Napenda kujua hatua za kulitoa gari bandarini

Habari wakuu naombeni kuuliza je kwa mfano nikawa nimeagiza gari yangu toka nje na imefika bandali ya Dar. Vipi kuhusu ghalama na process zakulitoa gari zinakuaje?
Mkuu kama bado hujafanikiwa tuwasiliane nikuunganishe na mtu anaofisi yake ndiyo inayofanya kazi hizo
 
Tafuta Clearing Agent atakusaidia kulitoa gari bandarini ,ila chagua wenye uzoefu maana ukimpata mvivu anaweza akakuingiza kwenye STORAGE,hakikisha ndani ya siku 7 tangu litue bongo uwe ushalitoa kinyume na hapo utaanza kupigwa STORAGE ambayo gharama zake inategemea na size(CBM) ya gari.
 
Attachments

  • Screenshot_20210301-211003.png
    Screenshot_20210301-211003.png
    74.8 KB · Views: 10
  • Screenshot_20210301-211032.png
    Screenshot_20210301-211032.png
    86.3 KB · Views: 10
  • Screenshot_20210301-211052.png
    Screenshot_20210301-211052.png
    94.2 KB · Views: 9
hizo process hazikuhusu, wewe tafuta hela wape document na hela kampuni ya clearing wakukabidhi gari

Hili ndilo jibu gani sasa? Nadhani ungenyamaza tu bila kuandika hiki, ingefaa sana...

Hata kama anawapa jamaa wa C & F, naye anapaswa kujua basics za process hizo...

Ndiyo maana kauliza...
 
Habari wakuu naombeni kuuliza je kwa mfano nikawa nimeagiza gari yangu toka nje na imefika bandali ya Dar. Vipi kuhusu ghalama na process zakulitoa gari zinakuaje?
Here is the process;

1. Chagua gari yako unayotaka kununua toka kampuni yoyote online. Usione soni kushirikisha rafiki, jamaa au ndugu mzoefu anayejua kufanya haya mambo. Don't pretend you know kumbe you don't or you know just a little...

Kuna jamaa yangu mwaka 2012 alijifanya anajua. Akanunua gari toka Japani aina ya Honda CR -V kwa dola 4,000 sawa na Tshs 8,000,000 wakati huo. Gari ikafika nchini vizuri kabisa bandarini DSM. Akashindwa kuikomboa bandarini kwa sababu alidhani ndiyo amemaliza. Hakujua kuwa kuna kodi na tozo za TRA karibu au zaidi ya Tshs. 9,000,000 tens...!

Unajua kulitokea nini? Ilimlazimu kuuza gari hilo hapo hapo bandarini chini ya Tshs. 5,000,000 kwa wajanja....!!

2. Watakupatia kitu kinaitwa "QUOTATION OF PRICE FORM & PROFORMA INVOICE" ikionesha gharama ya gari lenyewe (FOB) na gharama za usafirishaji + insurance (CARGO IN FREIGHT a.k.a CIF). CIF ni gharama ya gari lenyewe + transportation from the original country to the destination country ktk bandari uliyochagua wewe kupokelea gari yako..

3. Ukishapokea hiyo fomu ya bei ya gari (quotation form & proforma invoice), fanya utaratibu wa kwenda kulipia gari yako aidha kupitia benki au njia zingine zozote za kufanya malipo kwa kadiri utakavyoelekezwa na kampuni inayokuuzia gari yako...

4. Ukishakamilisha kulipia gari yako huko, utaratibu wa kusafirishiwa gari yako mpaka bandari utakayoipokelea gari yako hufanyika mara moja. Kwa Tanzania mara nyingi ukiagiza gari popote iwe Marekani au Ulaya au Asia hususani Japan, Korea au Uchina, huchukua muda wa Sikh kati ya 45 na 90 kufika bandari ya Dar...

5. Mpaka hatua hiyo, unakuwa umeshanunua gari tayari. Lakini haiwezi kuruhusiwa kuwa barabarani hata itakapokuwa imefika bandarini mpaka uhakikishe umelipia kodi na tozo zingine zote za serikali ndipo utaruhusiwa kuondoka na gari yako. Kwa hiyo hatua ya tano ni hii...

