Napendekeza watu hawa waajiriwe kuleta ufanisi.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Napendekeza watu hawa waajiriwe kuleta ufanisi....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sajenti, Aug 26, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikijiuliza ni kwa kiasi gani mawaziri, manaibu waziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanavyoweza kufanya kazi zao kwa ufanisi na hatimaye kutoa tija kwa taifa. Kwa maoni yangu nimeona ni jambo hilo ni gumu kutokana na aina ya mfumo wa utumishi Tanzania, ambapo waziri ambaye mara nyingi huwa ni mbunge anayewakilisha wananchi wa jimbo lake hujikuta ameegemea zaidi katika kufanya kazi za serikali kama mmoja wa wasaidizi wa rais katika wizara husika. Hali hii hupelekea wengi wa mawaziri kujikuta wakishindwa hata kuwatumikia wapiga kura wao.Nakumbuka kuna waziri mmoja katika jimbo moja katika mkoa wa Tanga alipoenda kwenye kampeni watu walimuuliza mbona tangu tulipokuchagua hukuonekana tena mpaka miaka 5 imepita leo ndio umekuja kuomba kura zetu tena..akajitetea kuwa majukumu aliyopewa na raisi akimaanisha uwaziri yamekuwa yakimfanya akose muda wa kutembelea wapiga kura wake.....:lol:

  Hili pia lipo kwa manaibu mawaziri na wakuu wa mikoa na hasa wale wenye kofia mbili ubunge na ukuu wa mkoa. Katika mchakato wa kura za maoni tumeona pia baadhi ya wakuu wa wilaya wakijitumbukiza katika mbio za kutaka ubunge mfano Bi Betty Machangu (kasulu), Said Bwanamdogo (kondoa) na wengine.

  Nadhani badala ya viongozi hawa kuwa wa kuteuliwa na raisi wengi wamekuwa wameshindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa kukosa uwezo na sifa kwa kazi walizopewa. HIvyo basi napendekeza kuwa nafasi za mawaziri, naibu waziri, wakuu wa mikoa na wilaya ziwe zinatangazwa watu wanaomba, kusairiwa na baadaye kuajiriwa tena kwa mkataba. Na atakaposhindwa ku-deliver anatimuliwa kazi.

  Kwa njia hii kuna uwezekano mkubwa sana wa kupata watu wenye sifa na uwezo na sio kusubiri raisi ateuwe majina ya wabunge kupewa uwaziri, ukuu wa mkoa na ukuu wa wilaya matokeo yake kutuwekea watu wa ajabu ajabu.....Hebu tulijadilili hili wadau .
   
 2. s

  skeleton Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mdau naona ni good idea, ila naona kama jambo hilo halitawezekana kwani hiyo process ya kutuma maombi itachukua muda mrefu kwani itatakiwa rais akipatikana ateue viongozi hao immediately ili waendelee kuwatumikia wananchi kwa haraka na shughuli ziendelee kama kawaida. Sasa mpaka watume maombi na yachambuliwe yote na kufanya usaili hadi kupata mtu sahihi itachukua muda mrefu.
   
 3. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,470
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Tatizo maoni ya maskini huwa hayasikilizwi
   
 4. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inawezekana hata sasa hivi wakiwa kwenye kampeni wizara zinaendeshwa na makatibu wakuu labda hata kwa ufanisi zaidi,kuna nchi kama Marekani ukiteuliwa waziri unajiuzulu useneta/uwakilishi na uchaguzi mdogo kufanyika ili kwenye jimbo wapate uwakilishi unaostahili.Tumerithi mfumo huu kutoka Uingereza labda ni wakati muafaka kuubadilisha kuepuka vituko kama vya Mramba alipokuwa waziri wa mawasiliano barabara za Rombo zikapata bilioni 20 Tabora nzima ikapata milioni 200.
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hili suala tumeshaliongelea sana kwamba huwezi ukachanganya mtu wa legislation kumleta kwene executive, au kumfanya a-overlap, ni upuuzi wa hali ya juu. Vilevile tunalalmika kwamba watu wetu hawana ajira, kwanini mtu mmoja ang'ang'ane 'ajira' mbili za ubunge na uwaziri? Tunakosa creativity halafu tubakai kuangaliana machoni.

  BTW, kazi wanazofanya wabunge ni redundant, na gharama ya kumaintain bunge ni kubwa sana wakati wanachozalisha NI SUFURI. Ni bora serikali ikajikita kwene shughuli za uzalishaji badala ya kutii kiu za siasa njaa.,.hatutoendelea kamwe tukiendelea na utaratibu wa sasa.
   
Loading...