Nasema hapana, 'majeshi' ya vyama vya siasa hapana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasema hapana, 'majeshi' ya vyama vya siasa hapana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kizotaka, Feb 29, 2012.

 1. K

  Kizotaka JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi vikundi vya vyama vinavyoiywaGuards ni vya nini, viko kwa manufaa ya nani? Kuna Yellow Guards, Green Guards,Blue Guards, White Guards na huenda kuna vingine vya siri. Vikundi hivi nihatari sana. Juzi juzi hapa tumeonyeshwa Green Guards live, vijana mtiti.

  Hata Interahamwekule Rwanda walikuwa ni jeshi la chama cha J Habyarimana, mambo yalipobadilikawalifanya mauaji yaliyotikisa dunia. Sasa hapa nyumbani majeshi haya ni yanini? Yanalinda chama na wanachama, taifa au raia wote bila kujali itikadi zakichama?

  Chuki za kisiasa zikizidi watatumika hawa. Kama waliopata mafunzo CCPwanaua watu je hawa wasio na mafunzo na wakapewa silaha si ndo itakuwa balaa!Tumeona kenya machafuko ya kisiasa, hatuko dunia nyingine sisi.

  Hivi vikundihavina maana yeyote, kama chipkizi na JKT vimetushinda tuache tulindwe naJWTZ,Polisi na Usalama basi.

  Hakuna habari ya chama kuwa na vikosi kama hivi nihatari sana. Mambo yanapobalika watatumika hawa jamani, wanamapenzi na chamakuliko taifa ni hatari. Vifutiliwe mbali.
   
Loading...