5. Chukua hati ulizonunulia gari yako, nenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Waoneshe nyaraka za ununuzi wa gari yako, kisha watakukokotelea kodi na tozo zingine zote za gari yako ikiwemo gharama ya usajili (Registration) ya gari yako hapa nchini Tanzania...

Ukishapewa gharama hizo, nenda benki lipia na tunza nyaraka hizo zote ulizofanyia malipo ya gari + TRA...

6. Subiri gari yako ifike. Ikifika bandarini, pokea gari yako. Ikatie Bima na Stika ya usalama barabarani. Kisha start enjoying driving...

MUHIMU na ZINGATIA HILI:

å Kama siyo mzoefu au hujawahi kuagiza gari mwenyewe moja kwa moja toka nje ya nchi, usije ukajiingiza kichwa kichwa kujifanya unaelewa bila kupitia kwa mtu mzoefu na unayemwamini....

Kuna matapeli wabobezi wa kimataifa wako kwenye sekta hii na huwaliza watu wengi sana kila siku. Be careful & intelligent before you go...

å Kwa usalama wa fedha zako na kuwa na uhakika wa kupata gari yako, ni vyema sana ukatumia fedha zaidi kidogo kwa kuwapa na ukawawatumia mawakala wabobezi na wazoefu wa kuagiza magari toka nje wafanye kazi hiyo kwa niaba yako. They are so good kiasi ambacho watakuletea gari yako mpaka nyumbani kwako ukitaka...

However, napo pia kuwa makini. Maana ziko kampuni zingine za uwakala wa uagizaji magari hapa hapa nchini zina watu wasio waaminifu ambayo wanaweza kukutapeli vilevile...

Shirikisha watu wazoefu watakuongoza..

ASANTE..
 
Model ni hiyo TA-ACA21W... So kule TRA angalia model inayofanania herufi hizo kwa umakini ila sio lazima ifanane kwa asilimia 100% kule tra wamekata baadhi ya herufi hawaandiki complete model.
Hivi mkuu nikitaka kujifunza models za gari naweza kuzipata wapi?Mfano nataka nijifunze models zote za RAV4 ila nimekomaa na google nimetoka kapa!
 
Hivi mkuu mwaka ni huo registration year au ni huo manufactured year?
043337.jpg
 
Mkuu umeandika vizuri na kwa urefu, ila kuna mapungufu.

1. Si lazima aende TRA, anaweza angalia makadirio ya kodi kwanza online aandae hicho kiasi cha pesa.

2. Wakala wa forodha ni lazima siyo hiyari na TRA Malipo yanalipwa na wakala wa forodha, TPA, na shipping line kote huko invoice anapewa wakala wa forodha,
Kingine port charges zinatoka baada ya meli kufika, hivyo siyo sahihi umwambie alipie mapema,

Cha msingi awe na hicho kiasi cha pesa mapema.

Wewe umeandika kama anaweza pambana mwenyewe vile.

Cha msingi ni atafute wakala mwaminifu na mwenye uzoefu,

Hapa kwa wakala ndo anaweza ingizwa mkenge na wale wa kugongesha. (Though kama ni makini hata wa kugongesha anatoa.)

Baada ya meli kufika hizo process zinachukua siku 2 had 3.

Kumbuka gari likikaa siku 7 baada ya kushuka melini storage charges zinaanza.
 
hizo process hazikuhusu, wewe tafuta hela wape document na hela kampuni ya clearing wakukabidhi gari
saw mkuu je unaemza nisaidia mwongozo kidogo mfano kwaioapo paso
Screenshot_20210302-183337_Chrome.jpg
Screenshot_20210302-183340_Chrome.jpg
 
Attachments

  • Screenshot_20210302-115540_Chrome.jpg
    Screenshot_20210302-115540_Chrome.jpg
    36 KB · Views: 7
Here is the process;

1. Chagua gari yako unayotaka kununua toka kampuni yoyote online. Usione soni kushirikisha rafiki, jamaa au ndugu mzoefu anayejua kufanya haya mambo. Don't pretend you know kumbe you don't or you know just a little...

Kuna jamaa yangu mwaka 2012 alijifanya anajua. Akanunua gari toka Japani aina ya Honda CR -V kwa dola 4,000 sawa na Tshs 8,000,000 wakati huo. Gari ikafika nchini vizuri kabisa bandarini DSM. Akashindwa kuikomboa bandarini kwa sababu alidhani ndiyo amemaliza. Hakujua kuwa kuna kodi na tozo za TRA karibu au zaidi ya Tshs. 9,000,000 tens...!

