Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,440
- 38,437
Husika na somo hilo hapo juu;
Haya ni makosa ya kawaida sana kufanywa humu mitaani mwetu tunamoishi:
Usikubali mtoto wako kuitwa MCHUMBA
Hii ipo sana mitaani kwetu. Babu, bibi na baadhi ya wanajamii, huwa na tabia hii kwa wajukuu zao, kuwaita watoto kwa msamiati huu - MCHUMBA. Ubaya wa tabia hii ni kwamba, inamjengea mtoto udadidisi mtoto juu ya jambo tajwa, madhara ni kwamba jambo hili litamkaa mtoto kichwani. Athari inaweza kuwa, kuanza kulifanyia kazi mapema zaidi kuliko kawaida.
Usikubali mwanao kutumwa SIGARA
Katika mazingira yetu, tunaishi na wavutaji sigara. Baadhi ni jamaa, ndugu na marafiki zetu, tena baadhi yao ni wale tunaowaheshimu sana. Usikubali watu hawa, wawapo nyumbani kwako ama karibu na mtoto wako, kumtuma mtoto dukani kununua sigara. Tabii hii itamfanya mtoto kupata udadisi juu ya kitendo ama kitu hicho, huwezi jua, mtoto anaweza kuvutika kuja kufanya kama alivoona mgeni husika akifanya!
Usikubali: mtoto kuangalia BONGO MOVIE peke yake:
Hili liko wazi zaidi. Maudhui na hata muundo wa picha nyingi za bongo movie, bado ni utata, inatosha kusema kuna ukiukwaji mkubwa wa maadili katika tasnia hii, inahitaji ujasiri wa kijinga kuangalia movie za ndugu zetu bongo movie tukiwa na watoto wetu! Katika movie hz, mavazi, lugha, vinywaji, mandhari, n.k vinaleta mushkeli kwa wazazi kuangalia movie hizi na watoto. Kwa kuliona hili, nimeamua kuwa mpenzi wa comedy za kina Majuto nyumbani, kuliko akina Wema na wenzake, angalau watoto niwaepushe na majanga kwa njia hii!
Usikubali mwanao kutumika kama kuwadi
Kuna tabia za ajabu sana uswahilini. Hii ni moja wapo. Watu wazima kuwatuma watoto kuwaitia wapenzi wao. Mtoto mdogo anatumwa akamwite boyfriend ama girlfriend wa mtu mzima, mbaya sana hii. Usikubali hii itumike kwa mtoto wako. Inakuwa mbaya zaidi pale ambapo mtoto huyu anapewa na vijizawadi vidogo vidogo kwa kutumwa huku, hasa vihela, hivi vinamshawishi kuingia ktk mambo hayo mapema!
Angalizo: kuwa makini na vifaa vya michezo vya watoto (waepushe kuchezea bunduki bandia, visu bandia, na vinavofanana na hivo). Katika misururu ya magari humu mijini, wazazi wananunua bastola za bandia , wananunua visu vya bandia kwa ajili ya watoto wao. Sio nzuri hii. Labda kama unajua dhamira yako nyuma ya malezi haya, lakini kinyume chake ni hatari sana.
Usiende na mtoto BAR.
Tumeshazoea. Mzazi kakaa bar, grocery, na maeneo mengine sawa na hayo, meza imechafuka pombe za aina mbali mbali! Mtoto analetewa soda ama anaagiziwa chips. Kwa macho ya mtoto na akili yake, anaweka udadisi juu ya vinywaji wanavokunywa watu wazima wanaomzunguka, huku akifikiria kwa nini yeye hajaletewa vile wanavotumia watu wazima, anaweza akapata hisia kuwa umri umembana, akikua na yeye atatumia vitu vile. Hii ni shida. Hii haijakaa sawa hata kidogo.
Usikubali: mtoto hajui namba ya simu ya mama/baba yake
Ni muhimu sana mtoto hasa Yule ambae ameanza kwenda shule, kujua namba ya simu ya mama ama baba yake. Ni vizuri kumkaririsha, isiwe namba za watu wote wa nyumbani, hapana, inatosha akikariri namba ya mama na baba tu. Maisha ya shule ya watoto wetu yana changamoto nyingi sana, simu ya mama ama ya baba inaweza ikatoa msaada Fulani wakati wa dharura kwa mtoto.
Usikubali: hujui anapocheza mwanao na anacheza na akina nani:
Tabia za watoto zina mikono ya watu wengi. Watu tofauti, maeneo tofauti! Kuna mzunguko mrefu mpaka mtoto wako kuwa na tabia hizo. Zipo tabia zilizotokana na wazazi, zipo zile alizozitoa shuleni. Zipo tabia ambazo anazipata mtaani kwa watoto anaocheza nao. Kuwa makini kujua watoto anaocheza nao angalau ni rahisi wewe kama mzazi kufanya uangalizi wa tabia za watoto wale, tabia za watoto wa jirani ni rahisi kuchukuliwa na mtoto wako. Tabia za shule sio rahisi sana kuzifuatilia, lakini inawezeakana! Pia jua watoto wanaocheza na mwanao, ni muhimu zaidi hasa zama hizi za maradhi anuai!
Kwa wenye Computer: usikubali mtoto (wadogo) kuzoea sana keyboard: computer keyboard (kumradhi sijapata Kiswahili halisi) zinalemaza muandiko wa mtoto husika. Ni vizuri watoto kuzoea aina hii ya teknolojia lakini mzazi kuwa makini sana katika hili. Ni kweli mtoto anaweza kuwa na muandiko wa ajabu sana, na bado akawa na akili shuleni, lakini kama upo uwezekano wa kumjengea mtoto uwezo wa kuandika vizuri, basi tufanye hivo!
Wenu katika ujenzi wa taifa,
slim5.