[QUOTE=Gama;kumbukeni kuwa magari ya su hayanunuliwi na wizara ya ujenzi(miundombinu). Su hufanya maamuzi yao wenyewe.
SU maanake nini? Si Shirika la Umma? Ivyo jombii serikali nayo ina mkono wake,kwani mashirika ya umma yanapewa ruzuku na serikali. Kwaiyo ununuzi wa hayo ma VX/GX bado unaiumiza serikali,hata kama hayo mashirika yanafanya maamuzi yenyewe. Ingekua yanajitegemea 100% basi suala la richmond na dowans lisingepigiwa kelele na wananchi (wananchi wanapiga kelele kwa vile pesa ya serikali inatumika hovyo). Pia jombii kumbuka tunalipa kodi na malipo kupata huduma katika mashirika hayo,ivyo unapaswa kuwa na uchungu wa pesa yako,uone inatumika kwa maendeleo ya mashirika hayo,na si anasa. Ungesema DFP ningekuelewa kwani hayo yananunuliwa na pesa za miradi za WAKUBWA,kama anavyoitaga rais wenu!