Napenda kujiunga na madereva wa IT

Wakuu habali za leo nilikuwa naomba kwa mwenye kuwa na connection ya watu wa magari ya it msaada jamani napenda kujiunga katika kazi hiyo
Sio kazi nzuri sana basi sometimes kunakuwa hakuna option. Hata mojawapo katika wale makomandoo baada ya kuachishwa alifanya udereva wa IT hadi alipopata kazi iliyo bora zaidi akaachana na IT. Tujifunze kwa waliotangulia.
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako
 
Kama huko DAR, Nenda pale posta karibu na jengo la nssf zamani ukianza kuulizia pale utapata mwaga kidogo. Au nenda mataa ya chang’ombe jirani na kituo cha mafuta cha oilcom ukiianza kuulizia pale utapata mwaga.
Ahsante sana nimefanikiwa kufika katika maeneo ya mataa ya chang'ombe jirani na kituo cha mafuta cha oil com lakini madereva waliopo pale wengi hawana lugha nzuri hila nitafika pia apo posta majibu nitakayo pata apo pia nitatoa mrejesho shukran sana
 
Hili ndilo tatizo letu watanzania wengi tuna kuwa na roho za kichawi chawi tu!!yaani ukimkuuliza mtu utaratibu wa kupata kazi sehemu alipo yeye, ni wachache sana wanaoweza kukupa muongozo, yeye anajua kuwa labda utafanikiwa yeye atoke hapo!!na ndio maana hata huko ulaya , utakuta mataifa mengine kama kenya, nigeria na nchi nyingi za west afrika wanapeana michongo , tu, lakini wabongo ataanza kukutisha, ohh hata mimi unajua maisha ya huku yamenishinda nataka nirudi tu home, wewe bora ukomae tu huko huko, huku ni hatari kwa maisha yako,
Hayo niliyakuta DRC, yaani watanzania wenzako wanakupiga fitina hadi wacongo ndio wanaingilia kutaka kukutetea!!!kisa umepeleka bidhaa kama zao sokoni!!!ila watu wa kigoma (waha)mungu anawaona!!!
 
Back
Top Bottom