Nasaha zangu mujarabu kwa wanandoa

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
1,486
1,861
Kuna wanandoa wengi hawaungani kindoa ili kuwa mwili mmoja, yaani umoja au ushirikiano wa kimaisha katika familia, bali huunganishwa na sifa au vitu alivyonavyo mtu.

Unaoa au kuolewa na fulani kwa kuwa ana elimu nzuri, mali nyingi, umbile zuri au cheo fulani. Mungu hakuunganishi na elimu, cheo, umbile au mali ya mtu. Unasahau kuwa utaishi na mtu, si vitu vyake!

Kwenye ndoa hatupaswi kufuata vitu alivyonavyo mtu, bali utu alionao mtu na tabia yake njema. Mungu anaunganisha upendo wa moyoni wa wawili bila kujali mali au vyeo vyao. Hivyo ni ziada tu, si kipaumbele!

Hao ndiyo ambao ndoa zao hudumu kwa kuvumiliana, kuchukuliana udhaifu na kupendana mioyoni - pawepo mali au pasina mali. Naonya: usioe au kuolewa na mali, elimu, umbile au cheo cha mtu. Oa au olewa na yeye alivyo - tabia yake njema.

Pia tukumbuke kinasemwa "anachounganisha" Mungu, si "wanachounganisha" watu wa makanisani, kimila au misikitini. Hao hawaoni mioyo ya watu bali huona sura ya nje yenye hila nyingi. Mungu huangalia yaliyoko moyoni (1 Samweli 16:7), ndiposa huunganisha hao wawili ikiwa mioyo haina hila. Ndoa nyingi Mungu hajawahi kuziunganisha!

Aidha, nirudie kusema: Mungu haunganishi vitu na watu, bali watu wenyewe na mioyo yao safi na upendo wa dhati! La sivyo talaka inakuwa inasubiri tu siku, maana ndani ya ndoa tunapaswa kuishi na mtu na utu wake, na si mtu na vitu vyake!!!
 
Nimependa ujumbe ndani ya mada mkuu ahsante, mada nzuri imebeba ujumbe muhimu sana tatizo lipo kwenye hiki kizazi chetu cha sasa adi wazazi wanachangia kwa asilimia kubwa kuyasambaratisha mapenzi yenye utu ndani yake kwa kutaka watoto wao waoe/waolewe na wenye pesa,mali au elimu bila kujali kuwa utu ni bora zaidi kuliko hivyo vyote.

Hii mada wachangiaji watakuwa wachache sana kutokana na jinsi mambo yalivyobadilika, hakuna utu now days bila kuwa na kitu.
 
Umeeleza ukweli mtupu, nakupongeza sana. Ila tusikate tamaa. Tuendelee kuueleza na kuusambaza ukweli hata kama tutabaki wachache. Mimi naamini ukisema ukweli uwe tayari hata kusimama peke yako, na Mungu atatakuwa upande wako.

Aghalabu ni heri kubaki peke yako na ukweli kuliko kujumuika na wengi kwenye mfumo wa maisha ya kisanii tu, hila na.ulaghai mwingi.

Ukweli ni lazima usemwe japo jamii imejisahau sana kwenye hili nadhani kuna mahali uzembe unafanyika sana katika malezi, usasa unaumaliza utu na tamaduni zetu
 
Back
Top Bottom