri ya kisiasa ili kuwafanya watu wafanye hivyo. Kitendo cha kuja mbele wiki moja kabla ya uchaguzi na kuonyesha kuwa kuna mgogoro ndani ya chama kunawatisha wananchi, kunawakumbusha mambo ya Dr Slaa na Lipumba kuanzisha zogo siku chache kabla ya uchaguzi. kuna siku Zitto aliulizwa juu ya harakati za kampeni za Membe, Jibu akajibu kuwa yuko busy anaandaa baraza la mawaziri, hiyo kauli ilikuwa ni ya kisiasa na ilikuwa ni jibu zuri la kuondoa kiwingu cha maswali ambayo yangefuata ambayo yasingekuwa mazuri kwa kambi ya upinzani.

Sasa Maalim ulishindwaje kutumia sense of humor, au positive propaganda kupangua damage yoyote unayodhani ilileymtwa na press conference ya Membe?. Maalim kwa nini hakukubaliana na baadhi ya mambo mazuri kabisa kwenye hiyo press conference ili kuonyesha balance, Kiukweli kuna mambo nyeti na mazuri pia ambayo Membe aliongea siku hiyo!

7. Ombi kwa mheshimiwa Membe
Mzee wangu Membe, nakuomba umuunge mkono Lissu, ikiwezekana usitumie mafumbo sana, tumia njia unayodhani inafaa ili ueleweke na uwe safe kisheria, naamini unamuunga mkono Lissu kwa namna moja au nyingine ndiyo maana ukajitolea kumpa nafasi afanye kampeni bila wewe kutofanya ili usimharibie. Ila kwa bahati mbaya wenzio hawajakuelewa, naomba uwaeleweshe kuwa ni nini hasa makusudio yako. Mimi naamini ukiusaidia upinzani kustawi itauwa rahisi kuipasua CCM kwa sababu usipoaminika wewe leo, wana CCM makini wataogopa kuikimbia CCM, na kwa bahati mbaya akina Zitto hawalioni hili.

Tunajua una wafuasi wengi nchini, wakiwemo wananchi wa kusini hasa Lindi, hawa wote Lissu anahitaji kura zao, nakuomba uwaombe kwa namna yoyote utakayoweza wampe kura Lissu ili tuuondoe utawala dhalimu wa CCM. Mwisho nakuomba uwasamehe akina maalim hawajakuelewa bado, hawajaelewa sense yako of humor, hawajaelewa kuwa unataka kucheza hii gemu kusaidia upinzani lakini bila kuingia matatani kwenye mkono wa sheria. Talk to them, i hope they will understand!
 
Mzee wa ubwabwa ni bora kuliko Membe wako mkuu!

Membe alifikiri huku field atakutana na makelele kama ya mitandaoni pia!

Membe kasema kutangaza kwamba una muunga mkono flani wakati wewe mwenyewe unagombea nafasi hiyo hiyo unapaswa kupelekwa mirembe. Membe hataki kwenda mirembe.
 
Kwenye karatasi ya kupigia kura ni namba tisa,mpatia japo kura moja ya kufutia machozi.
Kwa iyo umemnawa magufuli?😂😂😂

Kweli Magufuli hana chake mwaka huu. Huu ni uthibitisho tosha kuwa Membe atapunguza kura chache atakazopata Magufuli na hana madhara yeyote kwa ushindi wa kimbunga wa Tundu Antiphas Lissu kwenye uchaguzi huu!
 
Mimi pia niliwaza hivyo mkuu, lakini nikaconclude kwamba mpaka unaona mtu anaitisha press kama vile na anatoa ya moyoni, ujue kuna mambo ndani yalishagonga mwamba..

All in all hii game ilitakiwa Membe amuunge mkono Lissu hadharani kila mmoja ajue.. Maana kuendelea kuing'ang'ania iyo nafasi ni kuzigawa kura bure tuu
 
Kwa iyo umemnawa magufuli?

Kweli Magufuli hana chake mwaka huu. Huu ni uthibitisho tosha kuwa Membe atapunguza kura chache atakazopata Magufuli na hana madhara yeyote kwa ushindi wa kimbunga wa Tundu Antiphas Lissu kwenye uchaguzi huu!

Are you serious. Lissu huyu Huyu. Anashinda kwa Kura zipi. Nakuomba urudi hapa tarehe 1.11.2020. usione Aibu.
 
Membe siyo wa kumchekea

'with us or against us'
Kwenye mabadiliko ya kweli lazima ma snitch wawepo. Hata South Africa wakati wa vuguvugu la kuondoa makaburu wapo weusi waliokuwa mapandikizi wa makaburu na wali wasnitch weusi wenzao. Membe hashangazi ila kikubwa hawezi kuzuia mabadiliko makubwa na ya kihistoria waliojiandaa kuyafanya watanzania mwaka huu!!

Tunaenda kumchagua kwa nguvu zote Tundu Antiphas Lissu hapo wiki ijayo na kumsimika kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025
 
Back
Top Bottom