Kwa mtazamo wangu hizo "flyover" hazitosaidia kivile. Tatizo la foleni Dar kweli ni sababu ya magari mengi na barabara chache, ila lazima tukubali MIPANGO ya kupunguza foleni imekuwa mibovu. Hivyo namuunga mkono mtoa thread. Pia kuna vibarabara "vidogo" vya nje kidogo ya Dar ila ni vya muhimu kweli, vingeboreshwa kwa kiwango cha lami. Mfano: barabara ya mlimani (chuoni) inayotokea Kimara Baruti, Kinyerezi road ingetakiwa ipanuliwe na itengenezwe lami mpaka Mbezi, kisha nyingine toka Kinyerezi ipite mpaka huko Pugu, chanika, mpaka mbagala, kongowe kisha Kigamboni. Yaani hizi ziwe barabara kubwa. Wenye magari wangekuwa na machaguo kadhaa ya kupita wanapoenda au kurudi makwao/ maofisini. Pia ingependeza kama mji mpya wa kisasa (maofisi), ungejengwa huko nje ya Dar mjini, yaani Kisarawe. Foleni zingepungua.