Napenda kufanya biashara ila sijapata muuzaji mwaminifu

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,774
3,460
Wakuu habari za majukumu ya kutwa mzima.

Mimi ni kijana wa kiume (31) nina ham ya kutaka kufanya biashara lakini kila ninae muamini na kumuachia mtaji anakula mazima yaani mpaka nashindwa kumuamini tena mtu yeyote hata kama hana nia mbaya na mimi.

* Wa kwanza tulikubaliana biashara fulani nikampa mtaji wa laki 4 lakini hadi leo sikuona mtaji wala faida.

* Wa pili na yeye nilimpa laki 5 na yeye hadi leo sikuona faida wala mtaji.

* Wa tatu na yeye nilimpa laki 3 lakini alijiongezea yeye kwenye biashara zake yeye nilimbana akarudisha pesa zangu.

Sasa hapa nilipo nimekaa nawaza tena nianzishe biashara lakini kuna mdau mmoja alinambia ni bora utoe vitenge Kigoma na kuleta Dar aidha kwa cash au mkopo.
Iwapo kama wateja watakua waaminifu ( wa mkopo).

Ila changamoto iliyopo ni kukosa mtu mwaminifu wa kutoa kule na kuleta sehemu husika.
Napenda kusaidia mtu kwa njia kama kama hiyo ili na yeye apate chochote lakini watu wa sasa hawafadhiliki.

Hapa nilikua nataka nitoe fursa ya shilingi laki 5 ya kuanzia lakini ndo mpaka sasa naumiza kichwa nani nimpe afanye hiyo biashara.
Kazi yake aende akavichukuwe na kuja navyo Dar.
Kama hana wenyeji atakua analala guest gharama juu yangu ilimradi vyuma vilegee.

Sasa wakuu nimeona nije hapa nipate ushauri wowote kwenu maana hapa pana watu wana maoni ya mbali kuliko hata mitaani.
Na pia najua kuna watu watabeza ila mnaruhusiwa ila siruhusu matusi tu......karibuni.
 
Ingia mkataba na mtu au tumia ndugu zako kabisa tena wa ndani kabisa eg mke na hata mdogo wako nawe utafanikiwa, nje ya hapo utateseka sana

Walinifanya hivyo vijana wawili nikamweka mke wangu sasa mambo ni murua japo waliniliza karibu 2.3 milions
Nashukuru moyo umetulia
 
Mkuu hayo mawazo tayari nilishawahi kufikiria, nipo na mdogo wangu wa kuzaliwa ila hataki kabisa shida ye anataka akae kwenye kiti azunguke kama boss.
Baba aliwahi kumpatia nafasi ya kwenda JKT aliamua kurudi hata mafunzo hayajaanza.
Kwa ufupi ni mvivu wa kutupwa lakini angefaidi matunda yangu.
 
  • Thanks
Reactions: Obe

Kwahiyo yupo tu kwako amekaa bila kazi?
 
Hapana hakai kwangu anakaa kwa baba ndo anakodeka.
Ww kama mkubwa wake yakupasa umfundishe adabu. Timua huko aliko kwa baba mwambie atafute kazi afanye sio anakaa tu anabweteka. Kumbuka saizi anadeka kwa baba akitoka hapo atakuja kudeka kwako. Shauri yako mtakuja nuniana kwa mbeleni msipo ziba ufa.
 
Sina uwezo wa kumfukuza maana anakaa baba sio kwangu Ba istoshe kitu kibaya zaidi kaowa juzi hana hata kazi za kufanya analishwa nyumbani huku nikitegemewa na mimi nnachotuma ndo aunganishie hapo hapo.
Ila kuna siku nilishakataa tangia siku aliyotafuta sababu ya kurudi JKT hadi leo sina ham nae.
Namsaidia kwasababu dam ni mzito kuliko maji lakini yamenifika shingoni maana anajua kunipangia matumizi ya pesa zangu ila yeye kazi hataki.
 
Back
Top Bottom