Je ni CCM ,CUF au ni vibaraka ndani ya CDM wakiwemo wakuu wao kwa kuivunja kila nyota inayotishia uhai wa CCM au inayotishia wakuu wenyewe ?
Kila utakaemsikia kafukuzwa au kasimamishwa uwanachama ndani ya CDM ,sababu za undani utaziona ni kuwa ananyemelea kugombea nafasi nyeti na hivyo huwahiwa mapema asije akawaangusha wazee wa Chama.
Ukiangalia Chama kama CUF wale waliofukuzwa wote hakuna alietishia uhai wa viongozi wakuu nikimaanisha kuwaangusha katika uchaguzi ,wengi wameonekana kujiengua wenyewe haswa pale wanaposhindwa kiuchaguzi na wengine kwa maslahi yao binafsi.
Kuna akina Lwakatare huyu nae amehamia CDM yanayomkuta huko kila mmoja anayajua ,Tambwe huyu mchumia tumbo CCM wesha mtupa ,mwengine ni Shaibu Akwilombe hajulikani amepotelea wapi na wengine wengi ambao walikiacha chama cha CUF ,lakini umakini na umahiri wa CUF umeonekana ,hakukutokea mtafaruku wala chama kuyumba kama inavyoonekana kwa CDM ,CDM inakufa ila inajikaza kisabuni ,ukweli ni kuwa CDM imechafua ile sura ambayo ilikuwa wameivaa ya kuwa chama makini na chenye muelekeo wa kuongoza Nchi hii .lakini imekuwa kama iliyovamiwa na viwavi jeshi ,imesambaratika na joto la kuzidi kusambaratika linaendelea.
Aidha viongozi wakuu wa CDM wanatumika na CCM kuuwa umoja wa WaTanzania ndio ukaona hawang'atuki au wameng'ang'ania ukubwa ,sio kosa ila ung'ang'aniaji wao haukubaliki ndani ya Chama wanachodai ni cha WaTz wote
Leo CDM inakufa vibaya sana ,kifo cha ajabu japo hakuna kifo kizuri. Beggars cant be choosers walala hoi hawana haki ya kugombea nafasi za juu.:A S 103: