Napenda kujua hatua za kulitoa gari bandarini

deal na registraton year ndo mwaka gari ilikua imeingia road.
Mkuu hii nimeitoa beforward.Hivi hapa vitu vilivyopo kwenye gari ni hivyo vyenye rangi ya orange au ni hivyo vyenye white iliyofifia?Yaani kwa mfano gari hii ina CD player au haina?
043412.jpg
 
Nafikiri changamoto yangu ni kwenye kujaza model.Kwenye website ya beforward hizi model ninazipata sehemu gani?
Model number unayoitaka mfano kwenye hii Subaru ni hiyo GH2. Kila model ya gari ina namba zake, angalia hapo utaziona, na pia utaziona zikifanana na za kwenye site ya TRA.
Screenshot_20210303-232417_1.jpg

Screenshot_20210303-232417_1.jpg
 
Mkuu umeandika vizuri na kwa urefu, ila kuna mapungufu.

1. Si lazima aende TRA, anaweza angalia makadirio ya kodi kwanza online aandae hicho kiasi cha pesa.

2. Wakala wa forodha ni lazima siyo hiyari na TRA Malipo yanalipwa na wakala wa forodha, TPA, na shipping line kote huko invoice anapewa wakala wa forodha,
Kingine port charges zinatoka baada ya meli kufika, hivyo siyo sahihi umwambie alipie mapema,

Cha msingi awe na hicho kiasi cha pesa mapema.

Wewe umeandika kama anaweza pambana mwenyewe vile.

Cha msingi ni atafute wakala mwaminifu na mwenye uzoefu,

Hapa kwa wakala ndo anaweza ingizwa mkenge na wale wa kugongesha. (Though kama ni makini hata wa kugongesha anatoa.)

Baada ya meli kufika hizo process zinachukua siku 2 had 3.

Kumbuka gari likikaa siku 7 baada ya kushuka melini storage charges zinaanza.
Wakala wa forodha si lazima. Serikali ilibadili sheria ya wakala wa forodha na kuruhusu watu binafsi kuchukua mzigo bandarini bila ulazima wa wakala wa forodha. Kutumia wakala ni hiyari yako na sio lazima.
 
Gari ya beyond 10yrs since date ya manufacture, inachajiwa kodi 2 yaani excise duty ya kawaida kwa kila gari (mpya or old) na pia excise duty on age (to discourage import of old vehicle to United Republic) all in all, to clear your import (any) from the port (airport au bandarini) you have to do it via a 'clearing and forwarding agent) ,this is a legal requirement. Otherwise bandarini kungekuwa kama stand ya ubungo asubuhi

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Kutumia wakala wa forodha sio lazima. Serikali ilibadili sheria na kuondoa ulazima wa mtu kutumia clearing and forwarding agent. Sio lazima ukitaka unatoa gari yako mwenyewe.
 
Mkuu umeandika vizuri na kwa urefu, ila kuna mapungufu.

1. Si lazima aende TRA, anaweza angalia makadirio ya kodi kwanza online aandae hicho kiasi cha pesa.

2. Wakala wa forodha ni lazima siyo hiyari na TRA Malipo yanalipwa na wakala wa forodha, TPA, na shipping line kote huko invoice anapewa wakala wa forodha,
Kingine port charges zinatoka baada ya meli kufika, hivyo siyo sahihi umwambie alipie mapema,

Cha msingi awe na hicho kiasi cha pesa mapema.

Wewe umeandika kama anaweza pambana mwenyewe vile.

Cha msingi ni atafute wakala mwaminifu na mwenye uzoefu,

Hapa kwa wakala ndo anaweza ingizwa mkenge na wale wa kugongesha. (Though kama ni makini hata wa kugongesha anatoa.)

Baada ya meli kufika hizo process zinachukua siku 2 had 3.

Kumbuka gari likikaa siku 7 baada ya kushuka melini storage charges zinaanza.
Asante kwa nyongeza na masahihisho. I agree with you...
 
