Napinga viongozi kuitwa waheshimiwa.

Napinga viongozi kuitwa waheshimiwa.

Mkata Mtaa

Senior Member
Joined
Jun 10, 2016
Posts
136
Reaction score
143
Zama za Viongozi kutaka kuitwa waheshimiwa mimi uwa naipinga siku zote.
Kwa nini uitwe mheshimiwa badala ya ndugu kama walivyokuwa wanaitana enzi za Mwl Nyerere?!
Nashangaa wanasiasa kutamka mara kwa mara kwamba wana muenzi Mwl Nyerere wakati hawataki kuitana ndugu.
Ata ahadi kwanza ya TANU inasema binadamu wote ni ndugu na Afrika ni moja.
Hii ahadi iliwekwa maksudi kuondoa ubinafsi kati ya watawala na wananchi kujikweza na kujitukuza au miungu watu.
Na katiba ya Jumhuri ya muungano wa Tz ya 1977 ibara 12 (2) inasema kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake,
Hii ina maana kwamba watu wote ni waheshimiwa, sasa kwa nini tusiitane wote waheshimiwa?!
kwa kwangu mimi naona bora turudishe neno Ndugu maana wananchi wote kuitana waheshimiwa haiwezi leta mantiki.
Heshima inatokana na tabia njema, adabu kwa wenzio, kuthamini wenzio, mchango unaotoa kwenye jamii, ubinadamu nk. Sio kwa kuwa umechaguliwa kuwa kiongozi wakati mwingine kwa rushwa, tabia mbaya kwenye jamii nk halafu unataka kuitwa mheshimiwa,
Neno mheshimiwa linatokana na heshima uliyonayo kwenye jamii inayokuzunguka sio kuilazimisha kwa sababu wewe ni kiongozi.
Neno ambalo liko sahihi ni kuitana ndugu kwa watanzania wote, maana ata kama una matendo mabaya hawezi kufuta undugu.
Kitendo cha kukuita Ndugu Raisi, Ndugu Mbunge, Ndugu Diwani nk, kinatosha maana ndio cheo chako.
Kama Amerika wanavyoweza kumuita raisi wao. Mr. President.

Munungu ibariki Tz
 
Back
Top Bottom