Unajua kulitokea nini? Ilimlazimu kuuza gari hilo hapo hapo bandarini chini ya Tshs. 5,000,000 kwa wajanja....!!

2. Watakupatia kitu kinaitwa "QUOTATION OF PRICE FORM & PROFORMA INVOICE" ikionesha gharama ya gari lenyewe (FOB) na gharama za usafirishaji + insurance (CARGO IN FREIGHT a.k.a CIF). CIF ni gharama ya gari lenyewe + transportation from the original country to the destination country ktk bandari uliyochagua wewe kupokelea gari yako..

3. Ukishapokea hiyo fomu ya bei ya gari (quotation form & proforma invoice), fanya utaratibu wa kwenda kulipia gari yako aidha kupitia benki au njia zingine zozote za kufanya malipo kwa kadiri utakavyoelekezwa na kampuni inayokuuzia gari yako...

4. Ukishakamilisha kulipia gari yako huko, utaratibu wa kusafirishiwa gari yako mpaka bandari utakayoipokelea gari yako hufanyika mara moja. Kwa Tanzania mara nyingi ukiagiza gari popote iwe Marekani au Ulaya au Asia hususani Japan, Korea au Uchina, huchukua muda wa Sikh kati ya 45 na 90 kufika bandari ya Dar...

5. Mpaka hatua hiyo, unakuwa umeshanunua gari tayari. Lakini haiwezi kuruhusiwa kuwa barabarani hata itakapokuwa imefika bandarini mpaka uhakikishe umelipia kodi na tozo zingine zote za serikali ndipo utaruhusiwa kuondoka na gari yako. Kwa hiyo hatua ya tano ni hii...

5. Chukua hati ulizonunulia gari yako, nenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Waoneshe nyaraka za ununuzi wa gari yako, kisha watakukokotelea kodi na tozo zingine zote za gari yako ikiwemo gharama ya usajili (Registration) ya gari yako hapa nchini Tanzania...

Ukishapewa gharama hizo, nenda benki lipia na tunza nyaraka hizo zote ulizofanyia malipo ya gari + TRA...

6. Subiri gari yako ifike. Ikifika bandarini, pokea gari yako. Ikatie Bima na Stika ya usalama barabarani. Kisha start enjoying driving...

MUHIMU na ZINGATIA HILI:

å Kama siyo mzoefu au hujawahi kuagiza gari mwenyewe moja kwa moja toka nje ya nchi, usije ukajiingiza kichwa kichwa kujifanya unaelewa bila kupitia kwa mtu mzoefu na unayemwamini....

Kuna matapeli wabobezi wa kimataifa wako kwenye sekta hii na huwaliza watu wengi sana kila siku. Be careful & intelligent before you go...

å Kwa usalama wa fedha zako na kuwa na uhakika wa kupata gari yako, ni vyema sana ukatumia fedha zaidi kidogo kwa kuwapa na ukawawatumia mawakala wabobezi na wazoefu wa kuagiza magari toka nje wafanye kazi hiyo kwa niaba yako. They are so good kiasi ambacho watakuletea gari yako mpaka nyumbani kwako ukitaka...

However, napo pia kuwa makini. Maana ziko kampuni zingine za uwakala wa uagizaji magari hapa hapa nchini zina watu wasio waaminifu ambayo wanaweza kukutapeli vilevile...

Shirikisha watu wazoefu watakuongoza..

ASANTE..
aaante sana mkuu nashikul kwailo
 
Hivi mkuu nikitaka kujifunza models za gari naweza kuzipata wapi?Mfano nataka nijifunze models zote za RAV4 ila nimekomaa na google nimetoka kapa!
Jaribu youtube iko vizuri zaidi kuna model za rav 4 hadi za 1998 zipo huko pia usiangalie gari ya kila mwaka kuna gari ambazo zilifanyiwa mabadiliko makubwa. Mfano rav 4 zipo model kama Generation 5 ambazo ndo zimefanyiwa major changes kimuundo na kimfumo ndo ambazo unatakiwa uangalie sana. Ndio ambazo unakuta TRA wameamua kuzitofautisha maana ni rav 4 jina tu ila hazifanani mazima.
 
Back
Top Bottom