Kutumia wakala wa forodha sio lazima. Serikali ilibadili sheria na kuondoa ulazima wa mtu kutumia clearing and forwarding agent. Sio lazima ukitaka unatoa gari yako mwenyewe.
Exactly...

Ndiyo maana serikali imeweka utaratibu mzuri Wa kiasi ambacho mtu anaweza kununua gari kwa kutumia viganja vya mikono yake tu kwa sababu gharama zote za bei ya Gari, ushuru Wa bandari, kodi za TRA nk nk mpaka gari kufika mkononi mwa mtu ziko wazi online 24hrs..

Kwa maana kuwa, mtu anaweza kulipia kila kitu i.e gari yenyewe, gharama za kulisafirisha, tozo za serikali zote na za bandari kwa kutumia simu au PC yake comfortably while seated home bila kumtumia mtu Wa tatu (wakala)...

Hii haina maana kuwa mawakala hawana maana au umuhimu. Hawa ni wazuri, wazoefu, wanazijua fitna za bandarini na za sekta hii kwa ujumla na hivyo wanasaidia sana especially kwa wateja au watu wasio wajuzi na wazoefu Wa kuagiza Magari toka nje ya nchi...
 
Here is the process;

1. Chagua gari yako unayotaka kununua toka kampuni yoyote online. Usione soni kushirikisha rafiki, jamaa au ndugu mzoefu anayejua kufanya haya mambo. Don't pretend you know kumbe you don't or you know just a little...

Kuna jamaa yangu mwaka 2012 alijifanya anajua. Akanunua gari toka Japani aina ya Honda CR -V kwa dola 4,000 sawa na Tshs 8,000,000 wakati huo. Gari ikafika nchini vizuri kabisa bandarini DSM. Akashindwa kuikomboa bandarini kwa sababu alidhani ndiyo amemaliza. Hakujua kuwa kuna kodi na tozo za TRA karibu au zaidi ya Tshs. 9,000,000 tens...!

Unajua kulitokea nini? Ilimlazimu kuuza gari hilo hapo hapo bandarini chini ya Tshs. 5,000,000 kwa wajanja....!!

2. Watakupatia kitu kinaitwa "QUOTATION OF PRICE FORM & PROFORMA INVOICE" ikionesha gharama ya gari lenyewe (FOB) na gharama za usafirishaji + insurance (CARGO IN FREIGHT a.k.a CIF). CIF ni gharama ya gari lenyewe + transportation from the original country to the destination country ktk bandari uliyochagua wewe kupokelea gari yako..

3. Ukishapokea hiyo fomu ya bei ya gari (quotation form & proforma invoice), fanya utaratibu wa kwenda kulipia gari yako aidha kupitia benki au njia zingine zozote za kufanya malipo kwa kadiri utakavyoelekezwa na kampuni inayokuuzia gari yako...

4. Ukishakamilisha kulipia gari yako huko, utaratibu wa kusafirishiwa gari yako mpaka bandari utakayoipokelea gari yako hufanyika mara moja. Kwa Tanzania mara nyingi ukiagiza gari popote iwe Marekani au Ulaya au Asia hususani Japan, Korea au Uchina, huchukua muda wa Sikh kati ya 45 na 90 kufika bandari ya Dar...

5. Mpaka hatua hiyo, unakuwa umeshanunua gari tayari. Lakini haiwezi kuruhusiwa kuwa barabarani hata itakapokuwa imefika bandarini mpaka uhakikishe umelipia kodi na tozo zingine zote za serikali ndipo utaruhusiwa kuondoka na gari yako. Kwa hiyo hatua ya tano ni hii...

5. Chukua hati ulizonunulia gari yako, nenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Waoneshe nyaraka za ununuzi wa gari yako, kisha watakukokotelea kodi na tozo zingine zote za gari yako ikiwemo gharama ya usajili (Registration) ya gari yako hapa nchini Tanzania...

