Narudia tena kukwambia Maalim Seif

Narudia tena kukwambia Maalim Seif

Wewe endelea kupinga kwamba haiwezekani Lipumba na Maalim Seif kuzungumza.
Lakini Wasipokubali kuzungumza , ujue wataishia kugawana mbao na tofari, amini nisemacho
 
Inawezekana ni msaliti,lakini husalitiwi isipokuwa u dhaifu!je maalim ameuona udhaifu wake?usaliti hautokei from nowhere.
Unaweza kutupa udhaifu wa Bwana Yesu ulio tumia na Yuda kumsaliti? Sijui watu wengine wanafikiri kwa kutumia kitu gani!
 
Msipo kubali kujadili kiini hasa cha hili tatizo la Cuf kwa kutanguliza ushabiki wa upande flani, fahamu kwamba mnachochea kuni kwenye moto
 
Kulikuwa na mtego wa panya nyumbani kwa binadamu. Panya akamwambia kuku nisaidie kuufyatua. Kuku kasema hainihusu. Panya kawendea mbuzi , naye kakataa. Kisha akasema huu mtego utawamaliza hamjui. Wakacheka sana. Siku mtego uliponasa nyoka aliyekuwa anavizia panya, sumu ya nyoka yule ilimuua baba mwenye nyumba aligogongwa. Wageni walikuja kwenye msiba na kuanza kuchinjiwa kuku. ..........
 
Mkuu ndo maana nasema wakae mezani na kuyamaliza, kwani Wote kuna sehemu wamekosea kwa namna flani.
Yatasemwa mengi lakini tatizo ni Lowasa kujiunga na ukawa
 
Napata ukakasi na kisomo chako na elimu yako ya kupambananua mambo. Huoni Lipumba anawavuruga watu. Futa andiko lako au lekebisha.
 
Mgogoro uliopo ndani ya Cuf ni mkubwa sana.
Maalim Seif unaushawishi mkubwa ndani ya Cuf, pia fahamu kwamba Lipumba nae anaushawishi mkubwa tu kama ulivyo wewe.

Habari ya mashabiki ndani ya mitandao ya kijamii si suluhu ya kumaliza mgogoro huu.

Umesikika ukisema ni Bora uzungumze na CCM, lakini si Lipumba. Mimi nasema hapana.

Mgogoro huu Utamalizwa kwa wewe na Lipumba kukaa mezani na kujadiliana Nini kifanyike ili muendelee na ujenzi wa Chama chenu.
Shirikisheni wanataaluma mbalimbali wa masuala ya kisiasa, kisheria, kijamii na kitamaduni katika maridhiano yenu.

Wapambe walio nyuma yenu si wema hata kidogo.
Msipo kubali kukaa na kuyamaliza kwa majadiliano hakika hata patikana mshindi. Matokeo yake mnaiua CUF kwa mikono yenu wenyewe.

Mmeijenga kwa jasho na Damu nyingi za wanachama wenu lakini haya hamkumbuki hata kidogo kwa kua kuna misukumo nyuma yenu isio salama.

Namalizia kwa kusema kwamba mchawi wa CUF ni wewe Maalim Seif na Lipumba.
Mtasingizia kila kundi, kila Raia.

Kubalini kukaa mezani na kuyamaliza.
ohaaa mzeeee. lipumba sio mwanachama wa cuf upooo
 
Subiri matokeo baada ya dakika tisini ndo uje tena
 
Mtanyoosha maelezo baada ya dakika tisini.
Ndipo utaelewa nilichoshauri kwa sasa
 
Wamesalitiana baada ya Lowassa kujiunga ukawa dakika za lala salama kwa malengo yake binafsi?
 
[emoji23][emoji23][emoji23], we ni Noma
 
Mgogoro uliopo ndani ya Cuf ni mkubwa sana.
Maalim Seif unaushawishi mkubwa ndani ya Cuf, pia fahamu kwamba Lipumba nae anaushawishi mkubwa tu kama ulivyo wewe.

Habari ya mashabiki ndani ya mitandao ya kijamii si suluhu ya kumaliza mgogoro huu.

Umesikika ukisema ni Bora uzungumze na CCM, lakini si Lipumba. Mimi nasema hapana.

Mgogoro huu Utamalizwa kwa wewe na Lipumba kukaa mezani na kujadiliana Nini kifanyike ili muendelee na ujenzi wa Chama chenu.
Shirikisheni wanataaluma mbalimbali wa masuala ya kisiasa, kisheria, kijamii na kitamaduni katika maridhiano yenu.

Wapambe walio nyuma yenu si wema hata kidogo.
Msipo kubali kukaa na kuyamaliza kwa majadiliano hakika hata patikana mshindi. Matokeo yake mnaiua CUF kwa mikono yenu wenyewe.

