Tumehimizana kuhanikiza harufu ya uzalendo kwa kila mwananchi.
Mimi na Ndugu Angola tumekubaliana kuvaa bendera za nchi. Ingawa mwenzangu ananishangaza kidogo alipochagua kuziweka bendera zake.
Pia tumekubaliana kutengeneza vipeperushi na majarida ya uzalendo tutagawa bure. Bendera za nchi zitagawiwa bure na lazima uiweke nje ya nyumba yako kila alfajiri na uitoe kila jioni.
Kabla ya kuiweka na kuiondoa utaimba wimbo wa nchi, kama huuwezi urekodi kwenye simu play wakati wa hayo matukio adhimu.
Hapo lazima uzalendo uje tu.