Ukishapewa gharama hizo, nenda benki lipia na tunza nyaraka hizo zote ulizofanyia malipo ya gari + TRA...

6. Subiri gari yako ifike. Ikifika bandarini, pokea gari yako. Ikatie Bima na Stika ya usalama barabarani. Kisha start enjoying driving...

MUHIMU na ZINGATIA HILI:

å Kama siyo mzoefu au hujawahi kuagiza gari mwenyewe moja kwa moja toka nje ya nchi, usije ukajiingiza kichwa kichwa kujifanya unaelewa bila kupitia kwa mtu mzoefu na unayemwamini....

Kuna matapeli wabobezi wa kimataifa wako kwenye sekta hii na huwaliza watu wengi sana kila siku. Be careful & intelligent before you go...

å Kwa usalama wa fedha zako na kuwa na uhakika wa kupata gari yako, ni vyema sana ukatumia fedha zaidi kidogo kwa kuwapa na ukawawatumia mawakala wabobezi na wazoefu wa kuagiza magari toka nje wafanye kazi hiyo kwa niaba yako. They are so good kiasi ambacho watakuletea gari yako mpaka nyumbani kwako ukitaka...

However, napo pia kuwa makini. Maana ziko kampuni zingine za uwakala wa uagizaji magari hapa hapa nchini zina watu wasio waaminifu ambayo wanaweza kukutapeli vilevile...

Shirikisha watu wazoefu watakuongoza..

ASANTE..
Mkuu una maelezo mazuri sana

Kwa kuongezea, SBT na Befoward wana branch zao hapa Dar es salaam so hata ukiwatumia wale hakuna kinachoharibika, kuliko mtu kuhangaika na huna ufahamu wa hivi vitu
 
Mkuu hii nimeitoa beforward.Hivi hapa vitu vilivyopo kwenye gari ni hivyo vyenye rangi ya orange au ni hivyo vyenye white iliyofifia?Yaani kwa mfano gari hii ina CD player au haina?
View attachment 1716308
Vyenye orange ndizo accessories zilizoko kwenye gari yako, hizo fainted ni kuwa hamna japo saa ingine inaweza kuonekana hivo while zingine zinafanya kazi

Kazi kwako churaaa
 
Habari wakuu naombeni kuuliza je kwa mfano nikawa nimeagiza gari yangu toka nje na imefika bandali ya Dar. Vipi kuhusu ghalama na process zakulitoa gari zinakuaje?
Process ni vema ukatutafuta sisi mawakala(clearing agent) ambao makampuni yetu yamesajiliwa na TRA pamoja na TPA. Inachukua siku 2 mpaka 3 kukamilisha process za kugomboa gari bandarini.
Gharama ziko kwenye makundi matatu (4) kama ifuatavyo;
A. Ushuru wa TRA: hapa ushuru utategemea na taarifa za gari husika.
B. Gharama za Bandari (Port Charges)
1. Handling: ambayo hutozwa $7 jumlisha VAT kwa CBM moja (Urefu x Upanax Kimo).
2. Wharfage charges: hutozwa 1.6% jumlisha VAT ya thamani ya gari (CIF value).
3.Corridor Levy: hutozwa $0.3 jumlisha VAT kwa CBM moja.
C. Gharama za Uwakala wa Meli (TASAC Fee): hutozwa $2.5 kwa CBM moja.
D. Gharama za Ukaguzi wa TBS (Destination Inspection charges): hutozwa $150 kama Inspection fee na TZS30,000 ikiwa ni service fee.
Mwisho mkuu ni ada uwakala, karibu katika yangu itakutoza Laki Mbili Tu (200,000). Napatikana kwa aniani ifuatayo;
Ruaha Freight Ltd,
Samora Avenue,
NHC building (between Samora House & Exim Bank),
Dar es Salaam.
Mob: 0718 866 651 (Whatsap or Call)
 
Back
Top Bottom