Mmeijenga kwa jasho na Damu nyingi za wanachama wenu lakini haya hamkumbuki hata kidogo kwa kua kuna misukumo nyuma yenu isio salama.

Namalizia kwa kusema kwamba mchawi wa CUF ni wewe Maalim Seif na Lipumba.
Mtasingizia kila kundi, kila Raia.

Kubalini kukaa mezani na kuyamaliza.

alikuwa anatandikwa virungu nyakati hizo sasa analindwa..
 
Kila Raia nchi hii kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ana haki ya kulindwa ikiwemo na mali zake, fahamu hilo
 
Hapo mnapotosha uma......
Hili tatizo ni dogo sn ila linakuzwa kwa lazima na serikali kwa maslahi ya ccm CHANZO KIKUU KIKIWA ccm KUSHINDWA VIBAYA ZANZIBAR NA KUPORA SHINDI
Maalimu seif hana wafuasi ila anawanajeshi na polisi kutoka ccm......
Serikali inafanya kwa makusudi kupitia kwa msajiri kudhoofisha cuf...
MUHIMU SHERIA ZA VYAMA VYA SIASA AMBAZO SERIKALI KUPITIA KWA MSAJILI WANAKIUKA ZIFUATWE......
lipumba alijiuzuru kwa hiari yake na pi baadaye alivuliwa hadi uanachama kitu ambacho serikali inatakiwa ikiheshimu mamuzi halali ya lipumba na ya cuf.....
Marekebisho mkuu:
Parapraph ya pili, sentensi ya kwanza---"Maalim Seif hana wafuasi", hisia zinaniambia ingesomeka " Profesa Lipumba hana wafuasi".(I stand to be corrected)
 
lipumba bila kupepesa macho ndo chanzo cha mgogoro cuf. alikurupuka sana kujiuzulu.....
 
Mshauri wa propesa ni Seif Ali Idi na Shein kwa upande wa Zanzibar na kwa upande wa bara analishwa maneno kutoka kwa Mutungi na Mkulu. Sasa kweli mtu huyo ana nia njema na cuf. Lipumba ni nyapala la mkoloni.
 
hawakumwaga damu hawa hasa huyo seif, Lipumba ndiye aliyekua akipigwa kila kukicha na kina Sumaye na Mkapa. angalia katika video hii kama utamuona Seif hapo:

Hivyo umesahau kuwa mzigo mzito mtwishe mnyamwezi? Seif alimtwisha mzee mapalala alipofika anapopataka akamfukuzilia mbali na baada ya hapo akamtwisha Prof IB naye alitaka afanye kama vile alivyofanya hapo awali lakini akasahau kuwa Prof naye ni mjanja kuliko yeye.
 
Lipumba ametumwa kuanzisha huu mgogoro, sasa unataka Seif azungumze nae nini? Kuzungumza na Lipumba ni kuhalalisha hivi vituko anavyoendelea kuvifanya, na hiyo haikubaliki. Lipumba amekikosea sana chama kwa kukubali kutumika ili kukiangamiza. Mbaya zaidi, Lipumba amemkosea Mungu wake kwa kukubali kukisumbua chama ili kipoteze muda wake na yeye badala ya kupigania haki(ushindi) kilichoporwa kule Zanzibara kwenye uchaguzi wa October, 2015. Dhambi hizi hazitomuacha Lipumba salama kwani Mungu wa kweli ni mwema sana. Mh. Seif endelea na msimamo huohuo kwani upo sahihi. Kama ulivyokataa kishiriki uchaguzi wa maigizo wa March, 2016 kule Zanzibar ndio hivyohivyo unavyotakiwa kukataa kufanya mazungumzo na mtu ambaye ni dhahiri kabisa kwamba anatumika na maadui wa chama, ambao sina haja ya kuwataja.
Ni kweli kabisa Lipumba alitumwa kuanzisha mgogoro ndani ya CUF na ndiyo maana aligongwa sana virungu na askari wakati akidai haki wakati huo maalim akiwa arabuni anakunywa kahwa.
 
Hivyo umesahau kuwa mzigo mzito mtwishe mnyamwezi? Seif alimtwisha mzee mapalala alipofika anapopataka akamfukuzilia mbali na baada ya hapo akamtwisha Prof IB naye alitaka afanye kama vile alivyofanya hapo awali lakini akasahau kuwa Prof naye ni mjanja kuliko yeye.
ni kweli kabisa nakumbuka hilo naona sasa kapatikana na mhuni mwezake.
 
Unaweza kutupa udhaifu wa Bwana Yesu ulio tumia na Yuda kumsaliti? Sijui watu wengine wanafikiri kwa kutumia kitu gani!
Hilo mbona liko wazi mkuu,lile fuko la fedha alilompa kubeba (alikuwa ni mshika fedha,ref:uyatendayo yatende haraka)na lile tonge alilomlisha likiwa na roho ya uuaji ndiyo udhaifu wake.Kasome tena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom