Nimemuona Prof. Anna Tibaijuka kupitia youtube aklialamikia kodi ya Tshs.12m kwa ajili ya Shule yake ya Sekondari. Binafsi naungana naye ni kwa nini kuwepo na kodi ya majengo kwa Shule za binafsi ili hali Shule hizi za binafsi zinatoa elimu kwa watoto wa Watanzania bila kujali rangi, dini, kabila. Kama kuna kodi kama hiyo inabidi Serikali ifikirie upya na kuifuta mara moja kwa Shule za binafsi.