Napenda uendeshaji wa IG Page ya Burna Boy

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,792
15,693
Niliwahi kusikia mtandao wa kijamii pekee anaoingia huyu jamaa ni WhatsAPP, mitandao mingine kuna watu maalumu wanaicontrol, nampa hongera admin wa IG page yake, ukiingia kwenye page yake utaona upekee tofauti na page za mastaa wengine wa Africa, it's very professional.

Hutaona sijui vijembe, birthday wishes, na upuuzi mwingine, yeye anaweka kazi tu na tarehe za show, kama akiweka picha ya show/clip basi ni moja tu, hapa bongo kina Diamond, Harmonize, n.k wakifanya show moja kubwa basi tutawekewa clip 20 na vijembe juu, sijui ushamba wa show,

kila wimbo wakitoa wanaweka clip 50 za mashabiki wakicheza, yaani ukikaa wiki ujaingia kwenye page zao unakutana na post 100 mpya, hivi tunakwama wapi jamani?
Screenshot_20191204-150440.jpeg
 
Donald Trump pamoja kuwa rais wa taifa kubwa muda wote yupo Twitter,kwa nini asiweke mtu wa kuiendesha?kaa siku tatu alafu ingia IG ya Chris Brown uone,wakina Sanchez wanapost mpaka mbwa inakuwa ajabu mtu kupost birthday??kila mtu na lifestyle yake aliyoichagua tuache kupangia watu namna ya kuishi kwa ku refer wengine wanavyoishi!!
 
Kwahiyo Mond akitoa Kazi kuipa promo kwakutuma clip na huyu anatoa kazi then anabunda unaona professional ni anayebunda.

Hao wakina brown wote ni wajinga.
Kama kazi ni nzuri inaenda tu, kwani nani aliyetoboa zaidi hapo?
 
Jamaa yupo active sana, hata wakati wa kuwania tuzo za Mtv ema mmakomde alihangaika mno lakini jamaa halikuwahi kupost ila na tuzo likachukua
 
Jibu swali
Huna hoja zinazoeleweka kinaendeleo

Sasa kazi mzuri inakubalika tu bila boost sasa kwakukubalika bila boost uki-boost pia sindio vizuri zaidi hauna hoja inayoeleweka kusifu hiyo page ni page ya kijinga ambayo ulipaswa kuikosoa kwa ulimwengu wa sasa.

Ndio maana nime conclude unasifu ujinga hii karne ushindani then asiyeenda na ushindani unamsifu ujinga.
 
Niliwahi kusikia mtandao wa kijamii pekee anaoingia huyu jamaa ni WhatsAPP, mitandao mingine kuna watu maalumu wanaicontrol, nampa hongera admin wa IG page yake, ukiingia kwenye page yake utaona upekee tofauti na page za mastaa wengine wa Africa, it's very professional.

Hutaona sijui vijembe, birthday wishes, na upuuzi mwingine, yeye anaweka kazi tu na tarehe za show, kama akiweka picha ya show/clip basi ni moja tu, hapa bongo kina Diamond, Harmonize, n.k wakifanya show moja kubwa basi tutawekewa clip 20 na vijembe juu, sijui ushamba wa show,

kila wimbo wakitoa wanaweka clip 50 za mashabiki wakicheza, yaani ukikaa wiki ujaingia kwenye page zao unakutana na post 100 mpya, hivi tunakwama wapi jamani?View attachment 1281560
watumiaji wote wa IG bongo kaonekana Diamond na harmonize tu? wabongo kwa nongwa hatujambo
 
Sio wetu huku sisi nyimbo ikifikisha 1m views anascreenahot anapost , kuna siku diamond alipost screenshot ya chat zake wassap nikaona huyu jamaa vipi
 
Burna Boy siyo mpenzi wa kutumia mitandao ya kijamii, alishaliweka wazi hilo, na inajulikana hivyo.
Asilaumiwe kwa chochote, kama unafanya kazi nzuri, itasambaa tu hata usipoisambaza wewe!
Endelea kujifunza kuhusu MARKETING. Kama unadhani kufanya kazi nzuri tu kunatosha jiulize kwa nini makampuni makubwa yanawekeza fedha nyingi kwenye marketing wakati yanajulikana na yanazalisha products nzuri ambazo nazo zinajulikana lakini bado wanazitangaza.

So usimuone diamond ku promote kazi zake kupitia Instagram ukamuona mshamba. That is part of marketing plans zake....na hiyo mitandao imemsaidia kufika hapo alipo.

Kwa hiyo kama Burna boy hatumii mitandao kama Insta kujipromote ni yeye....na ana plans zake za kujitangaza ambazo ni tofauti na wengine.

Zile clips ambazo unaona diamond anapost akiwa na umati wa watu wengi ni advertisement na imemsaidia sana. Maana mashibiki wanataka contents na yeye anawapa wanachotaka.
 
Jamaa anasifu ujinga then anatuaminisha uwo ujinga anaofanya uyo Burna boy ndio professional.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom