NasDaz's Daladala Users' Principle

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,135

Hii
ni principle maalumu kwa watumiaji wa daladala! Najuwa wapo watakaoibeza; lakini wapanda daladala wenzangu, don' undermind this principle! Don' do it just because umeona kuna member kafanya hivyo coz' may be yeye si mmoja wetu!!! and if u ignore it, trust me, sooner or later u'll regret!!!
The principle states that "To every unnecessary delay of even a half a minute or less, may cause a total delay of even a quarter an hour or more!"
Nini hasa maana ya hiyo kitu!!! Je, umeshawahi kufika kituo cha daladala na pale unapofika tu, mara unakuta daladala iliyokuwapo inaondoka na wewe kulazimika kusubiri daladala nyingine?!!! Baada ya daladala hiyo kuondoka, unajikuta unakaa kituoni kwa dk 15 au zaidi bila kupata daladala nyingine! Hapo unakumbuka kwamba, endapo ungefika kituoni nusu dakika tu kabla ya muda uliokuwa umefika, basi daladala iliyokuacha ungekuwa umeiwahi!!! Lakini kwavile ulichelewa kwa hiyo nusu dakika tu, unajikuta unakaa kituoni kwa zaidi ya robo saa!!!! Ukirudisha akili nyuma, unakumbuka kwamba, nusu dakika iliyokuchelewesha ni ile uliyoitumia kujiangalia mara ya tatu kwenye kioo (unnecessary delay) wakati ulishafanya hivyo kabla!! kama usingeipoteza dakika hiyo, bila shaka ungewahi kupanda daladala iliyokuacha!!!
Hii principle naitumia mara kadhaa, na kila nipakuja kuipuuza, mara nyingi najikuta ikinirudi!!!!

Likewise, hii principle inaweza ku-apply hata kama unatumia usafiri binafsi!!! Hebu assume unatoka zako Ubungo unaenda Tazara ni ki-Mark II chako! Unafika Mabibo Hostel, unakumbuka kwamba kuna mshikaji hapo unataka ukamsalimie( au ukamuoneshe kwamba nawe siku hizi una-drive?) wakati hukuwa na hiyo nia kabla (unnecessary delay)! Unaamua kuchepuka na kuingia Mabibo Hostel lakini unafika huko, uliowakusudia hawapo hivyo hapo hapo unaamua kugeuza gari (umepoteza dakika mbili tu!) Unafika Buguruni, unakuta bonge la traffic Jam iliyosababishwa na ajali ya gari iliyotokea dakika moja tu iliyopita! hapo ndipo unakumbuka kwamba, endapo usingepitia Mabibo Hostel (wakati hukuwa na sababu za msingi za kupitia), si ajabu dhahama hiyo ingeanza wakati wewe umeshavuka eneo la tukio!!!

Kama nilivyotangulia kusema hapo kabla, ukipuuza principle hii, sooner or later utakuja ku-regret na kama ukii-apply into practice, u'll always be the winner!
My take ni kwamba, tuache visingizio visivyo na maana; hatuna sababu za kuchelewa makazini kwa visingizo vya usafiri!!!!
Generally speaking, over 75% ya kuchelewa kwetu kunasababishwa na sisi wenyewe!!! Hatutaki kuishi kulingana na mazingira tuliyonayo!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom