Nasema sitaki rais achague viongozi wa dini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasema sitaki rais achague viongozi wa dini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Feedback, Jul 6, 2011.

 1. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kwenye gazeti la Habarileo kuna taarifa kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu (CUF), ameitaka serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujaza nafasi za viongozi watendaji katika ngazi za dini ya Kiislamu akiwemo Mufti pamoja na Kadhi Mkuu ambazo zipo wazi kwa muda mrefu.

  Jussa amesema, viongozi hao ni muhimu zaidi kwa waumini wa dini ya Kiislamu na kutojazwa kwa nafasi hizo tangu kufariki kwao dunia, si jambo jema. Amesema, anafahamu kwamba uamuzi na uteuzi wa kujaza nafasi hizo upo kwa Rais, lakini wapo wasaidizi wake akiwemo waziri wa wizara ya Katiba na Sheria ambao wanao uwezo kumshauri kuhusu uteuzi wake.

  My comment:

  Nauliza ikiwa utaratibu wa rais kujaza nafasi za kidini upo kikatiba na kama upo unahusisha dini zote au ni dini ya kiislamu tu kama haupo kikatiba kwanini rais wa nchi ahusishwe na uteuzi wa Mufti na Kadhi Mkuu ambao ni viongozi wa dini? Nasema sitaki rais wangu aliyechaguliwa na wananchi wote bila kujali itakadi za dini ahusishwe na uchaguzi wa kiongozi yeyote wa dini. Waheshimiwa naomba kutoa hoja.
   
 2. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Zanzibar kabla ya kuwa na muungano walikuwa na taratibu zao, mila na desturi zao na dini yao ya kiisilamu, walikuwa na katiba yao na sheria zao, yote haya yalikuwa yanafanyika kbla hata ya Tanganyika kuungana na Zanzibar ndio maana hata kwenye sherehe za dini za kiisilamu kama vile sikukuu za IDDI zote kunakuwa na gwaride la Baraza la IDDI na hii ni kwa sherehe za kiisilamu tu na mgeni rasmi katika sherehe hizo anakuwa Rais.
  Sasa jua ya kwamba hio ndio katiba yao kama hupendi kavunje muungano ambao wazanzibari hawautaki na wewe unalazimaisha wala hamjalazimishwa kujiunga na zanzibar sasa unakereka nini vumilia tu japo inakuuma ndugu.
   
Loading...